Nakumbuka nilipokuwa nasoma mlimani kipindi hicho mtandao maarufu ulikuwa hi5 basi kule nikakutana na kijana mmooja matata yaan pichaa alizokuwa ananitumiaa zilikuwa balaaa mtoto wa kike nikadataa though mi zangu zilikuwa za ukweli,basi bwana siku zikaenda tukawa tushazoena yeye alikuwa anakaa mbezi mi nakaa hall 3 basi siku ya siku akaniambiaa anataka tuonane basi bwana nikamwambiaa anifate chuo na tulipanga tuende kwanza best bites coz ilikuwa mchana for lunch.tukakubaliana mi nikawa nipo sana xcited kuonana na mkaka handsome hatareee yaan inshort alikuwa kakamilika kila idara,basi bwana sikutaka anifate kule hall three nikamwambiaa atanikuta container.Basi mtoto wa kike nikauparaaa balaaa akaniambiaa amekaribia pale udasa basi na mm nikajisogeza kituo cha container ....nikawa nimesimama nikshangaa gari limepaki upande wa pili kama unaelekeaa kule utawala......ili kuwa discover nyeusi full tinted ,akanipigiaa simu nimeshakuonaa njoo upande wa pili uingiee ndani ya gari ,nikavuka ile nafunguaa mlango jaman nikishtukaa balaaaaaa manake nilikutana na mbaba mtu mzima zaidi ya baba angu yaan kwa uogaa nikajijutaa namsalimiaa shikamoo baba akaniambiaaa achaa zako,akagunga milango tuakenda jaman alijuaa kanisa sipo comfortable manake mpka tunafika kule nilkuwa kama msukule na yy alilitambuaa hilo basi tulivyomaliza kulaa akanirudisha akajiongeleshaa weee nikashuka akanipa ela nikarudi zngu room jaman baaada ya hapo nolimblock kilaa sehemu....na sijuwasiliana naye tena
Though baadae nilikuja kumuona kwenye tv flan nikajuaa kazi yake na mpkaa sasa najuaa anapofanya kazi na kitengo alipo ila sijawah mtafutaa!!!