Swali gani hupendi kuulizwa?

Swali gani hupendi kuulizwa?

Au pale unapoenda kuomba kazi kwenye kampuni ya ulinzi kwenda kulinda Godown tandale huko kisha wanakuuliza kama unajua kiingereza, utadhani vibaka wa Tandale wana PHD ama wametoka ughaibuni!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]weka picha
Hio
Screenshot_20191010-222828~2.jpeg
 
Katika mazingira yetu tunayoishi au mazingira ya shughuli zetu za kila siku tunakutana watu tofauti ambao wametoka sehemu mbalimbali iwe mikoani au nje ya nchi ambao wamekulia mazingira tofauti.

Kuna watu wanapenda kudadisi vitu ambavyo hawavihitaji au hakuna faida yeyote wanapata ila basi tu na mwengine anakuuliza apate sababu ya kukudharau au ubaguzi.

1.Mimi sipendi mtu aniulize wewe kabila gani. Siku hizi wamebadilisha style wanakuuliza mtu wa wapi?

2.Umeoa hata miezi 3 haijaisha mtu anauliza vipi ndoa ishajibu?

Hayo maswali mi sielewi mtu anauliza ili iweje au anafaidika nini akijua hayo!

Tushare pamoja maswali ya kipumbavu kama haya.
Sipendi maswali ya konda. Unatoa nauli anakuuliza wangapi
 
Back
Top Bottom