Mkuu, Japan ilikuwa mbioni ku surrender baada kalemewa na vita, ukweli huo Marekani walikuwa wanaujua sana - sasa kilicho tokea ni nini? Urusi ilitaarifu Marekani kwamba baada ya Urusi kuwashinda Wajapan huko Manchuria ilikuwa na mpango kabambe wa kuivamia na kuikalia Japan, taarifa hizo ziliwashtua sana Wamerikani ukiwekea maanani umahili ulionyeshwa na jeshi la red army dhidi ya Hitler huko Ulaya/Ujerumani - wakati huo hata jengo la Bunge la Ujerumani lilishatekwa na Red Army - nguvu na kasi ya ushindi wa Jeshi la Stalin uliwashtua sana ma Field Marshals na Majenerali wa majeshi ya Wamerikani na Uingereza na Rais Truman wa Marekani pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Winston Churchil.
Baada ya maelezo hayo machache sasa swali ni: Kwa nini Marekani ilidondosha mabom ya Nuclear wakati wakijua wazi kwamba Wajapan walikuwa mbioni ku surrender? Jibu ni rahisi:Cha kwanza kabisa lengo lilikuwa kuwatisha Warusi, pili ni kuwawahi Warusi kabla hawajavamia Japan na kuikalia - na inasemekana baada ya kudondosha mabom mawili huko Japan, Marekani walibakiwa na bom moja tu! Which means kati ya mwaka 1942 mpaka mwaka 1945 Marekani walihunda mabom manne tu - moja lilitumika kwenye majaribio kwenye jangwa la Nevada na mawili yalidodoshwa Japan na moja likabaki kama hakiba na kibaya zaidi mali ghafi ya kuhunda bom yalichimbwa Congo DRC (Belgiani Congo ya wakati huo) lakini Churchil na Truman wakawa wanadanganya Dunia kwa kudai eti madini ya kuhunda bom yanachimbwa Canada. Mara nyingi Amerika ujitetea eti walilazimika kutumia bomb la Nuclear dhidi ya Japan to save lives za manajeshi wao kama Marekani ingehamua kuivamia Japan, hiyo si kweli lengo lilikuwa ni la kisiasa/Geopolitics zaidi kuliko kitu kingine.
Utumiaji wa Nuclear bomb kwa mara ya kwanza Duniani ndiko kulianzisha uadui mkubwa baina ya Urusi na Marekani vile vile na ushindani mkubwa wa kuhunda silaha za maagamizi baina ya Urusi na Marekani ingawa na Uingereza ilikuwa inajitumbukiza humo humo kwa kuwa walikuwa wanashirikiana na Marekani katika tafiti na uhundaji wa silaha za Nuclear, Wafaransa na Wachina walifuata baadae kabisa.