Swali Butu: Mambo haya 4 Magufuli anayafanya tofauti na Marais 3 waliomtangulia! Nani anabisha?

Swali Butu: Mambo haya 4 Magufuli anayafanya tofauti na Marais 3 waliomtangulia! Nani anabisha?

state agent,
Maskini weee!!! Yaani hapo ndiyo umechangia huu uzi ambao umeuita mwiba.
Hapa anaongelewa JPM tu na mambo ambayo ameyafanya tofauti na marais wengine wanne waliomtangulia. Wewe unalete habari ya DJ wa casino....!!! Wewe siyo State agent, ni Satan agent!
 

A load of rubbish, do you know the meaning of evidence? What you brought is not evidence. Bring the evidence what you alleged!
 
Mbona kama mnaogopa/mnakwepa sana kusema anamzidi hata Mwl. Nyerere pia? Mnawaonea tu kina Mwinyi, Mkapa na JK?

Wao pia kwa nafasi zao walifanya mengi tu tofauti na bora kuliko watangulizi wao na waliowafuatia. Mwinyi alileta biashara huria....aliachana na ujamaa kwa vitendo. Hili halikuwa Jambi dogo tena wakati Mwalimu angali hai. Mzee Mwinyi pia alirudisha demokrasia ya vyama vingi (ambayo awali ni Nyerere aliyeifuta). Hili pia sio jambo dogo. Huyu wa sasa anaturudisha nyuma sana katika hili. Na mengine mengine tu makubwa. Akaja mkapa pia amefanya mengi sana na kurekebisha mabaya ya mtangulizi wake.....kayasema mwenyewe juzi hapa kwenye kitabu chake. Magufuli amepata umaarufu kupitia utawala wa Mkapa na JK, sivyo? Ama zile kilometa za barabara za rami na madaraja aliokuwa anakariri hayana maana yoyote? JK pia alifanya mengi mazuri tofauti na watangulizi wake. Demokrasia ilishamiri zaidi, uhuru wa watu na vyombo vya habari pia ulishamiri. Mapato ya kodi yaliongezeka, biashara zilishamiri pia. Kajenga mabarabara na madaraja mengi tu (akisaidiwa na Magufuli), daraja la kigamboni, uwanja mpya wa ndege nk nk.

Bila shaka Magufuli pia anafanya makubwa na ya tofauti.

Wote kuna mabaya walifanya. Je inawezekana Magufuli pengine anangoza kwa mazuri na mabaya pia? A zero-sum game?
 
Back
Top Bottom