Swali fikirishi: Je, tunahitaji idadi kubwa ya watu ili kujikwamua kiuchumi au tunahitaji watu wenye tija kwenye uchumi wetu?

Ili tuwe na maendeleo inatakiwa nchi itengeneze mifumo inayowavuta watu kufanya Kazi za uzalishaji kwa kuzigeuza fursa zilizopo nchi kuwa ziada ya kupata pesa za kigeni
 
I dont think it is the problem of people being idle. Ngono ni utamaduni ambao umejengeka kwenye mindset na ilitakiwa viongozi wenye maono kuondoa ila ndivyo hivyo tena... hatuna. Unakuwa na viongozi wenye maono ya Magufuli unadhani hata wangefanya kazi namna gani ingesaidia? NB: sikatai kwamba kuwa idle kunachangia ila siyo sababu kuu. KIpindi cha Nyerere kulikuwa na kampeni kubwa sana ya uzazi wa mpango na ingeendelea mapaka sasa ungekuta watu wengi wanajitambua.
 
Viongozi hawapo kwa ajili yako, afrika uongozi ni ajira binafsi na sio wito wa kuipigania jamii, thus mifumo yetu ya sheria inawaogopa au ni butu kwa Wala rushwa na mafisadi
Correct 100%
 
Kuhusu swala idadi ya watu na maendeleo binafsi Nakuunga mkono ni Bora uwe na idadi ndogo ambayo ina tija kuliko ilivyo sasa watu shazi lkn matokeo hakuna
Agreed
 
Hao wajinga watachimba mitaro,watafanya kazi ngumu nk
Umewahi kutembelea nchi yoyote iliyoendelea? Hizo kazi za mitaro unazosema zinafanywa na wataalamu. Hlafu kazi ngumu sio lazima zifanywe na wasiokuwa na elimu kubwa. Kinachotakiwa ni kuimarisha mifumo ya technolojia ili isitumike nguvu kubwa sana, bali sayansi tu. Japo mannual work sikatai kwamba hazipo maana hata Ulaya zipo. Ila ni kazi zenye heshima ambapo mtu anafanya na anaweza kwenda vacation hata mara 3 kwa mwaka. Namnisha vacation ya kwenda hata nje ya nchi kufurahia maisha huko...
 
Ila we jamaa unajua umuhimu wa watu katika uchumi..?.kabla hujamuita mtu mjinga unatakiwa ufikiri kile alichokifikiri kipindi anahamasisha watu wazaliane kwa wingi..

Unajua watu ndiyo soko la bidhaa zinazozalishwa na viwanda na hayati Magufuli alikuwa na agenda ya kuhamasisha ujenzi wa viwanda vingi hapa nchini ili kuzalisha bidhaa zenye soko la uhakika..kwa hiyo ingesaidia kuimarisha makusanyo ya kodi ambayo ingetumiwa na serikali kujenga na kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu..

Pia idadi kubwa ya watu itasaidia kuongeza matumizi ya huduma za kijamii kama maji , umeme, afya, n.k.hii itasaidia kuongeza mapato serikalin...

Yote haya yanasaidia katika kukuza uchumi wa nchi yetu...alafu hata hao wazungu kipindi wanaanz kujenga nchi zao pia walikua na idadi kubwa sana ya watu na walikua na viwanda vingi sana hivyo walizalisha na kuuza na bidhaa nyingine kukosa masoko na kuanza kutafuta masoko nje ya nchi zao ndo ikabidi kuja huku africa na huko asia ili kupata wateja wapya kwa kubadilishana madini kwa bidhaa za viwandani..

So watu ni rasirimali katik ukuaj wa uchumi kikubw ni serikal kuwek misingi mizuri kutumia rasirimali watu kwa ukuaji wa uchumi...

#fikiri kabla ya kuzungumza.
#mdomo huponza kichwa.
 
Hakuna mtaalamu atachimba mtaro au kuchapia ukuta,hizo ni kazi za mafundi Wala hazihitaji Elimu Bali skills za kuona na Kutenda.
 
Hakuna mtaalamu atachimba mtaro au kuchapia ukuta,hizo ni kazi za mafundi Wala hazihitaji Elimu Bali skills za kuona na Kutenda.
Ndio maana nikakuuliza umewahi kutembelea nchi zilizoendelea? Nchi zilizoendelea kazi za ujenzi hazifanywi na washinda juani kama bongo... Mfano Ulaya vitu vingi (sio vyote) vinafanyika kwa machine. Sasa unaweza okota mtu mtaani akaweza ku-operate machine ya kuchimba mtaro bila ya kuw ana skills?
 
Ni kweli.

Nyerere mwenyewe alikutana na tatizo la mfumuko wa kuzaliana watu. Katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa kwanza baada ya uhuru, Nyerere na serikali yake walijipanga sana kutoa huduma kwa wananchi, kujenga hospitali, madarasa etc.

Wakakaa chini na kuangalia figures, wajenge nini wapi, wafanye nini, wakajipanga kweli. Watu walikuwa na ari kubwa, motisha kubwa sana ya kujenga nchi kwa sababu ndiyo kwanza walikuwa wamepata uhuru kutoka kwa mkoloni.

Baada ya kuisha ile miaka mitano, wakakuta hali bado ni mbaya sana, kwa sababu licha ya kwamba walijipanga sana, lakini kuna kitu kimoja walikuwa wamekidogosha, hawakupiga hesabu la ongezeko la watu.

Wakajikuta wana deni kubwa sana la kuongeza huduma, kwa sababu hata ukipiga hesabu za kukidhi mahitaji ya watu ya leo, by the time unakamilisha mipango na ujenzi etc, huduma zinaohitajika zinakuwa zaidi ya zile ulizotoa, simply by population increase.

Kibaya zaidi, ukizaa watoto wengi unahitaji miaka mingi ya kuwalea na kuwasomesha kabla hawajawa productive members of society, hapo maana yake uchumi wako uwe imara katika kutoa huduma tu bila wanaopewa huduma kuchangia, hapo kwetu ni kizungumkuti.
 
Huku ni kufikiria ukiwa umejifungia ndani ya box. Inaonyesha jinsi elimu yetu ilivyo ya kiwango cha chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…