gfsonwin , mada za MM zimekuwa za ''kukaanga mbuyu na kuacha wenye meno watafune''
Kinachonigusa sana ni suala la kulinganisha ''utamu wa tango na Nanasi'' kwavile tu yote yanasemwa ni matunda. Hapa ni pale wanapomtaja Mwalimu kwa ulingano na waliomfuata
Mazingira ya Mwl Nyerere hayakuwa ya jana au juzi yalikuwa ya nyakati zake tofauti kabisa
Utasemaje Mwl hakujenga vituo vya afya ikiwa hatukuwa na hospitali za rufaa, Wilaya au mikoa?
Hoja rahisi ni ujenzi wa vituo 400 n.k. Mwl akipata Uhuru population ilikuwa milioni 9, hivi alihitaji vituo 400 vya nini ukilinganisha na population ya watu milioni 55?
Pamoja na hayo Mwl alijenga vituo vya afya na zahanati, na alama zake zipo kwa ushahidi
Tena vituo vya afya vikiwa na huduma muhimu ikiwemo magari ya kusafirisha Wagonjwa.
Wengi hawajui Hospitali ya rufaa ilikuwa Princess Margareth ikiwa na vile vijumba vya Makuti
Hatukuwa na chuo cha madaktari, muhimbili ili train Medical Assistant na AMO. Tuache hilo
Watu hawajui Reli ya Mnyuzi Tanga imejengwa wakati wa Mwl.
Gharama zake zingeelekezwa vituo vya afya na zahanati pengine tungekuwa na zaidi ya 400
Reli ya kati ilifanya kazi kila siku kama ilivyokuwa reli ya kaskazini, Tanga-Moshi- Dar
Hii reli ya kati haijengwi inakarabatiwa kwa kuifanyia ''improvement'' ya SGR
Hayo ni mbali na barabara, viwanda , shule , vyuo n.k.
Mwl hakusambaza umeme kila kijiji kwasababu alijenga mabwawa ambayo hadi leo hatuna bwawa jingine linalotoa umeme zaidi yake. Tunamsumanga Mwl kwa kutupa vyanzo
Tunaambiwa kuna elimu bure! hapana! elimu bure ilikuwa wakati wa Mwl.
Waulize Marais na mawaziri walisoma UDSM lini walichukua mkopo, wapi walilipa ada.
Tena walikuwa nyakati hizo walilipwa hadi nauli za kwenda na kurudi kutoka likizo
Mwl alichukua nchi akiwa na wasomi wa kiwango cha degree 5. Leo hali ipoje?
Watu hawaangalii changamoto za Mwl kuliweka Taifa pamoja na sisi kujivunia Utanzania
Ni kipi kinafanyika leo ambacho hakipo katika template ya Mwl Nyerere?