Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?


Nikupongeze tu umekuwa mstaarabu kwa kuzingatia nchi yetu demokrasia bado tuna safari
 
Wewe ni mchonganishi
 
Kuna baadhi walisoma uzi uhuu kwa " kuruka ruka", sasa hivi wanaona aibu baada ya kuusoma uzi huu kwa " utulivu" . Ulifafanua vizuri mleta mada.
 
Pascal tutake Radhi.
Ulichoandika juu kama subject title ni tusi Kwa Wanawake wote.
Tabia za kike ni zipi! Nani anazitengeneza na kuzihamasisha.
Let's stop creating gender bias on issues.
 
Kugoma maana yake ni kuweka pressure kwa mtu mwingine ili atatue tatizo lako/

Put preesure on someone else/another person so that can solve your problem

Na mtu yeyote anaeweka Pressure ili mtu mwingine afikiri kwa niaba yake Kutatua tatizo

Ana ji disqualifie kua kiongozi au kukaa katika UONGOZI kwasababu

Kiongozi siku zote anatengeneza mindset ya ku solve matatizo ya wengine

na sio kusokuma kwa wengine wamsaidie kutatua TATIZO lake.

Kiongozi haangaliii HAKI YAKE anaangalia FUTURE yake

Wanaogoma wengi wanafunzi/wana siasa they do not think like LEADERS

A leader should suppose to come with HOJA simamia hoja yako

it is not easy BUT who told you Being a LEADER is as easy as you THINK?

Yeyote anae goma huwa AUTOMATICALY namundoa kwenye list ya kumuita KIONGOZI

Fiikiria tena

kabla huja quote ujumbe wangu.
 
Ninavyokufahamu mimi Paschal Mayala wewe ni Intellectual ambae ulitakiwa kuja na ukweli kuisaidia jamii ya Kitanzania, badala yake umekuja na mada ambayo imejaa unafiki wa hali ya juu.Kwa hiyo wewe haupo ndani ya nchi hii kujionea kwa macho yako mambo yanavyoendelea na badala yake unaanza hadi kuwatukana wanawake.
Hizi ni dalili za kutaka uteuzi.Kiukweli umeandika pumba.
 
Inaonesha pasco shuleni kwenye hisabati alikuwa very low
Duh...!, laiti ungalijua.
Sijitapi wala sijidai kuhusu numbers ila amini usiamini nikiwa darasa la 7, kwenye school mock exam ya maswali 25, niliongoza kwa kupiga 96%, nilikosa moja, kuna hesabu ya eneo la chombo cha chakula cha kuku, darasa zima walipatia, mimi tuu peke yangu ndio nikakosa.

Baada ya kugaiwa mitihani nikafanya tena likaja jibu lile lile, sikukubali nikamuomba Mwalimu tufanye ubaoni. Nikaitwa nikashusha likaja jibu lile lile langu, akaitwa mwanafunzi mwingine akafanya, jibu likaja lile la waliopatia, mwalimu akauliza darasa, nani kapata, darasa zima wakaonyesha ni yule mwenzangu, wote wakasema nimekosea na nikazomewa.

Kiukweli kwa ubishi mimi mbishi, sikukubali nikaorodhesha kila kipande na kuonyesha jumla ya eneo lake, niko right na wale wengine wote they got it wrong. Wengine wakawa wana nishangaa kwamba nimeongoza hesabu na bado nalalamika, essence ya kulalamika sio kutafuta 100 bali kutendewa haki.

Ndipo mwalimu akakubali hilo swali lifanywe upya ubaoni, likaja jibu langu, mwalimu akashangaa na kujiuliza How could it be, maana jibu la kwenye marking scheme ni jibu lile la wote.

Swali likaja kwa nini darasa zima wamepatia na Mimi Ndio nimekosea, kumbe kuna wenzetu wana Kiongozi cha Mwalimu, walicopy jibu kule kumbe kwenye Kiongozi cha Mwalimu hilo Swali limekosewa!. From then, nilijulikana ni kipanga wao wa hesabu.

Au nikuwekee matokeo yangu ya O level ushuhudie mwenyewe kwa macho misonge iliyonipeleka Ilboru?.
P
 
Pascal tutake Radhi.
Ulichoandika juu kama subject title ni tusi Kwa Wanawake wote.
Tabia za kike ni zipi! Nani anazitengeneza na kuzihamasisha.
Let's stop creating gender bias on issues.
Ma Kagemuro, soma uzi wote neno kwa neno huku ukiweka kituo panapohusika...!!! Pascal siyo wa hivyo umdhanivyo.
 
Mayalla,kwa heshima yako,nomb ubandike update mpya ya hii makala yako.kwa hali ilivyo sasa,nadhani kuna vitu utakua umeviona!!
 
JK aliruhusu zile operesheni sangara na nyinginezo nyingi zisizo na mtazamo wa kimaendeleo kwa wananchi.

Watu washinde juani wakisikiliza hotuba wakati ardhi yao ni fursa tosha ya kukua kwao kiuchumi.
 
ni katika tanzania pekee wau waliosoma wanakuwa wapumbavu kwa kutaka vyeo.
 
JK aliruhusu zile operesheni sangara na nyinginezo nyingi zisizo na mtazamo wa kimaendeleo kwa wananchi.
Watu washinde juani wakisikiliza hotuba wakati ardhi yao ni fursa tosha ya kukua kwao kiuchumi.
Siku hizi hizo hotuba za marudiomarudio kila siku yaleyale watu wanashinda kwenye kumbi zenye A/C! Ukipenda sana kitu unakuwa mtumwa na kupoteza akili.
 
Ma Kagemuro, soma uzi wote neno kwa neno huku ukiweka kituo panapohusika...!!! Pascal siyo wa hivyo umdhanivyo.
Neno moja linaweza kusambalatisha sifa zako zote ulizozijenga kwa miaka mingi, ninakumbuka ziara ya kikundi cha muziki The Beatles enzi hizo, walikwenda Maerekani na kupokelewa na maelfu ya watu uwanja wa ndege. Walipoteremka kwenye ndege na kuhojiwa na waandishi wa habari kwa mbwembwe za umaarufu wao na idadi ya wapenzi waliokuwepo hapo wakaropoka We are popular than Jesus Christ! Ziara yao iliishia hapohapo watu walifyatuka na kuchanachana mabango na kuvunja rekodi za santuri walizokuwa nazo na ukawa ndiyo mwisho wa kikundi hicho. Watanzania tumezoea tunapomdharau mwanaume humfananisha na akili za kike na kitoto; Muungwana akikosea huomba radhi haraka.
 
Ha ha haa ! They went too far..! Labda kwa kizazi cha sasa wansingesusiwa hao Beattle na kauli yao hiyo!!
===
Mkuu uko sahihi sana, kama ni 'kivaa viatu vyako katika hili'. Kuna wakati nilipata shida kidogo kumuelewa Pasco wa JF na hii ilitokana na kusoma posts zake kwa 'rasharasha'...nilipoona kwa nini mambo yanayonitatiza kwenye posts za Pasco na baadaye Paskalli yako 'consistent' ...nikaamua kusoma posts zake kwa 'masika', nikawa nasoma na kuhusanisha na masuala mengine ya wakati huo, yaliyopita, na yanayotarajiwa katika muktadha moja na mwingine na mwingine. Hii ilinisaidia 'kumuelewa' Pasco. Ni kwenda naye mdogo mdogo kirasharasha, kivuli, mpaka kimasika..!! Anaelewaka tu huyu, ndugu.
---
Nimeeleza yote hayo, si kwamba na mtetea Pasco kwa kila jambo, la hasha!!! Kama kuna sehemu amekwaza wanaJF ama walimwengu kwa ujumla hana budi kuomba msamaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…