Swali fikirishi: CHADEMA ni chama cha Siasa, Harakati au Haki za Binadamu?

Swali fikirishi: CHADEMA ni chama cha Siasa, Harakati au Haki za Binadamu?

SOPINTO

Senior Member
Joined
Oct 19, 2020
Posts
155
Reaction score
387
Jina lake kamili ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kifupi chake ni CHADEMA kifupi ndani ya ufupi wa jina ni CDM, lakini kuanzia ngazi ya msingi ya hiki chama hakihakisi kabisa jina la chama hichi , sasa maswali yanakuja mengi na kutaka kujua hivi hiki chama ni cha mlengo gani?

Kuna wakati Chama cha Mapinduzi CCM ilikisaidia sana hiki chama kupanda kisiasa na wakati huo kilijizolea wabunge wengi sana ndani ya Bunge la Tanzania ikiwa pamoja na wanachama wengi kuanzia ngazi ya shina mpaka juu , wanasiasa maarufu nchini mfano kutoka CCM wakaamia katika hiki chama , mafanikio makubwa yakajitokeza ikiwa pamoja na hayati Kingunge Ngombare mwanasiasa nguli nchini ambaye ni mmoja wa waasisi wa CCM nae akaamia katika hiki chama.

Karibia wote hawa waliokuwa wanachama wapya walikuwa na mlengo wa kubadili mifumo ya uendeshaji wa hiki chama kwa lengo la kujikita katika misingi ya falsafa ya sayansi ya siasa na kwa asilimia kubwa walifanikiwa katika hilo kiashiria kimojawapo ni katika Uchaguzi mkuu wa 2015 , waswahili wanasema mazoea ujenga tabia , mapema baada ya uchaguzi mkuu falsafa ya sayansi ikawa inabadilika siku baada ya siku mpaka pale mwendazake alipoamua na kusema kuwa sasa hakuna shughuli za kisiasa mpaka msimu wa uchaguzi , mambo yakawa mambo.

Na hawa wanasiasa maarufu nchini baada ya kuona kuwa mazoea yamejenga tabia ambayo haiendani na falsafa zao pamoja na shinikizo kutoka CCM nao wakaamua kutoka na baadhi ya kauli zao ni kuwa kule bado hakueleweki maisha yao ni kama maisha ya Kambale kila mwanachama ni kiongozi basi nao wakarudi walikotoka.

Hivi karibuni Rais awamu ya sita akarudisha uhuru wa vyama vya siasa na kufungua milango na uwanja wa siasa ila akatoa angalizo kuwa kila mwanasiasa afanye siasa zake katika eneo lake , sasa cha ajabu wanachama wa chama cha Chadema wanachanganya watanzania na kuleta maswali ya kujiuliza je ; hiki chama kimesajiliwa kama chama siasa , harakati au haki za binadamu.

Yani hawajali hata hali ya afya iliyopo sasa wakati dunia na taifa linapambambana na UVIKO 19 na kutaka watu watulie katika maeneo yao bila kukusanyana viongozi wa chama hiki wanahamasisha wanachama wao kuja Dares salaam kutoka katika mikoa mbalimbali na kurundika katika mahakama ya kisutu, CHADEMA ni vyema mbadilike na muwe na mlengo maarum kama siasa iwe siasa , harakati basi tujue kuwa nyie ni wazee harakati na kama haki za binadamu basi tuelekee katika njia hiyo.

Asanteni.
 
Ukifuatilia siasa za dunia, utagundua mwanzo wa Democratic Party cha Marekani na Labour Party cha Uingereza, hivi ni vyama vilivyopingana na vyama vikongww vilivyolea matajiri kwa miaka mingi. Harakati za kuvisimamisha hivi vyama ilikua kama harakati wanazopitia Chadema sasa hivi.
 
Chadema ni chama cha siasa, kinachofanya harakati zake kupitia misingi ya demokrasia na utawala bora, chini ya mwamvuli wa haki za binadamu.
 
Chadwma ni chama cha siasa, kinachofanya harakati zake kupitia misingi ya demokrasia na utawala bora chini ya mwamvuli wa haki za binasamu.
Baada ya kusoma historia ya biashara ya utumwa mpaka ilivyokomeshwa na ukawa ndiyo mwanzo wa misingi ya haki za binadamu. Ninauhakika Chadema watafanikiwa hata kama itachukua muda.
 
Wewe tafsiri vyovyote ila cha muhimu Chadema inalinda na kutetea haki za raia.
 
Kama hili ni swali fikirishi kwako akili yako imedumaa
 
Back
Top Bottom