Wanabodi,
My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki uchaguzi sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.
1. Tume yetu ya NEC, japo sio inclusive lakini ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.
2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.
3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.
4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.
5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.