Swali fukunyuzi: Kabudi katuasa vizuri sisi Wakenya, ila mbona huko kwao Tanzania hawazingatii haya haya anayoturai?

Swali fukunyuzi: Kabudi katuasa vizuri sisi Wakenya, ila mbona huko kwao Tanzania hawazingatii haya haya anayoturai?

Unafiki ndio sifa namba moja ya kiongozi hapa Tanzania, sifa ya pili ni uongo na sifa ya tatu ni ujinga. Ukiwa nazo hizo sifa na ukazitumia vizuri atavuna vyeo vya dezo hapa Tanzania mpaka unazeeka na kuingia kaburini.

Ndio anachokifanya Professor Kabudi.
Hata wewe mnafki usipakaze mabaya ya mtu ikiwa wewe auko safi tena kwa maneno ya kuambiwa.
 
Sasa mkuu ulitaka akushauri muendeleze mivutano ya ki siasa au vp nyie mmemualika ilitakiwa asemaje
 
Ili jamvi lina unafki ndani yake hata huyo kabuni ni profesa tu na sio mwanasiasa kama mnavyompigia kelele.
 
Sasa mkuu ulitaka akushauri muendeleze mivutano ya ki siasa au vp nyie mmemualika ilitakiwa asemaje

Ndio maana nikaanza kwa kusema ameshauri vizuri na tumepokea ushauri wake, ila nikahoji kwanini huu ushauri hauzingatiwi huko alikotoka, leo hii Watanzania mumegawanyika kwa misingi ya vyama hadi mnafanya mambo ya ajabu kama baadhi yenu kushangilia ndege kukamatwa, wengine kushangilia timu ya taifa kushindwa, yaani uzalendo wameushusha kwa ajili ya hiyo migawanyiko.
Ni muhimu na nyie mkaiga hili la BBI, mlitekeleze kwa kuwaleta Watanzania wote wawe kimoja, rais akubali kushuka na kukaa meza moja na wapinzani kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi. Pia muache mikwara na kauli mnazotoa za kuonyesha maeneo ya upinzani yanatengwa kimaendeleo kama adhabu ya maamuzi yao mabaya.
Upinzani wametunishiwa misuli hadi wakajitoa kwenye uchaguzi ikapelekea CCM kunyakua ushindi wa 99.9%
Hivi unafikiria mamilioni ya Watanzania ambao wako kwenye mlengo wa upinzani wanahisi vipi kwa sasa.

Hicho hicho tulikua nacho huku, kwamba mlengo wa serikali unashinda ila kwa nja zisizo wazi, mamilioni ya wafuasi wa upinzani wanabaki wakiishi maisha ya hasira na chuki, taifa la kihivyo sio kabisa, muhimu kurekebisha.
 
Nimemsikiliza Kabudi Youtube, japo Wakenya wengi wanamsifia ila alichoongea nadhani ni uongo na unafiki

Hasa aliposema eti Wakenya waache politics of Power wawe na politics of development, huu ni unafiki mkubwa hasa ukiangalia uchaguzi ulivyofanyika kibabe juzi hapa Tz, na siasa zinavyoendeshwa kiujumla hapa.

Pia alipowaambia eti Wakenya waache kutukuza Ukabila, kwani Tz hatukuzi ukabila wala hatujuani makabila yetu

Ni kweli Kenya kuna ukabila zaidi ya Tz, lakini Tz pia ukabila unachipua na anayeumwagilia maji ni boss wake

Magufuli kila mara amekuwa akiwalazimisha viongozi majimboni mwao wazungumze kilugha na wananchi, akiwaambia kuzungumza kikabila kutawafanya wananchi wajue kuwa ni "mtu wao", huku sio kutukuza makabila?

Magufuli pia amekuwa akitamka sana na kufanya utani wa kikabila (ambao mara nyingi unakera) utasikia akiwaambia nyie Wafipa wachawi, Wagogo wavivu, Wachaga wanapenda hela, Wasukuma sisi hatuna mchezo n.k, huku sio kupalilia ukabila?
 
Tatizo la ukabila la Kenya sio la kusadikika au kudhani, ni la muda mrefu toka nchi hio ipate uhuru wake.

Tatizo hilo la ukabila limekuwa lilisababisha maelfu ya raia wa Kenya kuwa displaced ndani ya taifa lao na pia watu wengi kupoteza maisha.

Tatizo hilo la ukabila limesababisha kabila moja la Kikuyu kutawala Kenya toks nchi ipate uhuru (ukimuondoa Moi).

Kenya si ndio ilikua na best constitution lakini ineshindokana kwa sababu ya huohuo ukabila, ndio maana wanakuja sasa na BBI ili kusawazisha mambo.... Johnny Sack,
 
Siyafahamu ila tunayoyasoma kwenye magazeti ndio yanashangaza, naona hata mabeberu wameng'aka kwanini CCM isihinde 99.9%
[emoji238][emoji238][emoji238]
FB_IMG_1574842071699.jpeg
 
Unafiki ndio sifa namba moja ya kiongozi hapa Tanzania, sifa ya pili ni uongo na sifa ya tatu ni ujinga. Ukiwa nazo hizo sifa na ukazitumia vizuri atavuna vyeo vya dezo hapa Tanzania mpaka unazeeka na kuingia kaburini.

Ndio anachokifanya Professor Kabudi.
Well Said
 
Watu wa chama hicho ndivyo walivyo wanajali mkono uende kinywani. Watetezi wakubwa wa awamu ya nne leo hii wanasema tulikuwa tunapotea. Kizuri watu wengi wameanza kuwastukia.
 
Tatizo la ukabila la Kenya sio la kusadikika au kudhani, ni la muda mrefu toka nchi hio ipate uhuru wake.

Tatizo hilo la ukabila limekuwa lilisababisha maelfu ya raia wa Kenya kuwa displaced ndani ya taifa lao na pia watu wengi kupoteza maisha.

Tatizo hilo la ukabila limesababisha kabila moja la Kikuyu kutawala Kenya toks nchi ipate uhuru (ukimuondoa Moi).

Kenya si ndio ilikua na best constitution lakini ineshindokana kwa sababu ya huohuo ukabila, ndio maana wanakuja sasa na BBI ili kusawazisha mambo....
Kuna watu wanafki umu wajipandikizia chuki wenyewe kwa maneno ya magazeti ya siasa na mitandaoni na ndio hao awafanyi kazi wanapiga mboyo ela ziachiwe.
 
Nimeisikiliza hotuba ya Profesa Kabudi wa kutokea Tanzania, kwa kweli ametiririka maneno yenye hekima na kutuasa Wakenya tuwe kimoja, pia akamsifia sana Rais wetu Uhuru kwa kukubali kujishusha na kuweka uzalendo mbele na kukaa meza moja na wapinzani kwa minajili ya vipaumbele vya taifa.

Nikawa najiuliza mengi, maana taarifa tunazozisoma kuhusu Tanzania zinakinzana na huu ushauri wa Professa kwa asilimia 100%, kule watu wamegawanyika kwa misingi ya vyama, yaani juzi tu chama kinachotawala kimeibuka na ushindi wa asilimia 99% baada ya upinzani kutunishiwa misuli hadi wakajiondoa.

Tumekuwa tukiona matamko na mikwara ya waliopo kwenye dola wakiweka wazi bila kuremba kwamba maeneo ya upinzani yanakosa maendeleo kama adhabu ya maamuzi yao mabaya.

Mifano ni mingi tu ambayo tunaisoma inayodhihrisha demokrasia ilivyofukiwa kwa Wabongo, sasa professa, hivi alikua anatuma ujumbe kwao nyumbani kinyemela au alikua na maana gani.

Pia juzi tuliona Spika wa Tanzania alitutembelea hapa Kenya na kusifia sana mfumo wetu wa kurusha shughuli za bunge mubashara, licha ya yeye kule kwao kubana hayo hayo aliyokuwa anasifia, sielewi mbona wakija huku wanasifia mambo ambayo wenyewe kwao wanayakandamiza na kuyadidimiza.
Jirani fuata wasemayo usifuate watendayo
 
Back
Top Bottom