Swali: Je, umeshawahi kumkimbia mtu baada ya kumkuta ndivyo sivyo? (with updates)

Swali: Je, umeshawahi kumkimbia mtu baada ya kumkuta ndivyo sivyo? (with updates)

Hahahaa. Umeonaeee.

Huku inabaki kuwa siri yako na kicheko kinakuwa hakiishi haswa ukute ni wale waliojaa tambo na madharau basi unabaki kucheka tu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mme wangu akiii wewe ulinifanyia nn mbona sikukukimbia[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Jang'ombe kuna nini vile? Jumlisha na [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji23] [emoji23] [emoji779]
Tunguri.jpg
 
Mm nahisi hujiamini kama ni mzuri ndio sababu huwa unakimbia,ktk thread zako zote hujawahi sema umekimbiwa,unajihami mapemaa
Naona Mkuu mvua imekuvuruga , maaana jibu lako hata sijalielewa hvi ,na mwisho kabisaa nlisema labda wao huwa wanakimbia na hapa swali ni je hujawahi kumkimbia mtu? huko kwingine ni wapi tena leta huo uzi
 
Wasaaaam!

Hapa nazungumzia zaid kwenye suala la kutongozana kati ya mwanamke na mwanaume.

Katika harakat za maisha mm kama Demiss uwiiiii nimeshawakimbia sana wanaume baada ya kukutana na vituko .

1.Huyu alikuwa mwanaume aliyekosea namba tukawa tunawasiliana zaid ya mwaka mmoja bila kuonana maana yeye alisema hana account facebook wala hayupo whatsap.
Basi alishiaa kuniambia tu sifa zake jinsi alivyo kwenye simu kuwa mweusi mrefu wastani na nguo anazopendelea kuvaaa akimaniisha hapo tayar nitahisi anafanana vipi .Aiseeh nilimwambia unafanana na Joh Makini akasema ndiyo .[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Na mm bila kukaaa nyuma nikamweleza sifa zangu yani muonekano wangu jinsi nilivyo kama Black chocolate ,mrefu alafu mwili wa wastani nina chura chokozi na ninapenda kusukaaa macho ya mviringo kama gololi.
Hapo mwanaume akavuta picha nafanana kama Alicia keys.

Balaa sasa siku ya kuonana nakumbuka nilikuwa nimeenda Jitegee sekondary kuchukua uhamisho wa Mdogo wangu basi kwa sababu yule mkaka alisema anafanya kazi Mitaa ya Uhasibu nikasema leo ndo siku ya kuonana maana kipindi tunawasiliana mm nilikuwa mkoan Morogoro hivyo nilikuja Dar kwa masuala ya uhamisho wa mdogo wangu.

Basi baada ya kumaliza issue zangu nikaenda kukaaa pale kituo cha uhasibu kwa ajili ya kusubiri gari za Mbagala huku nawasiliana na yule mkaka aje tuonane .

Uwiiiii nilikuwa nimekaa kwa machale najua mnaelewa mchezo wa kuviziana na mtu usiyemjuaaa inavyokuwaaa ni balaaaaa akipig simu unachelewaa kupokeaaa unaangalia nan anayekupigia[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Uwiii ghafla vuuup namuona mkaka anakuja amevaa likaptulaaa kubwaaa halimtoshi alafu kachomekea na Tshirt jaman chini kavaaa mabuti ni anatishaa jaman uwiiiii(Mnisamehe Demiss napenda mahanshaamy mnanijua lakini)

Mkaka alikuwa anatisha uuuuuuh nisingeweza kumvumilia kwa kweli nilitoka nduki nikaingia kwenye DCM zile zilizokuwa zinaenda Mbagala Rangi 3 na Mbagala kuuu.

Kituko sasa badala ya kupanda Gari za Kwenda Mbagala Rangi 3 nikajikuta nimefika Mbagala kuu hapo simu nimeizima kabisaa
Nilivyofungua sm nilikutana tu na sms za kwann nimemkimbia mm wala sikujibu nikapotezea.

2.Sharobaro mwembamba
Katika maisha hakuna kitu sikipendi kama wanaume wembamba alafu warefuu .
Huyu mkaka sharo nakumbuka sjui alikosea namba na yeye alikuwa anakaa Kimara suka huko tukawa tunawasiliana .

Baadae akawa amenitumia nauli nitoke Moro niende Dar nikasema niende kuonana na mtu simjui wala siwezi nikikutana anafanana kama kibwengo nitafanyaje sitak aiseeee ikabidi ile nauli iishie kwenye mitumba ya Sabasaba sokoni watu wa Moro mnaelewaa shughuli ya Sabasaba.

Basi yule mkaka akaona isiwe tabu ngoja aje mwenyewe mpaka Morogoro aje tuonane.
Siku hiyo nikaenda kukaaa pale Vijana social hall ipo maeneo ya sabasaba ila nilikaa pembeni yake nikawa nampa Direction huyo mkaka aje mpaka Geti la vijana social.

Jaman alivyofika ni mwembamba mrefuu alafu kavulana kadogo kiukweli mm nisingeweza nilivyojiridhisha ni yeye nikazima simu alafu nikapita pale pale alipokuwa amesimama nikaenda zangu kuchukua bodaboda nikasepa zangu Home.(Uwiiii kaka unisamehe nisingeweza)


Ila jaman haya yalikuwa maisha ya kupita tu na ilikuwa ni lazima itokeee hivyo msinilaumu sana.

Bila kusahau kuna member moja wa hapa Jamiiforum nilishawahi kumkimbiaaa jamn sikutegemea kama ningemkuta hivyo nilitoka ndukiiii[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]nusu nivunje milonjoo kwa sababu alinitumia picha siyo zake siku namuona weeeee nilikimbiaaa Mwendo kama Chopa za Urusi.



Mrs Jr chamdeko.
Hv vitu bado vinatookea mpaka kipindi hiki????.... Ckuhizi kila mtu ana smart phone... So video call ndio solution... Siwez kutana na mtu bila kumpiigia video call kwanza
 
Sitosahau kipindi nasoma advance lyamungo secondary. Kuna mwana mmoja akapata manzi fb dem kapost picha kali ajabu. Jamaa karusha sound mtoto kaelewa. Ikawa siku moja tumekuja kishule moshi town maeneo ya hindu mandal kuchangia damu salama. Jamaa akasema ngoja nimchek yule demu tumekaa upande wapili wa barabara dem akasema nakuja tukasubiri alipofika jamaa anataka kukimbia demu akaita kwa nguvu wee nimeshakuona subiri nivuke. Aisee alikuwa mnene ajabu halafu mrefu so akawa kipande cha mtu. Dem kamganda jamaa ajab had akakubali kwenda kuchangia damu. Ajabu ni kwamba alifungwa mikono yote hakuonekana mshipa wakampa soda na biskuti wakamwambia tunashukuru maana ulikuwa na nia ya kuchangia ila afya imekataa[emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mim kuna mtu alikoseaga namba ikaja kwangu kupokea sauti nzuriii mweee ,tukawa tunaongea tu ,tunawasiliana tu nikawa namuwazia atakuwa bonge la handsomee ,,siku naenda kuonana naee kidogo nizimieee limtu kama Li lemutuz halaf mi kadogoo nikamsalimia shikamooo baba ,wakati kwenye simu nilikuaga simsalimiii ,nikamuambia nimepita tu tutaonana baadaee [emoji23][emoji23],,nikivyotoka hapooo nilibadili na laini na ya simu maana kidogo nizimiee
 
Back
Top Bottom