Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Sasa sheria ikisema kuwa tume ni huru basi kiuhalisia ni huru? Really?
 
Paskali wewe zoba kweli, si ulisema magufuli ndio rais na hakuna mwingine angeweza kutokea kuja kuongoza nchi hii, ukiamini ungepata uteuzi
 
Kwa mujibu wa wezi wa Uchaguzi ndio nini hapo mbele...??
 
1. Kwa upande wangu, kususa au kususia kitu au jambo fulani la kisiasa au lisilo la kisiasa si tabia ya kike au kitoto kwa sababu jambo lolote linalofanywa kwa kuchagua ni uhuru wa mtu kuchagua kushiriki au kutoshiriki jambo fulani na ni haki yake pia.
2. Nieleze jambo ambalo nilishiriki kususa (ingawa si la kisiasa) na kufanya hivyo haikuwa tabia ya kike au kitoto.
3. Nilitaka kusafiri kwenda mahali fulani. Nilipofika stendi ya magari nikakuta gari linaloenda huko na kuingia ndani. Watu wengine pia waliingia pia viti vikajaa na wengine wakasimama.
4. Tukamwambia dereva aondeshe gari maana tumeshachelewa tunakoenda kwa sababu ya kusubiri kwa muda mrefu na gari limeshajaa. Yeye na konda wake wakatujibu kuwa tusiwaingilie kwenye biashara yao na wataondoa gari wakipenda wao na si kuambiwa na abiria.
5. Mbele yetu kulikuwa na gari linakuja na baadhi yetu tulianza kushuka mmoja mmoja na wote wakashuka, ingawa konda alijaribu kufunga mlango, lakini tulimziri nguvu na kuhamia kwenye gari lile lingine.
6. Wasafiri walikuwa wa kusubiri muda mrefu na gari lile la kwanza lilikuwa limeshasubiri muda mrefu.
7. Uamuzi tulioufanya kusema ukweli ni kwamba "tulisusa" kusafiri kwenye gari ambalo dereva na konda wake wanaamua wanavyotaka na si kuangalia upande wa abiria wanataka nini na tulichokifanya haikuwa tabia ya kike au kitoto. In fact, uamuzi wetu ulikuwa ni uhuru wetu na haki yetu ya kuchagua gari tunalotaka tusafiri nalo na si kwa matakwa ya dereva au konda.
8. Hata katika masuala ya siasa sioni sababu ya kushiriki jambo ambalo mhusika anaona hana masilahi nalo na ambapo ushiriki wake utakuwa na tafsiri ya kukubaliana nalo na kuliendeleza kitu ambacho ni 'contradiction'. Mfano, kama kuna vipengele kwenye sheria ambavyo mbunge anaona havifai kupitishwa kama vilivyo bila kuvifanyia marekebisho, nitamshangaa mbunge ambaye atashiriki kuipitisha hiyo sheria ikiwa na hivyo vipengele ambavyo yeye mwenyewe anaona havifai kupitishwa bila kuvifanyia marekebisho na kuna njia mbalimbali za kufanya hivyo, kususa kukiwa ni njia mojawapo. Njia nyingine ni kubaki ndani ya bunge na kupiga kura ya hapana au kutopiga kura. Haifai kuwahukumu, kuwalaani na kuwaona kama wana tabia ya kike au kitoto wanaotetea masilahi yao ya kisiasa kwa kutumia uhuru wao wa kuamua kushiriki kupitisha hoja fulani kama uamuzi wao hakuvunji Katiba au sheria yoyote ya nchi au hata haukiuki dhamiri yao.
9. Na kwa vile uamuzi wa bunge unafuata wingi wa wabunge (kura) kupitisha jambo fulani, hivyo ni uhuru na haki ya kila mbunge kuamua asuse, akubaline na wabunge wengi, asipige kura nk kwa sababu hoja inayopitishwa na wabunge wengi ndiyo huwa uamuzi wa bunge na hakuna tena haja ya kutafuta nani aliunga mkono au nani hakuunga mkono au nani alisusa.
10. Kutaka kuona ukweli katika hili angalia sheria zinazopitishwa bungeni - sheria ikishapitishwa na majority na ikisaniwa na Rais ina'bind' kwa kila mtu, wakiwemo wabunge walioipitisha na waliosusa.
11. Kwa hiyo, mjadala ambao unafanya baadhi ya wabunge kususa (kusimamia hoja inayokataliwa na wengine) ni haki yao kuunga mkono hoja, kutounga mkono au kususa. Hiyo ndiyo demokrasia yenyewe.
 
Hili tumewaambia sana humu, they never learn!. CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena! na kuhusu hii tabia yao ya kususa susa, pia tuliisha wapaka humu Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?
P
 
Japo naunga mkono hoja, ya "ukisusa sie twala...," na siungi mkono hii tabia ya kususa susa.... Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto? na hapa Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! na Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA is almost dead, due to deadly mistakes! This is your only survival -- do or die. Msirudie kosa

Lakini kama wanasusa for genuine reasons za kutotendewa haki, kama tulivyo shauri hapa Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Najua by now wasoma trends wanajua the consequences za kutotenda haki kwenye uchaguzi, sisi washauri huru tuliisha shauri kabla Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! hivyo Shaka asijitape wakisusa kwa kutetendewa haki sisi twala, badala ya kula wakajikuta wao ndio wanaliwa vichwa!.

Karma haina mswalie Mtume, walishindwa kumlinda Blaza, karma ikafanya yake!, ili kumlinda Maza na karmic consequences, sisi tunao ijua karma, lazima tumsaidie Maza kwa kumweleza ukweli ili aepuke the consequences na yeye asije... hivyo kwa kuanzia tumemshauri Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
 
Kwa hili la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kuruhusiwa, ni uthibitisho wa matokeo mazuri ya majadiliano, mazungumzo na maridhiano at the same time kuthibitisha kususa bila malengo, hakuna faida yoyote kwa msusaji.
Kususa sio dili, dili ni kukaa mezani kuzungumza
P
 
Jana Rais Samia aliporuhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, pia alizungumzia kurekebisha sheria na mwisho kuutanzua mchakato wa katiba mpya.

Hivyo haya ni mambo ya kuyarekebisha
Maadam Mama kaanza, Mama amalize.
P
 
Asante sana kwa taarifa hii, ushauri wangu ni atangaze chochote na alalakike vyovyote kuhusu hizi figisu figisu za uchaguzi wa serikali za mitaa, ila hala hala ,Chadema wasifanye kosa 2019 kususia uchaguzi wa serikali za mitaa,hivyo uchaguzi wa 2020 waliambulia jimbo moja tuu la ngama,wakasusia kuutambua uchaguzi,wakauita ni uchafuzi, baada ya maridhiano wakautambua na kuyatambua matokeo。

Kufanya kosa sii kosa,kosa kurudia kosa, Chadema wasirudie makosa,wasijitoe kwa kususia uchaguzi wa seikali za mitaa!。
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…