Wanabodi,
Hili ni swali kuhusu tabia, huu mtindo wa kuzira au kususa, sio tabia za kitoto hizi au tabia za kike?!. Jee ni nini the motive behind kususa, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata walichokusudia?!.
Nakumbuka nikiwa mtoto, kususa ni kuonyesha protest ili kupata attention, kisha ubembelezwe!.
Tabia hizi za kitoto, zimekuwa zikiendelezwa na wanawake, ati akigundua amesaidiwa katika kumhudumia mtu wake, na yeye anasusa kutoa zile huduma, eti nenda kapate kule kule!. Au ukirudi umechelewa sana karibu na asubuhi, anasusa kukufungulia, mlango eti kalele huko huko!.
Baadaye ukimbeleza yanakishwa na life return to normal, ambapo baada ya muda, utapatiwa tena huduma nje, na utachelewa tena kurudi, utasusiwa utanuniwa, utasamehewa and life goes on!.
Kufuatia kususa susa kufanywa zaidi na wanawake, jee huku kususa kisiasa sio tabia za kike?!. Tabia za kiume ni kukabili, kupambana, kufight to the end hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu!.
Sasa huku kususa kisiasa, lengo lake ni nini?. Huko kususa, kumewahi kuzaa matunda?!. Kuna msema wa ukisusa wenzio twala, jee kuwasusia ngendere shamba la mahindi, kutasaidia au watu walisusa ili tuu wabembelezwe, na wasipobembelezwa, jee kususa huku kuna faida kwao?!.
Nawatakia Ijumaa Njema.
Pasco