Sitasahau Kipindi Nimejiunga Badoo Miaka Hiyo Na Kisimu Changu Cha Nokia C2. Nilikuwa Nawatambishia Masela Kitaa Kwa Totoz Wazuri Wa Badoo . Sasa Ikifika Katika Kuscan Yupi Wakutoka Nae Ili Nikomeshe Roommate Baada Ya Kurudi Chuo Udsm. Nikampata Mmoja ( Jina Kapuni) Kwa Mujibu Wa Picha Alikuwa Ana Asili Ya Kinyarwanda Na Mimi Ugonjwa Wangu Ni Totoz Wa Kiethiopia, Rwanda Na Somalia. Kimoyo Moyo Nikasema Nimeokota Dodo Kwenye Mpapai. Bhasi Tukapanga Tukutane Sinza Mori Big Bon, Yeye Ni Mkazi Wa Manzese. Nikakaa Pale Elegance Hotel Karibu Na Bodaboda Ili Akishuka Kwa Daladala Nimwambie Ashuke Sheli Ili Nijirizishe Kama Anafaa. Hapo Nimevaa T-shirt Ya Ukali, Jeans Kali Na Safari Boot Za Brown, Kwa Kweli Nilikua Namuonekano Wa Mwanaume Rijali Plus Tabasamu La Ki Gentleman Huku Nikiachia Harufu Ya Old Spice Perfume Kutoka Mcity, Saa Mike Ross , Eye Shades Za Ukweli Na Kofia Ya Nike. Ghafla Ikaja Daladala Pale Mori Huku Nipo Alert Kutazama Utukufu Wa Mungu Wenye Asili Kutoka Kwa Kagame. Kwa Jinsi Alivyo Nieleza Yupo Kama K-lyn. Asalaleeh, Punde Si Muda Simu Aina Nokia Asha Niliyoazima Kwa Roommate Kwa Mauzo Ikaita Nyimbo Ya Sexual Healing 'Marvin Gaye ' Nikaona Taratibu Limama Makamo Na Shangazi Yangu Linajongea Karibu Na Sheli Kutoka Kwenye Daladala. Haki Ya Nani Nilimuangalia Vizuri Ni Ana Kome Kubwa Utosini Kama Yule Aliyedai Binti Wa Lowassa, Miguu Mifupi Kama Pimbi, Wigi Amevaa Kama Yale Ya Nick Minaj Kitu Ambacho Kikamfanya Aonekane Kama Kima, Mwanaume Sikuamini Nikakata Simu Nikapiga Mimi, Hapo Ameshavuka Barabara Kuja Sheli Nikaona Anatoa Simu Kwenye Kipochi Sasa Alivyokuwa Anaongea Mdomo Wake Hakunji Chapati Huyu, Mikononi Anaonekana Ananata Kwa Kumuangalia, Vijimbi Kama Mbwana Samatta . Nashukuru Hakuniona Hapo Hapo Nikamwambia Boda Naomba Nitoe Baru Mpaka Mlimani city. Tukatoka Kwa Mithili Ya Bomu La Hiroshima Na Nagasaki Mpaka Mlimani. Pale Nikaagiza Mango Juice ( Samaki Samaki), Nikawasha Simu Matusi Niliyokutana Nayo Ilibidi Niivunje Laini [emoji23][emoji23][emoji23]. Tangu Siku Hiyo Nimeacha Kiherehere Cha Kujuana Kwa Mtandao.