Swali Butu: Mambo haya 4 Magufuli anayafanya tofauti na Marais 3 waliomtangulia! Nani anabisha?

Na. M. M. Mwanakijiji

Yote tisa, kumi tuseme ukweli. Kuna mambo ambayo mtu anaweza kuamua kuyachukia dhidi ya Rais Magufuli. Mtu anaweza kuamka na kuapa kwa jina la miungu na mababu zake ya kwanini hataki kulisikia jina la Rais Magufuli. Tena mtu anaweza akaamka hata usiku wa manane kama mtu aliyepatwa na jinamizi akiwa na hofu ya Magufuli. Siwezi kuwasemea wale ambao wakisikia jina la Rais Magufuli wanaweza kujihisi pumzi zinawaisha na kujisikia unyonge. Umpende au umchukie Rais Magufuli bado anaonekana kugawa hisia za watu mbalimbali tena kwa ukali sana; ama unamkubali au unamkataa; hakuna upande wa katikati.

Na wapo pia ambao wanaposikia jina la Magufuli kwao wanajisikia matumaini, faraja, na wengine wanakuwa kama yule mwanamuziki aliyeimba wimbo wa “Magufuli Raha Tu”. Hawa wanaposikia jina la Rais Magufuli ni kama wanapata Amani ya huko mbeleni, wanajua nchi iko salama na kuwa wao na watoto wao wanashuhudia mambo ambayo labda hayakudhaniwa kuwa yanaweza kutokea katika nchi hii hii ya Waafrika tena miongoni mwa zile nchi zilizokubali jina la “Maskini Zaidi” duniani. Kwa hawa ukitaja jina la Magufuli hata ukiwaamsha usingizini wengine wanaweza kuhisi ni kama unawakatisha zile ndoto tamu tamu zinazoweza kumfanya mtu ajikute anatafuna mto akidhania ni keki!

Vyovyote vile ilivyo kuna mambo manne ambayo naweza kuyasema kwa ufupi tu ambayo Rais Magufuli anayafanya tofauti sana na viongozi wengine. Bila ya shaka kuna mengine anayafanya ambayo yanafanana na watangulizi wake na kubwa katika hayo ni ile hali ya kutukuza chama chake na kukifanyia kila namna ya msaada na mbinu ya kutaka kiendelee kubakia madarakani kwa miongo mingi ijayo. Sidhani kama kuna kiongozi atakayekuja kutoka CCM ambaye atafikiria au kujaribu kufanya kinyume cha hilo. Hata hivyo, binafsi ningependa kudokeza yale mambo ya kiutendaji (executive) ambayo Rais Magufuli anayanya – kwa maoni yangu – kwa namna tofauti na viongozi watatu waliomtangulia.

1. Dhana ya Kujitegemea Ameipa Magurudumu
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati anaikaripia serikali ya Rais Mkapa kufuatia ile sera ya “ubinafsishaji wa mashirika ya umma” na ile hali ya kujaribu kuendekeza sana “wawekezaji wa nje” aliwahi kusema hivi (naapa nimenyambulisha kidogo) “Mnaweza kuamua kuachana na siasa ya ujamaa, lakini hamuwezi kuachana na sera ya kujitegemea”.

View attachment 1266057
Rais na viongozi wengine wakiangalia modeli ya bwawa la kufulia umeme la Nyerere, Rufiji.
​

Nadharia hii ya “Kujitegemea” ni miongoni mwa dhana ambazo bila kueleweka zinaweza kumfanya mtu awe duni mbele ya wengine. Mtu ambaye ni “tegemezi” au Nyerere aliita “ombaomba” kwa kiasi fulani anajidunisha mbele yaw engine. Kwa muda mrefu nchi zetu hizi za Kiafrika zilifika mahali za kuomba hadi misaada ya kujenga vyoo! Na bado hata leo kuna watu ambao wanasubiria serikali iwafanyie vitu ambavyo hata vilivyopo ndani ya uwezo wao. Kurudi kwenye “kujitegemea” ni kurudi kwenye kuuheshimu na kuulinda utu wetu kama binadamu. Hivi ni kweli, tunahitaji msaada wa kigeni kupanda bustani ya maua shuleni, au kwenye ofisi? Je, ni kweli tunahitaji msaada kutoka SIDA, USAID, EU, JICA, DANIDA, NORAD ili kuweza kufanyia ukarabati shule zetu kongwe, kujenga shule mpya, kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za watoto wetu, au kujenga viwanja vya kuchezea watoto na maktaba? Magufuli anaposema “tunaweza” anataka kutuambia kuwa “tumechelewa kujitegemea!”

Magufuli tangu kuingia kwake madarakani ameamua kulishikilia hili kama kwa mapembe. Analazimisha Taifa liwe na fikra za kujitegemea. Na hapa ni katika kutumia raslimali zake, uwezo wake, watu wake na mipango yake katika kujiletea maendeleo. Hakuna jambo linalotishia uhuru na utu wetu kama taifa kama kutegemea watu wa nje kwa mafanikio yetu. Jambo hili la kulazimisha taifa kujitegemea linaweza kuwa ni mafanikio makubwa zaidi ya Rais Magufuli kuliko mambo mengine.

Binafsi sitoshangaa kwa mwaka unaokuja Magufuli akiagiza wizara na idara zote kuandaa bajeti zao za 2020/2021 bila kuweka ndani au kusubiria misaada ya kigeni. Sitoshangaa kabisa akaamua kutukatisha kunyonya (weaning) kutoka kwa mashangazi zetu wa Ulaya na kulazimisha taifa kupanga bajeti yake kwa kutumia mapato na vyanzo vyake vya ndani. Misaada ya kigeni ikawa siyo tena ya moja kwa moja kwenye bajeti (Non-direct budgetary support). Akiamua kufanya jambo hili nawahakikishia dunia nzima itashtuka na hawatoamini na siyo hivyo tu wapo wenzetu humu humu (wapingaji) ambao watatuambia kwanini hatuwezi kujitegemea kwenye bajeti!

2. Amekataa Kuheshimu Sura
Kwa muda mrefu watu walikuwa wakishika madaraka walikuwa wanajiona wamefika. Watu walipoapishwa kushika ofisi yeyote walijisikia wako salama na wengine walifanya sherehe na kujisahau wakidhania sasa hatimaye na wao wamekuwa kwa waliokuwemo. Magufuli amewafanya sasa hivi watu kutokuwa salama kwenye vyeo vyao. Mtu anaweza kudhania hili ni jambo baya; lakini kiutawala hakuna jambo muhimu kama watu kurudi na kutambua dhana ya “cheo ni dhamana”. Hakuna aliye salama kwenye kiti chake na kuwa wakati huko nyuma watu walitegemea “Rais kuwalinda” sasa hivi hakuna anayeweza kuishi na kujihisi kuwa analindwa. Unaweza hata kuwaonea watu huruma.

Lakini kinyume na hisia ya wengi Rais Magufuli haoni aibu au kufikiria mara mbili kumuondoa hata mchezaji nyota kwenye mechi! Kulikuwepo na baadhi ya “wachezaji nyota” na wakajikuta wanaondolewa na mechi inaendelea kupigwa na watu wakashinda vile vile. Jambo hili limewafanya baadhi ya watu wanaojidhania au wanaojifikiria kuwa ni wachezaji nyota kujiangalia mara mbilimbili kweli kweli. Sasa hivi, hakuna kujali sura, tunajali utendaji wa kazi. Niliandika mada moja mwanzoni mwa utawala wa Magufuli na labda watu hawakuelewa uzito wake; nilisema “Tengua Tengua Inayokuja”. Sasa hivi ukipewa kiti cha utawala sheherekea huku unatokwa machozi. Wale wale watakaokuletea maua ya pongezi ndio watakaomletea mwingine maua ya pongezi.

Matokeo ya hili ni kuwa tunaona watendaji wengi – hasa mawaziri – wakiwa wanyenyekezu, wenye kujituma na kila mmoja akijitahidi kujionesha yuko kazini. Hata yule mwana mpendwa baada ya kupigwa mkwara wa juzi, tunamuona naye sasa hivi anakalia kitu kwa kukinyemelea! Wanaofikiria Magufuli anaiheshimu sana sura yake, watakuja kushangaa sana siku si nyingi.

3. Amekuwa Muwazi Mno hadi Kupitiliza
Kwa muda mrefu tulikuwa hatujui mambo yanayoendelea ndani ya serikali yetu. Mambo mengi tulikuwa tunayasikia kwenye majungu tu na vijiwe. Mambo mengine tulikuwa hata hatuyajui kabisa lakini sasa hivi ni kama tumefunguliwa mlango na madirisha tuchungulie kinachoendelea ndani. Rais Magufuli kwa ile tabia yake ya kutokuwa mzuri sana wa maneno, na kukataa kuyapamba maneno yake anaweza kuonekana wakati mwingine kama “fyatu” fulani hivi. Lakini kwa wanaomjua na sisi ambao tumemfuatilia kwa muda mrefu tunajua ni kuwa hana tabia ya kuficha ficha. Hata ile kauli yake maarufu ya “Msema kweli mpenzi wa Mungu” kimsingi inatuambia tu kuwa haoni sababu ya kwanini Watanzania wafichwefichwe. Kile anachoamini ni ukweli atakisema hadharani na wazi kabisa na wakati mwingine kutoificha aibu ndani ya serikali yake mwenyewe. Na watu wakaona – wakamsema na hata kumnyoshea kidole yeye mwenyewe. Rais wetu kwa kiasi kikubwa hana siri sana! Kuna mambo ya siri lakini ukiangalia sana mambo mengi ambayo watu wangependa kuwa ya siri hayana usiri wa maana kivile zaidi ya kufichiana tu siri zisizo na maana.

Uwazi huu umewasaidia wananchi kuona nini kilikuwa kinafanyika na nini kinafanyika sasa hivi. Bahati mbaya inaweza kusemwa ni kuwa uwazi huu ungenoga zaidi kama vyombo vya habari visingekuwa vinajisikia vinabanwa au kuulizwa ulizwa vinapojaribu na vyenyewe kufichua mambo. Hili sitolishangaa litatokea pia kwani “msema kweli ni mpenzi wa Mungu”. Siyo majungu, siyo umbeya, siyo porojo bali ukweli tu. Kwa vile Rais ameamua kuwa muwazi kwa wananchi ni lazima awaache na wananchi wawe wawazi kwa serikali yao; kwa maana halisi ya quid pro quo (nipe nikupe). Hakuna haja ya kufichana.

4. Ameamua Kufanya Ujenzi Mpya wa Taifa
Mojawapo ya mambo ambayo labda ni kubwa zaidi (linaloendana na lile la kwanza) ni uamuzi wake wa kufanya ujenzi mpya wa taifa (national reconstruction). Magufuli ni kama amedakia alipoachia Nyerere. Ukiangalia sasa hivi ni kana kwamba miaka ya Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete haipo. Ni kama Magufuli ameamua kuifuta na kuichukua nchi mwaka 1985. Akiichukua nchi mwaka 1985 anaikuta nchi ambayo imetoka kwenye janga la wahujumu uchumi (ufisadi), viongozi ambao wameshaonja ubepari na sasa kila mtu anataka kula kwa raha zake, na kuwa analikuta taifa ambalo wananchi wake wanatafuta maisha bora. Magufuli anaingia na kuamua kuendeleza mambo yale ya msingi ya kujenga misingi.

View attachment 1266052
Ujenzi wa Tanki la Maji huko Singida
​

Katika hili ameamua kufanya masuala ya ardhi na makazi, miundombinu (infrastructures), elimu, maji, umeme na nishati, kilimo, madini na afya. Katika mambo haya Rais Magufuli anajaribu kupalilia nchi na kupanda mbegu ili wengine waje kuvuna. Na anachofanya – na labda wakati mwingine wengi hawasikii – ni kuwa katika nchi nzima, na kwa wakati ule ule (simultaneously) miradi mbalimbali inatekelezwa.

Anachokifanya ni kuhakikisha kuwa hakuna sehemu kubwa ya nchi ambayo inaweza kujihisi inapitwa. Ukiwasikiliza watu wenye kukosoa kinachofanyika “Chato” unaweza ukadhania Magufuli amegoma kufanya jambo lolote sehemu nyingine ya nchi. Hili linaweza kuwa ni udhaifu wa taasisi zenyewe kujieleza lakini kwa tunaofuatilia tunajua jinsi gani matanki ya maji, njia za umeme, hospitali, vituo vya afya, barabara, vinavyoendelea kujengwa au vilivyokwisha jengwa ndani ya miaka hii minne kulinganisha na miaka mingine yote.

Mwisho
Mambo haya manne Magufuli anayafanya kwa namna ya tofauti sana. Lakini tofauti hiyo naweza kuielezea inatokana na mambo makubwa mawili ambayo hayakuwepo huko nyuma. Moja ni kuwa amekataa kufuata kilichoandikwa vitabuni. Kwamba, namna ya kufanya mambo ni a, b, na c kama watu walivyosoma shuleni. Badala yake anawalazimisha watendaji walio chini yake kufikiria nje ya sanduku na kujaribu vitu tofauti. Matokeo yake baadhi ya mambo ambayo yangekuwa yanachukua muda zaidi au raslimali zaidi yanaweza kufanyika kwa ubora na uharaka kuliko huko nyuma. Chukulia mfano wa mambo mawili tu kati ya mengi – suala la Masoko ya Madini na Vituo vya Mabasi – mambo haya hayakutangaliwa na vikao virefu vya sera na mipango; ni mambo ambayo yaliamriwa na watu wakapewa kazi kwenda kuyatekeleza.

Jambo la pili ni kuwa Rais Magufuli hana hofu ya kukosea au kuonekana amekosea. Kwa wanaomjua Magufuli hili wala si jambo jipya. Toka zamani Magufuli amekuwa ni mtu wa kufikiria kitu na kukitenda labda wakati mwingine kwa gharama kwa serikali au hata hadhi yake; lakini hofu ya matokeo ya kisheria (legal ramification) haijamzuia Magufuli kufanya kitu anachoamini ni sahihi. Hofu ya kuogopa kushtakiwa, au kugombana na wakubwa haikumzuia. Tuliona hili wakati wa suala la Makanikia na jinsi gani baadhi ya watu waliona kama Magufuli amegusa wakubwa na hatokuwa salama tena. Lakini Magufuli alisimamia kile hadi dakika ya mwisho. Hata hili suala la ujenzi wa Bwawa la Nyerere; kwa wengine liliwatia hofu kuwa wakubwa watetezi wa “mazingira” wangemkwamisha; lakini kama huwaombi dola zao watakukwamisha kwa lipi?

Miye nasubiria watakapoanza kutengeneza zile “cable cars” kuruka Ngorongoro na kutengeneza viewing platforms kama zilizoko kwenye vivutio vingi kwenye nchi za wenzetu (nenda pale Grand Canyon utaona). Sitoshangaa kuna watu watapiga kelele kweli. Wakati wenzetu wana barabara za lami zikikatisha Yosemite Parks na Parks nyingine huko majuu sisi kwetu tunaambiwa hata zinatishia wanyama na kuvuka kwa wanya kana kwamba hakuna namna ya kushughulikia hilo. Hili la pili ndio linaweza au limeweza kumtengeneza Magufuli maadui wengi wan je. Hana heshima kwao na kitendo chake cha kutokwenda kwao “kujionesha onesha au kujitambulisha” kunawakwaza wengi kweli kweli. Rais wa Afrika asiyependa kushikana mikono huko New York, Geneza, Paris na London ni mtu wa tofauti sana.

Mambo haya 4 bila ya shaka Magufuli anafanya tofauti sana na wengine watatu waliomtangulia. Inawezekana yapo mengine mengi ambayo anayafanya tofauti na wenzake. Na hapa nazungumzia yale chanya. Mtu mwingine anaweza kubisha. Nani anabisha?

Niandikie:
[email protected]

======
Mawazo ya wadau
Kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa mfano , huyo mtu wako anaheshimu nini? sura,wowowo,elimu yake kubwa ,Kabila yake au uchapakazi wake?
 
Kuna kitu fulani huko mashuleni tumejengewa nadhani kimetuathiri wengi.Ni pale mwalimu anapoainisha "Advantages" za issue fulani halafu chini yake anaainisha "Disadvantages" za issue hiyo hiyo papo hapo.
Hoja za MMJ zimejikita ktk "possitivities" za Mkulu ikiwa kama "icons for his legacy" nafikiri tunapaswa kuitendea haki mada yake kwa kuziangalia hizi. Labda mtu mwingine aje na uzi mpya wa "negativities" hapo pia hatutasita kumpa yampasayo kuyapata "with due weight". Kwa uzi wa MMJ tumejielekeza katika mazuri yake tu.
 
Tatizo wako soo caught up na miundo mbinu..kila wakitengeneza barabara hii,wanaona watengeneze na nyingine..wanasahau kuweka mambo kwenye balance,maeneno mengine pia kama Elimu yanahitaji matengenezo pia,..kila kitu kifanyike moderately.....

Mfumo wetu wa Elimu ukifumuliwa elimu itakayotolewa ikiwa inaendana na mazingira..(relevant education), then tatizo la ajira litapungua sana tuu...hawa wahitimu wa sasa hivi tunaweza tusijue la kufanya kuhusu wao,lakini tuna nafasi kubwa tu ya kurekebisha hili tatizo kwa wahitimu wanaokuja.......

Lugha pia imekua identified kama ni barrier kwenye Elimu yetu,lakini nothing is done,mie sijali kama tutatumia kiswahili kote kuanzia vidudu mpaka chuo au kutumia kingereza kuanzia vidudu mpka chuo...lazima tuchague lugha moja kama tunataka wasomi na sio wahitimu waliokariri theories...
Siku ukiwekwa kuwa Waziri wa Elimu (in case now you are not) halafu ukapewa support kuki-implement hiki ulicho nacho kichwani I'm 100% sure changamoto nyingi sana tulizonazo zitajitumbua zenyewe.
 
1. Kuipa magurudumu dhana ya kujitegemea.

Magufuli ni mtu mwenye utovu wa elimu ya kisiasa. Ni Mkemia aliyejikuta kwenye siasa. Hajui akitaka kujitegemea aanzie wapi.

Yupo incoherent.

Mfano mdogo. Aliona kuingilia biashara ya korosho kwa nguvu ya jeshi ndiyo kitu kizuri. Akaonywa hilo si jambo jema na litaangusha mapato, hakusikia, matokeo yake, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Oktoba 2019 inasema mapato ya exports za mazao ya kilimo kwa mwaka ulioishia Agosti 2019 yameanguka kwa asilimia 55, ukiyalinganisha na ya mwaka uliopita. Sababu kubwa kabisa ya kuanguka huku ni serikali ilivyoingilia kwa mabavu biashara ya korosho, zao la kwanza kwa kutupatia fedha za kigeni.

Kwa kila shilingi 1000 tuliyopata mwaka wa kabla ya huu uliopita, kwa mwaka uliopita tumepata shilingi 450, hasara ya shilingi 550, zaidi ya nusu nzima!

Mtu aliye incoherent, ambaye anakwenda kwa kuhamanika kwa munkari bila mkakati, hawezi kutupa hoja ya kujitegemea.

2. Magufuli hajakataa kuheshimu sura. Anatengeneza image ya uongo kwamba yeye haheshimu sura. Magufuli angekuwa haheshimu sura kweli, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, angekwishaondolewa siku nyingi sana. Makonda ana scandals nyingi sana. Scandal iliyomvua nguo kabisa Magufuli ni pale Makonda alipotaka kuingiza samani kwa ujanjaujanja, Magufuli akamsema kama anamuogopa vile, wakati kawaida yake anatumbua watu kabla hotuba haijaisha. Hili limetuonesha kwamba Magufuli ni bully tu, anawa bully watu fulani, akifika kwa watu wake kina Makonda anachekacheka, hata wavamie redio na bunduki au waingize vitu bila kulipa kodi. Kabakia kutukana viongozi wenziwe na wake zao tu.

3. Uwazi
Uwazi ni kitu kizuri. Lakini there is such a thing as "too much information". Rais anatakiwa kuwa muwazi, lakini anatakiwa kuwa na kifua cha kuweka maneno.Magufuli hana kifua cha kuweka maneno, anaropoka sana, huu si uwazi. Kuna tofauti ya mtu kuwa muwazi na mtu kuwa mropokaji. Magufuli si muwazi, ni mropokaji. Usichanganye hayo mawili.

4. Ameamua kufanya ujenzi mpya wa taifa

Kuna habari moja, sijui kama ni ya kweli au kutungwa, lakini ina funzo zuri, hivyo kwa msingi huo, naiona inafaa kurudiwa, hata kama ni ya kutungwa, kwa sababu ina mafunzo mema.

Wanasema kulikuwa na Waziri mmoja wa Fedha wa Nigeria. Alienda Uswizi kwenye mabenki makubwa ya dunia. Akaaulizia, hapa benki kubwa kabisa inayoficha hela za vigogo wa Nigeria iko wapi? Akatajiwa. Akaenda ile benki, akasema mimi waziri wa fedha wa Nigeria, naomba kuongea na mkurugenzi wenu.

Akapewa appointment na Mkurugenzi, akaenda kuongea naye.

Akamwambia Mkurugenzi, nimekuja hapa nina shida, Africa tunaibiwa sana fedha. Nataka unipe list ya wateja wako wa kutoka Nigeria, na hela walizoweka katika benki yako, tuwahakiki na biashara zao kama hela hizi ni halali, wanalipa kodi etc.

Yule Mkurugenizi Swiss banker akamwambia wewe jamaa una kichaa ama nini? Sisi tuna sheria za kulinda wateja wetu hapa. Waziri akamwambia mimi sijajja kufanya mchezo hapa, nina barua kutoka serikali ya Nigeria. Mswizi akamwambia hata ingekuwa serikali ya Uswizi au Marekani, hatujali, tuna sheria zinatulinda. Waziri akasema sawa, tutafuta deals zote za serikali ya Nigeria na benki yako, mtakosa hela nyingi sana. Yule Mkurugenzi akasema wala sijali. Waziri akatoa bastola, akamuwekea Mkurugenzi kichwani, akasema nipe majina haya, usiponipa nakufyatulia risasi ufe. Banker Mkurugenzi Mswizi akasema Waziri wewe niue tu, majina sikupi.

Waziri akasema, vizuri sana. Nimeitafuta benki yenye usiri kama hii kwa muda mrefu sana sijaipata. Haya hapa mamilioni yangu nataka mniwekee, maana kwa usiri huu umehatarisha mpaka maisha yako, nikiweka hela zangu hapa, hakuna atakayejua.

What is the point of this story? Mara nyingine watu wanaojifanya wakali sana kupinga rushwa, kujenga taifa etc, wanaweka show tu. Wao hao hao ndio wapigaji wakubwa na wala rushwa wakubwa.

Magufuli hawezi kuwa ameamua kujenga taifa, kwa sababu analigawa taifa kisiasa, ameharibu umoja wa kitaifa kuliko rais yeyote aliyempita, anasema wazi kwamba atapendelea watu wa CCM. Sasa hapo anajenga taifa au anajenga watu wa chama chake?
Kuongea tu taifa linajengwa kwa katiba bora inayotegeneza institutions imara na si bla bla za Magufuli,watu kama akina Mm wanaoandika upuuzi ndo wanawafanya watu waione elimu kwa sasa si chochote
 
Hahahahahaaaa hata sijui nacheka nini!
Amekuwa muwazi???? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] We mzee wewe ngoja nikuheshimu kama baba yangu
 
Balaaa juu ya balaa.Nyeupe,nyeupe.Nyeusi,nyeusi.Nukta.
Eti Jiwe anataka kujitegemea!.

Wewe mzee uko out of touch, either umeamua kujitoa ufahamu au hujui kinachoendelea nchini.
Sema tu kuwa Jiwe anapenda slogans, na maneno maneno tu ya mwalimu Nyerere nadhani akilini mwake anadhani kuwa eti yeye ni kama Nyerere, kitu ambacho ni illusion, kiufupi ni kwamba hana charisma, wala intellectual prowess wala leadership skills za mwalimu.

Kujitegemea kupi wakati anapotunga sheria za ajabu ajabu bungeni wananchi tukipiga kelele anaweka pamba masikioni lakini Wazungu wakikohoa anakimbia haraka haraka bungeni kuzibadirisha!. Mfano ni Sheria ya Takwimu

Pili kama ni muwazi basi aanzishe uchunguzi wa Kupotea Be Saanane, na aanzishe uchunguzi wa aliyempiga risasi Lissu na aanzishe uchunguze wa nani alimpoteza Kanguye na aliyemuua kada wa Chadema wa kata ya Hananasif.

By the way, unazungumzia uwazi upi wakati serikali yake imejitoa katika mkataba wa kuendesha nchi kwa uwazi?, au uwazi unaosema wewe ni yale maneno ya kutishatisha watu, kukaripia watu, kuproject mamlaka waziwazi mbele za watu, Je huo ndo uwazi unaousema wewe?
Mtu aliyetunyima bunge live ili tusione serikali yake inavyojibu hoja za wawakilishi bungeni ndo unatwambia ni. muwazi?. Wewe mzee hauko serious!!

Tatu haina maana kama uthubutu wako unavunja sheria za nchi, kwanza ni ujinga kusifu mtu eti ana uthubutu hata kama ni kwa kuvunja sheria. Walioweka sheria siyo wajinga, kuna njia moja tu ya kufanya kama sheria inakuchelewesha kwenye mambo yako, badili sheria ulete nyingine kwanza ndo ufanye mambo yako!
Nilitegemea ukemee hii tabia inayoota mizizi ya kutoheshimu sheria, lakini badala yako wewe unaiona kama a plus, something to cheer, something ya kujitapa

Lakini nikukumbushe tu pia
Mpaka sasa deni la Taifa linazidi kukua, Kasi ya ukopaji ya Jiwe inazidi kasi ya ukopaji ya maraisi watatu waliopita, Kiufupi anatuingiza katika shimo refu la deni la Taifa. Hili ni jambo la kuogofya siyo kusifu.

Mwisho, haina haja ya kusifu mtu kwa kutumia "induction method", bali tuwekee kazi zake hapa tuzichambue moja baada ha nyingine, Usitueleze jinsi chai ilivyo tamu, tupe hiyo chai tuinywe tuone. Nikimasnisha weka kazi za Jiwe moja baada ya nyingine tuifanyie critique, Siyo blah blah.

Mtu anatumia pesa za umma bila kuidhinishwa na bunge kinyume cha sheria kama vile kununua ndege na kulipa korosho ambazo yeye ndo alisababisha tatizo halafu unamsifia uthubutu? - Mzee you are out of your mind.

Mtajitahidi sana kumpamba na kumremba Jiwe Lakini as long as Serikali yake haitaki kuchunguza waliompiga risasi Lissu, waliompoteza Kanguye, Waliompoteza Ben Saanane, Sifa zenu ni kazi bure
 
Kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa mfano ,hugo huyo mtu wako anaheshimu nini? sura,wowowo,elimu yake kubwa ,Kabila yake au uchapakazi wake?

Sifa ulizoainisha hapo ni elimu na uchapakazi tu ndizo zenye maana kwa watu wazima. Hayo ya sura na mengine hayo ni umbea na mipasho ya kupuuzwa. Kuhusu elimu, sheria ya uteuzi kwenye nafasi hiyo ikoje? Na je, kwenye uchapakazi, ‘yardstick’ za uchapakazi kwenye nafasi hiyo ni zipi?
 
Wise
Asante sana mkuu, jitahidi sana kuumiza kichwa kutetea. Naamini una kazi ngumu sana ya kupamba ili utufanye tuamini kwamba 'nyeusi ni nyeupe'. Tusichokijua ni kwa nini una kazi hii!
Mzee si tunaiona nyeusi au macho yetu yana makengeza?
Kwa kweli sielewi hasa nini malengo ya nyuzi zako kama hizi! Ila tambua kwamba historia itamuandika kila mwenye kutenda na matendo yake.
 
Sifa ulizoainisha hapo ni elimu na uchapakazi tu ndizo zenye maana kwa watu wazima. Hayo ya sura na mengine hayo ni umbea na mipasho ya kupuuzwa. Kuhusu elimu, sheria ya uteuzi kwenye nafasi hiyo ikoje? Na je, kwenye uchapakazi, ‘yardstick’ za uchapakazi kwenye nafasi hiyo ni zipi?
unaniuliza mimi au mwanakijiji au mteuaji?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Yote tisa, kumi tuseme ukweli. Kuna mambo ambayo mtu anaweza kuamua kuyachukia dhidi ya Rais Magufuli. Mtu anaweza kuamka na kuapa kwa jina la miungu na mababu zake ya kwanini hataki kulisikia jina la Rais Magufuli. Tena mtu anaweza akaamka hata usiku wa manane kama mtu aliyepatwa na jinamizi akiwa na hofu ya Magufuli. Siwezi kuwasemea wale ambao wakisikia jina la Rais Magufuli wanaweza kujihisi pumzi zinawaisha na kujisikia unyonge. Umpende au umchukie Rais Magufuli bado anaonekana kugawa hisia za watu mbalimbali tena kwa ukali sana; ama unamkubali au unamkataa; hakuna upande wa katikati.

Na wapo pia ambao wanaposikia jina la Magufuli kwao wanajisikia matumaini, faraja, na wengine wanakuwa kama yule mwanamuziki aliyeimba wimbo wa “Magufuli Raha Tu”. Hawa wanaposikia jina la Rais Magufuli ni kama wanapata Amani ya huko mbeleni, wanajua nchi iko salama na kuwa wao na watoto wao wanashuhudia mambo ambayo labda hayakudhaniwa kuwa yanaweza kutokea katika nchi hii hii ya Waafrika tena miongoni mwa zile nchi zilizokubali jina la “Maskini Zaidi” duniani. Kwa hawa ukitaja jina la Magufuli hata ukiwaamsha usingizini wengine wanaweza kuhisi ni kama unawakatisha zile ndoto tamu tamu zinazoweza kumfanya mtu ajikute anatafuna mto akidhania ni keki!

Vyovyote vile ilivyo kuna mambo manne ambayo naweza kuyasema kwa ufupi tu ambayo Rais Magufuli anayafanya tofauti sana na viongozi wengine. Bila ya shaka kuna mengine anayafanya ambayo yanafanana na watangulizi wake na kubwa katika hayo ni ile hali ya kutukuza chama chake na kukifanyia kila namna ya msaada na mbinu ya kutaka kiendelee kubakia madarakani kwa miongo mingi ijayo. Sidhani kama kuna kiongozi atakayekuja kutoka CCM ambaye atafikiria au kujaribu kufanya kinyume cha hilo. Hata hivyo, binafsi ningependa kudokeza yale mambo ya kiutendaji (executive) ambayo Rais Magufuli anayanya – kwa maoni yangu – kwa namna tofauti na viongozi watatu waliomtangulia.

1. Dhana ya Kujitegemea Ameipa Magurudumu
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati anaikaripia serikali ya Rais Mkapa kufuatia ile sera ya “ubinafsishaji wa mashirika ya umma” na ile hali ya kujaribu kuendekeza sana “wawekezaji wa nje” aliwahi kusema hivi (naapa nimenyambulisha kidogo) “Mnaweza kuamua kuachana na siasa ya ujamaa, lakini hamuwezi kuachana na sera ya kujitegemea”.

View attachment 1266057
Rais na viongozi wengine wakiangalia modeli ya bwawa la kufulia umeme la Nyerere, Rufiji.
​

Nadharia hii ya “Kujitegemea” ni miongoni mwa dhana ambazo bila kueleweka zinaweza kumfanya mtu awe duni mbele ya wengine. Mtu ambaye ni “tegemezi” au Nyerere aliita “ombaomba” kwa kiasi fulani anajidunisha mbele yaw engine. Kwa muda mrefu nchi zetu hizi za Kiafrika zilifika mahali za kuomba hadi misaada ya kujenga vyoo! Na bado hata leo kuna watu ambao wanasubiria serikali iwafanyie vitu ambavyo hata vilivyopo ndani ya uwezo wao. Kurudi kwenye “kujitegemea” ni kurudi kwenye kuuheshimu na kuulinda utu wetu kama binadamu. Hivi ni kweli, tunahitaji msaada wa kigeni kupanda bustani ya maua shuleni, au kwenye ofisi? Je, ni kweli tunahitaji msaada kutoka SIDA, USAID, EU, JICA, DANIDA, NORAD ili kuweza kufanyia ukarabati shule zetu kongwe, kujenga shule mpya, kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za watoto wetu, au kujenga viwanja vya kuchezea watoto na maktaba? Magufuli anaposema “tunaweza” anataka kutuambia kuwa “tumechelewa kujitegemea!”

Magufuli tangu kuingia kwake madarakani ameamua kulishikilia hili kama kwa mapembe. Analazimisha Taifa liwe na fikra za kujitegemea. Na hapa ni katika kutumia raslimali zake, uwezo wake, watu wake na mipango yake katika kujiletea maendeleo. Hakuna jambo linalotishia uhuru na utu wetu kama taifa kama kutegemea watu wa nje kwa mafanikio yetu. Jambo hili la kulazimisha taifa kujitegemea linaweza kuwa ni mafanikio makubwa zaidi ya Rais Magufuli kuliko mambo mengine.

Binafsi sitoshangaa kwa mwaka unaokuja Magufuli akiagiza wizara na idara zote kuandaa bajeti zao za 2020/2021 bila kuweka ndani au kusubiria misaada ya kigeni. Sitoshangaa kabisa akaamua kutukatisha kunyonya (weaning) kutoka kwa mashangazi zetu wa Ulaya na kulazimisha taifa kupanga bajeti yake kwa kutumia mapato na vyanzo vyake vya ndani. Misaada ya kigeni ikawa siyo tena ya moja kwa moja kwenye bajeti (Non-direct budgetary support). Akiamua kufanya jambo hili nawahakikishia dunia nzima itashtuka na hawatoamini na siyo hivyo tu wapo wenzetu humu humu (wapingaji) ambao watatuambia kwanini hatuwezi kujitegemea kwenye bajeti!

2. Amekataa Kuheshimu Sura
Kwa muda mrefu watu walikuwa wakishika madaraka walikuwa wanajiona wamefika. Watu walipoapishwa kushika ofisi yeyote walijisikia wako salama na wengine walifanya sherehe na kujisahau wakidhania sasa hatimaye na wao wamekuwa kwa waliokuwemo. Magufuli amewafanya sasa hivi watu kutokuwa salama kwenye vyeo vyao. Mtu anaweza kudhania hili ni jambo baya; lakini kiutawala hakuna jambo muhimu kama watu kurudi na kutambua dhana ya “cheo ni dhamana”. Hakuna aliye salama kwenye kiti chake na kuwa wakati huko nyuma watu walitegemea “Rais kuwalinda” sasa hivi hakuna anayeweza kuishi na kujihisi kuwa analindwa. Unaweza hata kuwaonea watu huruma.

Lakini kinyume na hisia ya wengi Rais Magufuli haoni aibu au kufikiria mara mbili kumuondoa hata mchezaji nyota kwenye mechi! Kulikuwepo na baadhi ya “wachezaji nyota” na wakajikuta wanaondolewa na mechi inaendelea kupigwa na watu wakashinda vile vile. Jambo hili limewafanya baadhi ya watu wanaojidhania au wanaojifikiria kuwa ni wachezaji nyota kujiangalia mara mbilimbili kweli kweli. Sasa hivi, hakuna kujali sura, tunajali utendaji wa kazi. Niliandika mada moja mwanzoni mwa utawala wa Magufuli na labda watu hawakuelewa uzito wake; nilisema “Tengua Tengua Inayokuja”. Sasa hivi ukipewa kiti cha utawala sheherekea huku unatokwa machozi. Wale wale watakaokuletea maua ya pongezi ndio watakaomletea mwingine maua ya pongezi.

Matokeo ya hili ni kuwa tunaona watendaji wengi – hasa mawaziri – wakiwa wanyenyekezu, wenye kujituma na kila mmoja akijitahidi kujionesha yuko kazini. Hata yule mwana mpendwa baada ya kupigwa mkwara wa juzi, tunamuona naye sasa hivi anakalia kitu kwa kukinyemelea! Wanaofikiria Magufuli anaiheshimu sana sura yake, watakuja kushangaa sana siku si nyingi.

3. Amekuwa Muwazi Mno hadi Kupitiliza
Kwa muda mrefu tulikuwa hatujui mambo yanayoendelea ndani ya serikali yetu. Mambo mengi tulikuwa tunayasikia kwenye majungu tu na vijiwe. Mambo mengine tulikuwa hata hatuyajui kabisa lakini sasa hivi ni kama tumefunguliwa mlango na madirisha tuchungulie kinachoendelea ndani. Rais Magufuli kwa ile tabia yake ya kutokuwa mzuri sana wa maneno, na kukataa kuyapamba maneno yake anaweza kuonekana wakati mwingine kama “fyatu” fulani hivi. Lakini kwa wanaomjua na sisi ambao tumemfuatilia kwa muda mrefu tunajua ni kuwa hana tabia ya kuficha ficha. Hata ile kauli yake maarufu ya “Msema kweli mpenzi wa Mungu” kimsingi inatuambia tu kuwa haoni sababu ya kwanini Watanzania wafichwefichwe. Kile anachoamini ni ukweli atakisema hadharani na wazi kabisa na wakati mwingine kutoificha aibu ndani ya serikali yake mwenyewe. Na watu wakaona – wakamsema na hata kumnyoshea kidole yeye mwenyewe. Rais wetu kwa kiasi kikubwa hana siri sana! Kuna mambo ya siri lakini ukiangalia sana mambo mengi ambayo watu wangependa kuwa ya siri hayana usiri wa maana kivile zaidi ya kufichiana tu siri zisizo na maana.

Uwazi huu umewasaidia wananchi kuona nini kilikuwa kinafanyika na nini kinafanyika sasa hivi. Bahati mbaya inaweza kusemwa ni kuwa uwazi huu ungenoga zaidi kama vyombo vya habari visingekuwa vinajisikia vinabanwa au kuulizwa ulizwa vinapojaribu na vyenyewe kufichua mambo. Hili sitolishangaa litatokea pia kwani “msema kweli ni mpenzi wa Mungu”. Siyo majungu, siyo umbeya, siyo porojo bali ukweli tu. Kwa vile Rais ameamua kuwa muwazi kwa wananchi ni lazima awaache na wananchi wawe wawazi kwa serikali yao; kwa maana halisi ya quid pro quo (nipe nikupe). Hakuna haja ya kufichana.

4. Ameamua Kufanya Ujenzi Mpya wa Taifa
Mojawapo ya mambo ambayo labda ni kubwa zaidi (linaloendana na lile la kwanza) ni uamuzi wake wa kufanya ujenzi mpya wa taifa (national reconstruction). Magufuli ni kama amedakia alipoachia Nyerere. Ukiangalia sasa hivi ni kana kwamba miaka ya Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete haipo. Ni kama Magufuli ameamua kuifuta na kuichukua nchi mwaka 1985. Akiichukua nchi mwaka 1985 anaikuta nchi ambayo imetoka kwenye janga la wahujumu uchumi (ufisadi), viongozi ambao wameshaonja ubepari na sasa kila mtu anataka kula kwa raha zake, na kuwa analikuta taifa ambalo wananchi wake wanatafuta maisha bora. Magufuli anaingia na kuamua kuendeleza mambo yale ya msingi ya kujenga misingi.

View attachment 1266052
Ujenzi wa Tanki la Maji huko Singida
​

Katika hili ameamua kufanya masuala ya ardhi na makazi, miundombinu (infrastructures), elimu, maji, umeme na nishati, kilimo, madini na afya. Katika mambo haya Rais Magufuli anajaribu kupalilia nchi na kupanda mbegu ili wengine waje kuvuna. Na anachofanya – na labda wakati mwingine wengi hawasikii – ni kuwa katika nchi nzima, na kwa wakati ule ule (simultaneously) miradi mbalimbali inatekelezwa.

Anachokifanya ni kuhakikisha kuwa hakuna sehemu kubwa ya nchi ambayo inaweza kujihisi inapitwa. Ukiwasikiliza watu wenye kukosoa kinachofanyika “Chato” unaweza ukadhania Magufuli amegoma kufanya jambo lolote sehemu nyingine ya nchi. Hili linaweza kuwa ni udhaifu wa taasisi zenyewe kujieleza lakini kwa tunaofuatilia tunajua jinsi gani matanki ya maji, njia za umeme, hospitali, vituo vya afya, barabara, vinavyoendelea kujengwa au vilivyokwisha jengwa ndani ya miaka hii minne kulinganisha na miaka mingine yote.

Mwisho
Mambo haya manne Magufuli anayafanya kwa namna ya tofauti sana. Lakini tofauti hiyo naweza kuielezea inatokana na mambo makubwa mawili ambayo hayakuwepo huko nyuma. Moja ni kuwa amekataa kufuata kilichoandikwa vitabuni. Kwamba, namna ya kufanya mambo ni a, b, na c kama watu walivyosoma shuleni. Badala yake anawalazimisha watendaji walio chini yake kufikiria nje ya sanduku na kujaribu vitu tofauti. Matokeo yake baadhi ya mambo ambayo yangekuwa yanachukua muda zaidi au raslimali zaidi yanaweza kufanyika kwa ubora na uharaka kuliko huko nyuma. Chukulia mfano wa mambo mawili tu kati ya mengi – suala la Masoko ya Madini na Vituo vya Mabasi – mambo haya hayakutangaliwa na vikao virefu vya sera na mipango; ni mambo ambayo yaliamriwa na watu wakapewa kazi kwenda kuyatekeleza.

Jambo la pili ni kuwa Rais Magufuli hana hofu ya kukosea au kuonekana amekosea. Kwa wanaomjua Magufuli hili wala si jambo jipya. Toka zamani Magufuli amekuwa ni mtu wa kufikiria kitu na kukitenda labda wakati mwingine kwa gharama kwa serikali au hata hadhi yake; lakini hofu ya matokeo ya kisheria (legal ramification) haijamzuia Magufuli kufanya kitu anachoamini ni sahihi. Hofu ya kuogopa kushtakiwa, au kugombana na wakubwa haikumzuia. Tuliona hili wakati wa suala la Makanikia na jinsi gani baadhi ya watu waliona kama Magufuli amegusa wakubwa na hatokuwa salama tena. Lakini Magufuli alisimamia kile hadi dakika ya mwisho. Hata hili suala la ujenzi wa Bwawa la Nyerere; kwa wengine liliwatia hofu kuwa wakubwa watetezi wa “mazingira” wangemkwamisha; lakini kama huwaombi dola zao watakukwamisha kwa lipi?

Miye nasubiria watakapoanza kutengeneza zile “cable cars” kuruka Ngorongoro na kutengeneza viewing platforms kama zilizoko kwenye vivutio vingi kwenye nchi za wenzetu (nenda pale Grand Canyon utaona). Sitoshangaa kuna watu watapiga kelele kweli. Wakati wenzetu wana barabara za lami zikikatisha Yosemite Parks na Parks nyingine huko majuu sisi kwetu tunaambiwa hata zinatishia wanyama na kuvuka kwa wanya kana kwamba hakuna namna ya kushughulikia hilo. Hili la pili ndio linaweza au limeweza kumtengeneza Magufuli maadui wengi wan je. Hana heshima kwao na kitendo chake cha kutokwenda kwao “kujionesha onesha au kujitambulisha” kunawakwaza wengi kweli kweli. Rais wa Afrika asiyependa kushikana mikono huko New York, Geneza, Paris na London ni mtu wa tofauti sana.

Mambo haya 4 bila ya shaka Magufuli anafanya tofauti sana na wengine watatu waliomtangulia. Inawezekana yapo mengine mengi ambayo anayafanya tofauti na wenzake. Na hapa nazungumzia yale chanya. Mtu mwingine anaweza kubisha. Nani anabisha?

Niandikie:
[email protected]

======
Mawazo ya wadau

Mzee Mwanakijiji,
Mimi najaribu kujikuna tu kama ambavo RC Mwanri huwa anajaribu kufurahisha hadhira anayoongea nayo.
Katika hayo manne uliyoya ainisha mimi nagusa kwenye 2 na 3 tu kama najikuna vile!

2. Amekataa Kuheshimu Sura:

Hili nalibishia kwa vile ulichosema hakina uhalisia wala ukweli. Wengi wamekosoa kuhusu watendaji waliokaribu na Magufuli wanaofanya mafyongo kwa kuvunja sheria na taratibu za nchi lakini bado wapo kwenye Timu ya Praise& Worship!
RC Makonda(Dar), RC Happiness(IRA), RC Gambo(ARU) na DC Ole Sabaya(HAI) ni Vuongozi wanaokiuka Katiba katika maeneo mengi lakini kwa vile ni watoto pendwa wanaomfurahisha Bwana Mkubwa kwa aidha Kunyanyasa na Kukandamiza UPINZANI basi wanaonekana SURA ZAO KUHESHIMIWA na kutetewa kila uchao.

Napenda nikupe kesi kama 2 za mfano. Kuna viongozi walitumbuliwa kwa makosa madogo kuliko hata aliyofanya Makonda aliyeingiza mali kutoka nje na kujaribu KUKWEPA KODI na mpaka leo yuko kazini...!!Linganisha kesi ya Makonda ya kukwepa Kodi kosa linaloangukia kwenye Uhujumu Uchumi na kosa la Mhe. Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani kwa kutumbuliwa baada ya kujibu swali Bungeni akiwa amelewa..!!! Hivi kwa akili ya kawaida nani alistahili kupewa onyo badala ya kufukuzwa kati ya Makonda na Kitwanga?

Kesi ya pili ni ya Mhe. Nape Nnauye na issue ya Clouds FM. Nnape akiwa Waziri wa Habari alitaka Haki itendeke kati ya Makonda na Clouds kwa kuvamia na Silaha akiwa na Askari kustitiza umbeya wake uende hewani. Nnape alipounda Tume kuchunguza huo upuuzi wa Makonda alizuiwa asitoe taarifa ya Tume yake na akaishia kufukuzwa kwenye Uwaziri. Kwa akili yako hapo nani alistahili kutimuliwa kazi kwa kusimamia Haki kati ya Makonda na Nnape? Mzee wa Kijiji majibu unayo hata kama unaweza kutetea ubazazi ili kumpendezesha Bwanakuba maana pengine NJAA KALI kama alivodai Makonda mwenyewe baada ya kushindwa kusimamamia ujenzi wa Machinjio ya Vngunguti...!!!

3. Amekuwa Muwazi Mno hadi Kupitiliza
Hili la kusema JPM amekuwa MUWAZI mno kiasi cha kupitiliza ni lugha zilezile za PRAISE&WORSHIP to the an angelic human being. Niseme hivi. Katika awamu zote 1-4 hii A5 ya JPM ndiyo inaonekana kufanya mambo mengi sana KISIRISIRI kwa kutumia MLANGO WA NYUMA. Kuna matukio kibao yamejitokeza tangu Magufuli aingie Ikulu lakini hayajawekwa wazi asilani. Kama JPM ni muwazi hadi kupitiliza hebu wewe utuambie nini kilichowazi kwa haya yafuatayo:
  • Kupigwa Risasi kwa Mhe.Tundu A. Lissu(MB) mchana kweupe tena kwenye makazi ya Wabunge na Viongozi huko Dodoma wakti wa kikao cha Bunge?Kwanini CCTV Camera ziliondolewa ambazo zingelisaidia kuwajua hao wabaya wa Lissu?Kwanini mpaka leo hii zaidi ya 2 years Jeshi la Polisi hawajafanya lolote badala ya kumlaumu Mhe. Lissu na Dereva wake kana kwamba wap ndiyo walijishambuliwa....!
  • Kutekwa na kupotezwa kwa Ben Saanane katika mazingira tatanishi na mpaka leo hajulikani yuko wapi. Polisi wakiulizwa wanadai bado wanaendelea na Uchunguzi....Huo wazi uko wapi Mzee wa Kijiji?
  • Mwandishi wa kujitegemea wa Mwananchi media ndugu Azory Gwanda jana ametimiza miaka 2 hajulikani aliko. Polisi wakiulizwa wanadai amejiteka mwenyewe!! Huo uwazi katika hili uko wapi Mwanakijiji?
  • Kutekwa kwa Mo Dewji likewise...!!!Hakuna uwazi wala ukweli katika tukio hilo!! Kuna siku JPM mwenyewe aliropokwa sijui kwa kuona haya au aibu ya Utawala wake alipowaambia Polisi kuwa Watanzania siyo wajinga...!!!Haiwezekani mtu tajiri na maarufu kama Mo atekwe Dar akae siku 9 nchi na vyombo vya Ulinzi na Usalama havijui mtu yuko wapi....!!!Lakini katika sekeseke hilo watu kama Makonda kama kawaida waliropoka kuwa Mo atapatikana akiwa mzima sijui kwa info gani aliyokuwa nayo..!!!Maana kama mtu ametekwa na magaidi, majambazi au wahuni na huna mawasiliano nao unauaje kuwa watamwachia akiwa salama? Na ndicho kilichotokea.Hapa kuna kitu HAKIJAWEKWA WAZI na kinajulikana vizuri sana na Rais Magufuli,IGP Ziro na Kamanda Mambosasa.
  • Yako mambo mengi sana ambayo utawala wa JPM hautaki kuyaweka wazi na hivo kuondoa hiyo sifa ya Uwazi wa kupitiliza..!!

  • Ngoja niishie hapa kwa kujaribu kujikuna kwa leo.
 
Shikamoo Mzee Mwanakijiji Mimi ni mwanao kama si mjukuu wako..
Naamini upo karibu na Bwana mkubwa..
Ila mfikishie hiki kilio changu..
Ajira Ajira ajira ajira baba...
Kwenye mambo mengi sana nipo pamoja naye.. Ila hyo kitu inafanya vijana wengi tumchukie kwa namna moja au nyingine huyo bwana mkubwa.
Serikali I HAKUNA ajira. Tumia maarifa uliyopata chuoni Wewe na wenzio kujiajiri.
Usiulize mtaji Utapata wapi. Mabenki yapo,vicoba vipo.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mimi najaribu kujikuna tu kama ambavo RC Mwanri huwa anajaribu kufurahisha hadhira anayoongea nayo.
Katika hayo manne uliyoya ainisha mimi nagusa kwenye 2 na 3 tu kama najikuna vile!

2. Amekataa Kuheshimu Sura:

Hili nalibishia kwa vile ulichosema hakina uhalisia wala ukweli. Wengi wamekosoa kuhusu watendaji waliokaribu na Magufuli wanaofanya mafyongo kwa kuvunja sheria na taratibu za nchi lakini bado wapo kwenye Timu ya Praise& Worship!
RC Makonda(Dar), RC Happiness(IRA), RC Gambo(ARU) na DC Ole Sabaya(HAI) ni Vuongozi wanaokiuka Katiba katika maeneo mengi lakini kwa vile ni watoto pendwa wanaomfurahisha Bwana Mkubwa kwa aidha Kunyanyasa na Kukandamiza UPINZANI basi wanaonekana SURA ZAO KUHESHIMIWA na kutetewa kila uchao.

Napenda nikupe kesi kama 2 za mfano. Kuna viongozi walitumbuliwa kwa makosa madogo kuliko hata aliyofanya Makonda aliyeingiza mali kutoka nje na kujaribu KUKWEPA KODI na mpaka leo yuko kazini...!!Linganisha kesi ya Makonda ya kukwepa Kodi kosa linaloangukia kwenye Uhujumu Uchumi na kosa la Mhe. Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani kwa kutumbuliwa baada ya kujibu swali Bungeni akiwa amelewa..!!! Hivi kwa akili ya kawaida nani alistahili kupewa onyo badala ya kufukuzwa kati ya Makonda na Kitwanga?

Kesi ya pili ni ya Mhe. Nape Nnauye na issue ya Clouds FM. Nnape akiwa Waziri wa Habari alitaka Haki itendeke kati ya Makonda na Clouds kwa kuvamia na Silaha akiwa na Askari kustitiza umbeya wake uende hewani. Nnape alipounda Tume kuchunguza huo upuuzi wa Makonda alizuiwa asitoe taarifa ya Tume yake na akaishia kufukuzwa kwenye Uwaziri. Kwa akili yako hapo nani alistahili kutimuliwa kazi kwa kusimamia Haki kati ya Makonda na Nnape? Mzee wa Kijiji majibu unayo hata kama unaweza kutetea ubazazi ili kumpendezesha Bwanakuba maana pengine NJAA KALI kama alivodai Makonda mwenyewe baada ya kushindwa kusimamamia ujenzi wa Machinjio ya Vngunguti...!!!

3. Amekuwa Muwazi Mno hadi Kupitiliza
Hili la kusema JPM amekuwa MUWAZI mno kiasi cha kupitiliza ni lugha zilezile za PRAISE&WORSHIP to the an angelic human being. Niseme hivi. Katika awamu zote 1-4 hii A5 ya JPM ndiyo inaonekana kufanya mambo mengi sana KISIRISIRI kwa kutumia MLANGO WA NYUMA. Kuna matukio kibao yamejitokeza tangu Magufuli aingie Ikulu lakini hayajawekwa wazi asilani. Kama JPM ni muwazi hadi kupitiliza hebu wewe utuambie nini kilichowazi kwa haya yafuatayo:
  • Kupigwa Risasi kwa Mhe.Tundu A. Lissu(MB) mchana kweupe tena kwenye makazi ya Wabunge na Viongozi huko Dodoma wakti wa kikao cha Bunge?Kwanini CCTV Camera ziliondolewa ambazo zingelisaidia kuwajua hao wabaya wa Lissu?Kwanini mpaka leo hii zaidi ya 2 years Jeshi la Polisi hawajafanya lolote badala ya kumlaumu Mhe. Lissu na Dereva wake kana kwamba wap ndiyo walijishambuliwa....!
  • Kutekwa na kupotezwa kwa Ben Saanane katika mazingira tatanishi na mpaka leo hajulikani yuko wapi. Polisi wakiulizwa wanadai bado wanaendelea na Uchunguzi....Huo wazi uko wapi Mzee wa Kijiji?
  • Mwandishi wa kujitegemea wa Mwananchi media ndugu Azory Gwanda jana ametimiza miaka 2 hajulikani aliko. Polisi wakiulizwa wanadai amejiteka mwenyewe!! Huo uwazi katika hili uko wapi Mwanakijiji?
  • Kutekwa kwa Mo Dewji likewise...!!!Hakuna uwazi wala ukweli katika tukio hilo!! Kuna siku JPM mwenyewe aliropokwa sijui kwa kuona haya au aibu ya Utawala wake alipowaambia Polisi kuwa Watanzania siyo wajinga...!!!Haiwezekani mtu tajiri na maarufu kama Mo atekwe Dar akae siku 9 nchi na vyombo vya Ulinzi na Usalama havijui mtu yuko wapi....!!!Lakini katika sekeseke hilo watu kama Makonda kama kawaida waliropoka kuwa Mo atapatikana akiwa mzima sijui kwa info gani aliyokuwa nayo..!!!Maana kama mtu ametekwa na magaidi, majambazi au wahuni na huna mawasiliano nao unauaje kuwa watamwachia akiwa salama? Na ndicho kilichotokea.Hapa kuna kitu HAKIJAWEKWA WAZI na kinajulikana vizuri sana na Rais Magufuli,IGP Ziro na Kamanda Mambosasa.
  • Yako mambo mengi sana ambayo utawala wa JPM hautaki kuyaweka wazi na hivo kuondoa hiyo sifa ya Uwazi wa kupitiliza..!!

  • Ngoja niishie hapa kwa kujaribu kujikuna kwa leo.
Akikujibu ni tag. Watu wanapoamua kutetea lazima waje na concrete reason. Na siyo hoja nyepesi kama hii ya MMK.
Binafsi namtetea sana rais kwenye jambo moja au mawili. La kwanza ni la kufufua treni ya dar Kilimanjaro hapo nampa heko kubwa sana. La pili ni lakuturuhusu kufyatua watt bila kuchoka. Yaan hapa napo nampa heko. Kwasabb sasa sitakuwa mhanga wa ddawa za kupanga uzazi😁
 
Back
Top Bottom