Miaka ya 2007-2010 nikiwa naishi Arusha, na kitambo hicho mig33 ikiwa juu sana, RFK yng aliopoa mrembo wa kutoka Tanga.
Lile basi la Tanga liliingia Arusha mida Saa 2 usiku. Mshkaji akaniomba nimsindikize kumpokea "Mgeni" wake. Alinisistiza nimsindikize kwanza kwa sababu za kiusalama na pili alinambia ndio Mara ya kwanza wanakutana, so km hatakidhi viwango, ajue jinsi ya kuchoropoka!
MSHKAJI akasema tukikaribia stand, tutembee Mbali Mbali mm na Yeye. Na niwe namuangalia (yeye mshkaji) muda ote, akipokea simu na mm nijifanye napokea simu, akiongea na Mimi nijifanya naongea, lengo ni kumpoteza maboya!
Wakati tunakaribia stand, eneo ambalo bint alisema amekaa, mshkaji akamuona na hapo HAPO akasema NIMEINGIA CHAKA!
Maskini tulimpita yule Dada km sio sisi, daah zilikuwa akili za Chuo Chuo zile!