Hii ilimtokea rafiki yangu wa karibu, kuna mkaka alikosea namba ndio ukawa mwanzo wa mawasiliano kipindi hicho tulikuwa kidato cha nne tukawa tunajisomea pamoja usiku yaani rafiki yangu alikuwa anaongea tu na simu usiku wote hana muda wa kusoma.
Yule kaka alikuwa anaishi moro siku hiyo akasema nakuja dom kuna mzigo naleta huko nataka tuonane maana hata mie nilikuwa naongea nae kwa simu ya rafiki yangu. Ilikuwa ijumaa tukawahi kurudi mwenzangu akajiandaa kwenda kumuona mgeni wake kurudi huko mwenzangu kabadilika yaani amekasirika anasema yaani toka nimezaliwa sijawahi kuonana na baba mwenye sura ngumu kama yule [emoji1] [emoji1] [emoji1].
Kesho yake alikuwa anarudi moro akamwambia kesho uje na shemeji nimuone(mie huyo) jamani kufika nje ya hiyo guest aliyofikia akampigia atoke nje tumefika alikuwa amevaa bonge la suruali la kitambaa na shati la mikono mirefu juu kofia.
Kwenye simu alikuwa na sauti nzuri hatari kuja kumuona nikabaki hoi.
Nilicheka njia nzima kama chizi hadi kufika nyumbani nacheka mwenyewe naulizwa unawehuka? Toka hapo yule baba akipiga simu utasikia hili nalo na matusi juu [emoji23] [emoji23] [emoji23]