SWALI: Hivi huyu Mrisho Mpoto ndio nani?!

SWALI: Hivi huyu Mrisho Mpoto ndio nani?!

Anajaribu kujiweka watofauti aslongest yeye ni Msanii lazima afanye Mambo tofauti sababu inambidi awe hivyo,

kumuongelea tu inatosha kuwa shabiki yake damu damu.

hahahahaha wauza viatu lazima wanamchukia sana huyu Jamaa.
Shabiki wa Rasta Farai?!
Rasta Farai Bongo?!
 
Hongera Sana MWIJAKU na NICOLE KWA KUFUNGA NDOA KWENYE WIMBO WA KIKI.

-Mrisho Mpoto ni Mchumia tumbo flani hivi ambaye kapewa masharti na mganga hasivae viatu ili aendelee kupata mali,anatuzuga kwamba kutembea peku ni afya sasa kama anajali afya mwili wake asingeuachia namna ile.
aisee...inaweza kua namna yake tu ameamua
 
Yassora_0403151436-meme.jpg
 
Sweet heart Honey Money Penny

Mrisho Mpoto ni kijana mdogo tu aliyeamua kufuata nyayo za nguli wa Sanaa za maonesho, Dr Mgunga wa Mnyenyelwa. Huyu alikuwa mwalimu wa Sanaa, Maigizo na lugha pale chuoni mlimani. Aliandika jina lake hapa nchini baada ya kifo cha Mwl Nyerere aliporindimisha kibao kiitwacho "Nenda Mwalimu" akina na kikundi cha Parapanda Arts. Ngoma hii haikueleweka vema maana ilijaa tashtiti, tafsida,_ki za masharti, majigambo na simanzi kwa wakati mmoja. Mgunga hakueleweka vyema.

Hapo ndipo mwanagenzi Mrisho Mpoto alipoazima jani. Hana ufundi wa Mgunga, lakini anaufundi wa biashara. Siri ya Mrisho ni kuchanganya mashairi, tashtiti, tamathali, ngeli, ghani na majigambo pamoja na vionjo vya muziki wa kizazi kipya na wanamuziki wake. Hii imemsaidia kwa kiasi Fulani maana wapenzi wa muziki hasa vijana wanavutiwa na kazi za Mrisho.

Kwa nini havai viatu, kwa nini anavaa gunia/magunia na ngozi (wakati mwingine)?. Yeye husema anaenzi tamaduni za Kitanzania. Nionavyo amekusudia Hii iwe "brand" yake. Amekusudia kuwa na muziki tofauti na mavazi tofauti. Anakusudia kuuza mavazi haya pia japo kutovaa viatu naona itakuwa ngumu kwake kupata wafuasi. Ni mthubutu ndio maana tunamjadili.Ametazama mbali.

Atafanikiwa kutambuliwa kama muasisi (pioneer) wa aina ya muziki anaofanya na mavazi anayovaa? Ni swali linalosubiri muda kupata majibu.


Doh
Sawa Pr wa Mrisho
 
Watanzania tuna husda sana.....!!!

Sijui ni kwanini tu nashindwa kutambua mipaka yetu..!!!

Sijui ni kwanini tunapenda ku dictate maisha ya watu..!!

Kama yeye ana enjoy kutembea peku ni sawa...as long as huko kutembea peku hakuingiliani na uhuru wa wengine..!!!!
Sawa Lawyer wa Mpoto
 
Back
Top Bottom