Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hili mada ya swali kuhusu tabia ya kususa, kisiasa, huu mtindo wa kuzira au kususa susa, kususia kila jambo usilokubaliana nalo, sio tabia za kike hizi?, au sio tabia za kitoto?!. Mtu unasusia jambo fulani la kisiasa, ili upate nini?. Kususia jambo lolote la kisiasa bila kupiga hesabu ya what do you want to achieve na kususa huko, sio political suicide?.

The Motive Behind Kususa.
Jee ni nini the motive behind kususa jambo fulani, una susa ili uachieve nini, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata kile walichokusudia?!. Kususa jambo fulani bila malengo, sio tuu ni utoto, bali ni ujinga, kwa sababu ni sawa na kumsusia ngedere shamba la mahindi!, utayavuna mabua!.


My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki uchaguzi sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.

1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, japo sio inclusive lakini ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.

2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.

3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.

4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.

5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.

Conclusion.
The bitter reality kwa wapenda demokrasia wa kweli wa mfumo wa vyama vingi nchini, mimi nikiwemo, tumeshuhudia hali hii ndio uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania ndio umefikia hapa baada ya miaka 26 ya vyama vingi, naweza kusema kuwa this is the peak ya upinzani Tanzania, upinzani Tanzania, ndio imefika mwisho wake sasa!. Sasa tuanze kujiuliza, jee kama hali ni hii sana, je hali itakuwaje kwa uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili mbinu na strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye ushindani usio sawa kupitia sanduku la kura, then, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuna hatari kubwa kwa CCM, kuyarejesha majimbo yote ya uchaguzi yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani, hivyo kuirudisha Tanzania kuwa ni nchi rasmi ya chama kimoja cha siasa, something which is not healthy at all to true modern democracy!.

Hongereni sana CCM kwa ushindi mtamu.
Poleni sana Chadema/Ukawa kwa kupoteza majimbo, wabunge na madiwani.

Tanzania kama taifa, tujipe pole kwa gharama kubwa za chaguzi hizi, ila tuombe sana Mungu alisaidie taifa letu kama gharama hizi za uchaguzi wa kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki, zinajumuisha, machozi, jasho na damu za Watanzania, kwa kugharimiwa na damu na roho za Watanzania, hakuna namna nyingine yoyote ya fidia kwa damu za watu na roho za watu, zaidi vya karma!'

Nawatakia Furahi Day ya Ijumaa Njema.

Wasalaam.

Paskali

Rejea za kuhusu Kususa.
Baada ya uchaguzi wa 2010, Chadema ilisusia matokeo na kujidai kuwa hawamtambui JK, ila bunge tuu lilipoanza, niliibua mjadala huu
Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Matokeo ya Chadema Kususia Hotuba ya JK na Kuapishwa kwa Pinda

Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.

Uchaguzi wa 2015 Ukawa wakadai Lowassa ndie mshindi, hivyo wakajifanya kususa, na kutomtambua Magufuli, mimi niliwapa ushauri ufuatao
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake - JamiiForums

Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!. - JamiiForums

Japo umegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, ulikuwa huru na wa haki!. Hongera CCM, CHADEMA poleni!. Mungu saidia Tz - JamiiForums

Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! - JamiiForums
 
pasco,
so mkuu ulitaka washiriki tu huo uchaguzi hata kama wao wanaona malalamiko yao hayasikilizwi??? haya tufanye kususa hakusaidii kwahio wakienda kwenye uchaguzi ambao wanaona hawajatendewa haki ndo watapata faida??? au kwasababu limefanywa na wapinzan labda??
 
Pasco CCM na wewe wamekununua?
Naamini atajibu aliyeulizwa, mi nataka kuchangia kitu hapa.

Binafsi sifahamu kwa sasa CUF wanasimamia nini. Hiki chama kilikuwa sehemu ya Serikali, mapungufu ya ZEC na ya mahakama kama yapo wamepoteza miaka mitano bila kuyarekebisha.

Sifurahishwi na kunyimwa haki lakini ukifikiria kwa upande wa pili ni kama mwenye hiyo haki haihitaji.

Nafasi waliyoipata CUF Zanzibar kama ingepatikana kwa CHADEMA bara hali ingekuwa tofauti sana. Kuna kitu hakipo sawa
 
pasco,


Jibu la swali lako nafikiri jibu unalo wewe mwenyewe na umeshaliandika kwamba kususa ni tabia ya mtoto hasa pale anapotaka attention sasa Wapinzani au wanaoitwa Wapinzani wasiposusa ina maana hakuna attention na kama hamna attention, basi no money, ila wakati huu wameingia choo cha kike kwa maana Magu hana huwo muda, yeye akili yake yote ipo kwenye kuindustrialize TZ na ,,atakayetukwamisha tutambomoa" kwa maneno yake mwenyewe Magu na hana muda wa kubembelezana mtu anayetafuta attention!
 
Pasco wa JF chukuwa maneno yangu kwa sasa Ukawa (cuf,chadema nk)..ni matawi ya CCM...watu muhimu,wazungumzaji wakuu ni mali ya CCM,hamna kuzira hii ni mipango mizito na sasa wameingia 18,nikikumbuka siku Kinana alivyosema Ukawa imebaki ukiwa baada ya Dr.Slaa na Prof.Lipumba kuondoka...hii ilikuwa siku Dr.Magufuli anaenda kuchukuwa fomu NEC...inahitaji uwe na uwezo mkubwa ili uelewe haya.
 
Pasco CCM na wewe wamekununua?
Mkuu The Big Boss, naomba nikuhakikishie katika maisha yangu yote, japo nina kadi ya chama cha siasa, sijawahi kuutumia uanachama wa chama changu cha siasa kwa kutanguliza mbele maslahi ya chama.

Paskali, anatanguliza mbele maslahi ya taifa, hanunuliki na yeyote kwa lolote kwa sababu hana price tag.

Mimi ni priceless, sio kwa chama changu CCM , wala Chadema, wala Ukawa, wala Lowassa wala Magufuli, au yeyote, hana uwezo wa kuninunua, kwa sababu I'm not for sale, na sina any price tag!.

Naomba uniamini hili ni swali tuu, nimeuliza hawa wanaosusa, wamesusa ili wapate nini?!.

Ni swali tuu.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…