Anachokifanya ni kuhakikisha kuwa hakuna sehemu kubwa ya nchi ambayo inaweza kujihisi inapitwa. Ukiwasikiliza watu wenye kukosoa kinachofanyika “Chato” unaweza ukadhania Magufuli amegoma kufanya jambo lolote sehemu nyingine ya nchi. Hili linaweza kuwa ni udhaifu wa taasisi zenyewe kujieleza lakini kwa tunaofuatilia tunajua jinsi gani matanki ya maji, njia za umeme, hospitali, vituo vya afya, barabara, vinavyoendelea kujengwa au vilivyokwisha jengwa ndani ya miaka hii minne kulinganisha na miaka mingine yote.
Ukweli hata mimi nilimkosoa kuhusu baadhi ya miradi iliyofanyika Chato, baada ya kujipa muda wa kufuatilia miradi ya huduma muhimu na miundombinu nili jiridhisha Mh. Magufuli hana mfano kwa watangulizi wake isipokuwa Nyerere.
Nchi inajengwa kila kona na uchochoro kwa kasi ya ajabu.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, huyu mheshimiwa anafanya kazi kubwa mno.
Namuomba tu ajitathimini kwenye mambo ya suala la Uchaguzi serikali za mitaa na tamko lake la kuzuwia mikutano.
Kunge punguzwa au kulegezwa mashariti ya mikutano ya wanasiasa au basi pawepo na usawa na wa CCM pia wasifanye mikutano.
Kuliko hali ya sasa unamuona Polepole na wengine wanafanya mikutano huku wa upinzani wanasakamwa hata kwa baadhi ya mikutano yao ya ndani.
Nahisi hili la mikutano au vurugu za uchaguzi kuna mahali wasaidizi wake ngazi za chini kabisa hawajamuelewa wanamchafua.
Mwisho angewezesha wizara husika na BOT waruhusu Tanzania kupokea pesa kwa Paypal, maana hapa watu wengi wanataka kufanya biashara kirahisi nje ya mipaka ya Tanzani walete pesa za kigeni na hili limekuwa kikwazo kikubwa.
Uoga sijui unatoka wapi? maana hizo pesa mwisho wa siku lazima zipitie mfumo wa kibenki hivyo zitahakikiwa tu uhalali wake, hakuna utakatishhaji pesa.
Ajira ni chache na watu wana elimu na ujuzi wa kuuza au kufanya kazi kwenye mitandao, fungueni watu tujiajiri.