Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Swali funyukuzi. Dah. Umetisha!!
Siyafahamu ila tunayoyasoma kwenye magazeti ndio yanashangaza, naona hata mabeberu wameng'aka kwanini CCM isihinde 99.9%
US and UK protest after Tanzania ruling party's 99.9pc win
US and UK embassies say poll officials "overwhelmingly" disqualified opposition candidates.www.theeastafrican.co.ke
Hata wewe mnafki usipakaze mabaya ya mtu ikiwa wewe auko safi tena kwa maneno ya kuambiwa.Unafiki ndio sifa namba moja ya kiongozi hapa Tanzania, sifa ya pili ni uongo na sifa ya tatu ni ujinga. Ukiwa nazo hizo sifa na ukazitumia vizuri atavuna vyeo vya dezo hapa Tanzania mpaka unazeeka na kuingia kaburini.
Ndio anachokifanya Professor Kabudi.
Wakitoka nje ya nchi wanarudishiwa akili zao, wakifika Namanga wakabidhi akili zinahifadhiwa Lumumba.
Sasa mkuu ulitaka akushauri muendeleze mivutano ya ki siasa au vp nyie mmemualika ilitakiwa asemaje
[emoji238][emoji238][emoji238]Siyafahamu ila tunayoyasoma kwenye magazeti ndio yanashangaza, naona hata mabeberu wameng'aka kwanini CCM isihinde 99.9%
US and UK protest after Tanzania ruling party's 99.9pc win
US and UK embassies say poll officials "overwhelmingly" disqualified opposition candidates.www.theeastafrican.co.ke
Na akipanda ndege ataziokotea akili zake airportNimecheka sana kwa hii kauli, ina maana huyu akigeuza kuja huko, akivuka mpaka Namaanga itabidi ashushe hizi akili alizo nazo huku.
Jikite kwenye mada..Sisi hatuna ukabila ulioota mizizi kama kwenu Kenya!
Well SaidUnafiki ndio sifa namba moja ya kiongozi hapa Tanzania, sifa ya pili ni uongo na sifa ya tatu ni ujinga. Ukiwa nazo hizo sifa na ukazitumia vizuri atavuna vyeo vya dezo hapa Tanzania mpaka unazeeka na kuingia kaburini.
Ndio anachokifanya Professor Kabudi.
Kuna watu wanafki umu wajipandikizia chuki wenyewe kwa maneno ya magazeti ya siasa na mitandaoni na ndio hao awafanyi kazi wanapiga mboyo ela ziachiwe.Tatizo la ukabila la Kenya sio la kusadikika au kudhani, ni la muda mrefu toka nchi hio ipate uhuru wake.
Tatizo hilo la ukabila limekuwa lilisababisha maelfu ya raia wa Kenya kuwa displaced ndani ya taifa lao na pia watu wengi kupoteza maisha.
Tatizo hilo la ukabila limesababisha kabila moja la Kikuyu kutawala Kenya toks nchi ipate uhuru (ukimuondoa Moi).
Kenya si ndio ilikua na best constitution lakini ineshindokana kwa sababu ya huohuo ukabila, ndio maana wanakuja sasa na BBI ili kusawazisha mambo....
Kwahiyo unataka kusema alichokifanya Kabudi huko Kenya sio unafiki?Hata wewe mnafki usipakaze mabaya ya mtu ikiwa wewe auko safi tena kwa maneno ya kuambiwa.
Jirani fuata wasemayo usifuate watendayoNimeisikiliza hotuba ya Profesa Kabudi wa kutokea Tanzania, kwa kweli ametiririka maneno yenye hekima na kutuasa Wakenya tuwe kimoja, pia akamsifia sana Rais wetu Uhuru kwa kukubali kujishusha na kuweka uzalendo mbele na kukaa meza moja na wapinzani kwa minajili ya vipaumbele vya taifa.
Nikawa najiuliza mengi, maana taarifa tunazozisoma kuhusu Tanzania zinakinzana na huu ushauri wa Professa kwa asilimia 100%, kule watu wamegawanyika kwa misingi ya vyama, yaani juzi tu chama kinachotawala kimeibuka na ushindi wa asilimia 99% baada ya upinzani kutunishiwa misuli hadi wakajiondoa.
Tumekuwa tukiona matamko na mikwara ya waliopo kwenye dola wakiweka wazi bila kuremba kwamba maeneo ya upinzani yanakosa maendeleo kama adhabu ya maamuzi yao mabaya.
Mifano ni mingi tu ambayo tunaisoma inayodhihrisha demokrasia ilivyofukiwa kwa Wabongo, sasa professa, hivi alikua anatuma ujumbe kwao nyumbani kinyemela au alikua na maana gani.
Pia juzi tuliona Spika wa Tanzania alitutembelea hapa Kenya na kusifia sana mfumo wetu wa kurusha shughuli za bunge mubashara, licha ya yeye kule kwao kubana hayo hayo aliyokuwa anasifia, sielewi mbona wakija huku wanasifia mambo ambayo wenyewe kwao wanayakandamiza na kuyadidimiza.