Israel imewahi kupigwa na njaa na kukimbilia Misri kuwa watumwa miaka Mia nne, imewahi kupigwa na babeli na kuuwawa watu wengi , waliobaki walihamishiwa utumwani kwa mamia ya miaka,
Imewahi kupigwa na Rumi, nyumba zote zilibomolewa na, mamilioni ya watu waliuawa na wachache waliobaki walitawanywa dunia nzima ili kuuwa na kufuta kabisa kizazi Cha wayahudi na jina la Israel, warumi ndio waliobadili jina la Israel na kuiita palestina,
Israel imepigwa na kutawaliwa na mataifa mengi ikiwapo ninawi, wafilisti, wasyria, wagiriki n.k wamefanyiwa maangamizi ya halaiki na wajerumani
Katika vipigo vyote washangiliaji na wazomeaji wakubwa walikuwa ni waarabu na wapambe wao
Hatimae mwisho, baadae ya miaka 2000 ya kusambazwa duniani, kuuwawa na kufutwa kabisa, taifa limerudi palepale na jina lile lile Israel.
Ni taifa pekee duniani lililo pita kwenye Moto uteketezao, na uangamizao bila kuteketea. Hakuna taifa linaloweza kupitia kwenye historia Kama hiyo na likabaki salama