Wanabodi,
Hili mada ya swali kuhusu tabia ya kususa, huu mtindo wa kuzira au kususia jambo, sio tabia za kike hizi au sio tabia za kitoto?!.
The Motive Behind Kususa.
Jee ni nini the motive behind kususa, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata kile walichokusudia?!.
Nakumbuka nikiwa mtoto, kususa ni kuonyesha protest ili kupata attention, kisha ubembelezwe!. The motive behind kususa kwingi ni ama ku create attention au kutaka kukomoa.
Tabia hizi za kususa ni tabia za kitoto, zimekuwa zikiendelezwa sana na wanawake, kwa leongo la kukomoa, mfano mke, au mpenzi wako wa kike, akigundua kuwa amesaidiwa katika kumhudumia mtu wake, na yeye anaamua kususa kutoa zile huduma, kwa hoja kuwa nenda ukapate hizo huduma kule kule!.
Au mume ukirudi home umechelewa sana usiku mkubwa karibu na alfajiri, huku umelewa, mke anasusa kukufungulia, mlango eti rudi ukalele huko huko ulikotoka!.
Baadaye ukimbeleza mke, anakusamehe, unafunguliwa mlango, mke anarudi room na kukupiga biti usimguse!, ukiendelea kubembeleza, mambo yanakishwa na life goes back to normal, hivyo kwa sisi wanaume wa Kiafrika wenye tabia za Kiafrika, hii tabia ya kususiwa na kusamehewa, ni kitu cha kawaida sana, wengi wa wasusaji, huwa wanasusa kutokana na hasira, lakini hasira zikipoa, kususa huwa kunaisha.
Kufuatia Kususa Kufanywa na Wanawake Zaidi, Jee Kususa Kisiasa Ni Tabia Za Kike?.
Kufuatia kususa susa kufanywa zaidi na wanawake, jee huku kususa kisiasa sio tabia za kike?!. Tabia za kiume ni kukabili, kupambana, kufight to the end hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu!.
Kususa Kisiasa, Lengo Lake ni Nini?. Jee Kususa, Huku, Kumewahi Kuzaa Matunda?!.
Kuna msemo wa Kiwahili usemao, "ukisusa wenzio twala", jee kuwasusia ngendere shamba la mahindi, kutasaidia au watu walisusa tuu ili wabembelezwe?, na wasipobembelezwa, jee kususa huku kuna faida kwao?!.
Nawatakia Ijumaa Njema.
Paskali