Wewe kabila gani,
Mtu akiniuliza hivyo tu, au hata nikimsikia kwa pembeni akiuliza hivo, namuona ni mtu fulani hivi yuko nyuma sana.
hasa katika mazingira ya kuhitaji msaada, and then mtu anakurupuka "we kabila gani"
Ukimwambia mimi sina kabila, utasikia, "utakosaje kabila bwana"
Ukimwambia basi mimi msukuma, au mimi mpare au mimi mmasai au mimi mnyatulu,
utamsikia akitaka akusemeshe kwa lugha ya kabila ulilotaja,
Asijue wengine tumezaliwa dar, tumesoma ujerumani,
Mara nyingi tu huwa tunashinda Hong kong kwenye maswala ya kibiashara na jioni tunaenda kupumzika Paris.
Kwahiyo hatujui kimatumbi hata cha kuombea nyapu.