Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Kwaio unataka kusema tume ya uchaguzi ni huru lakini hapo hapo unasema kuna changamoto za hapa na pale ambazo kimsingi zinaleta athari juu ya matokeo ya uchaguzi i.e. mshindi ni yule atakae tangazwa na tume, pia matokeo ya uraisi hayatahojiwa sehemu yeyote ile, tatu mawakala wa upinzani kuzuiwa nje daah kweli paskali amekua kilaza
 
Miongoni mwa vitu vinavyokwamisha taifa letu ni pamoja na uwezo mdogo wa wananchi wetu kufanya uchambuzi yakinifu ndio maana tunanunua ndege ya starehe ikituletea hasara na kujenga SGR ya kuzalisha faida miaka 20 ijayo, badala ya kuwekeza kwenye kilimo, huku tukiagiza mchele, sukari na mafuta ya kula badala ya kuzalisha!.

Vivyo hivyo unaulizwa swali, badala ya kujibu, unatoa tafsiri ya jina!. Mada kwenye bandiko hili ni kususa, kuzira na kugoma, jadili mada, usijadili jina la mtoa mada au hali yake kama ana njaa au ameshiba!. Jadili hoja iliyopo mezani. Ukiona jina la mtu nalo ni mada ya kujadili, lifungulie thread, tutachangia.

P
 
Hata kama Haita saidia kutokana na ukandamizaji unaondelea dhidi ya viongozi na hata kwa wanachama wa vyama vya upinzani, lakini jambo LA muhimu ni kufikisha ujumbe kwa wananchi na hata jumuia za kimataifa wajue ni nini kinacho endelea Tz.
 
Mayala tatizo la tume si mkurugenzi bali ni wanaccm wanaosimamia uchaguzi kwani hata maelekezo ya kumtangaza mshindi walipewa wanaosimamia na kutangaza matokeo. Gari huendeshwa na injini (mkurugenzi) lakini hakuna hata siku moja imedhutumiwa kusababisha ajari.
 
nimesita kusoma hili bandiko kwa sababu kichwa cha habari kinadharau wanawake.
Mkuu Ng'wana, kwanza pole!, kusita kusoma kitu pia ni kususa, au kuzira!, na mwisho, haya maneno uliyaona kwenye bandiko hili
"
Kuna Tabia za Kike na Tabia za Kiume
Kwa hapa naomba kwanza kuomba radhi wanawake wote, ni mama zetu, bibi zetu, shangazi zetu, shemeji zetu, wake zetu, wachumba wetu, wapenzi wetu na binti zetu, samahanini sana, ukizaliwa mwanamke uanamke wako sio tuu ni yale maumbile ya kike, bali hormones, tabia, mwenendo na thinking. Tofauti kubwa ya mwanamke na mwanaume zaidi ya sex organs ni emotions and reactions katika situations mbalimbali, ndio maana wewe mwanaume ukifiwa hata na baba yako mzazi, unapigiwa simu unaelezwa, na mwanamke, unauliza kwanza yuko wapi, kama yuko sokoni, utasubiri arudi nyumbani. Baadhi ya tabia kama kulia kwa sauti na kujigalagaza, kuwa na tabia za umbeya, uoga, etc, kunaelezwa ni tabia za kike, hata mtoto wa kiume akililia lia, anaambia usililie lie kama mwanamke. Baadhi ya tabia za kulia lia katika siasa, ni tabia za kike, wanaume wao wamefundishwa kupambana na sio kulia lia!"

Yanamaanisha nini?.
P.
 
Mayala ingependeza zaidi éndapo ungeishia tu kuomba radhi... Maelezo mengine bado yanaleta taharuki kwa wasomaji...
 
Umejitahidi sana kufikiri positively, lakini umesahau njia mojawapo ambayo kwa sasa Mbowe amezungumza kuwa ndiyo ufumbuzi wa madhira haya,njia yenyewe ni "Wanasheria wa chama wanaendelea na taratibu za kesi ktk mahakama" Na taratibu nyingine mbalimbali.Najuwa utaniuliza mahakama gani?Jibu ni kwamba mahakama zina ngazi mbalimbali ndani ya nchi hadi kimataifa.
 
I due respect your foolish advertisements,let your foolishness prevails out of my content!!
I can hardly see a sane, wise and prudent person debating in derogative terms.
Seems like you needed those rude words for your low self esteem therapy, and I'm very happy to have helped a sick person.

Keep using those provocative and low life phrases against me cause they don't hurt my ego, albeit they make you sound more or less of unintelligent person.
 
binafsi nilikuwa nawadharau sana wanaosusa kupiga kura. Mpaka sasa mimi pia nimeshaungana nao, wewe kashiriki tu na endelea kuwashawishi wapinzani wabebe maji kwenye tenga huku ukiwasifia wana busara.
 
Paskali umeupandisha uzi huu.
Kwa nini watu wasuse?
Hoja walizotoa katika kususa nazo umziangalia?
Kwa nini usiangalie scenario nzima unakimbilia katika matokeo?
haya maswali hayajibu anazuga na like tu kwasababu nafsi yake ipo wazi alichokiandika hakipo sawa, yaani anapeleka mashambulizi kwa mjeruhiwa ili afaidi matunda na mtesi wa majeruhi! Kwamba yeye ni priceless.... hii kauli dizaini kama waitara aliitoa kipindi fulani mbele ya chakubanga......
 
usiwafananishe wanawake zako na wake zetu, tena; usimfananishe mwanangu na mwanao
 
usiwafananishe wanawake zako na wake zetu, tena; usimfananishe mwanangu na mwanao
Tofauti ya wanawake zangu na wake zako ni nini?, na tofauti ya mwanao na mwanangu ni nini hadi wasifanane?.
P
 
Mayala ingependeza zaidi éndapo ungeishia tu kuomba radhi... Maelezo mengine bado yanaleta taharuki kwa wasomaji...
Ndio maana nimemwambia asifananishe wanawake zake na wake zetu. Anaomba radhi kisha anadhihaki wanawake! Bogus
 
I've just seen your hocused technical terms!!!
 
Usemayo ni mazuri kama ni kweli. Tatizo ni makala yako ya leo. Hailingani na hadhi yako. Chunguza wote walioishabikia ni akina nani. I thought you won't even dream of being counted among them. Save only for a terrible nightmare! Utakuwa unafahamu hunger strikes. Hakuna utoto hapa. Hakuna udemu kabisa. Kwa ambaye katiba sio kipaumbele, demokrasi si lolote, hayo ni bure. Anaona unachelewa, ungekufa tu. Katika democracy, kususa ni mojawapo ya tools. I dare say, a strong tool kama maandamano. Parties take seats on the negotiating table. Haya yahusu waelewa na waungwana tu. Wanaojulikana sana kama wasiojulikana hawamo. Mchezo gani? Timu inaingia na kamisaa, washika vibendera na refa wao. Inaita timu pinzani wacheze. Yataka moyo wa chuma!
 
binafsi nilikuwa nawadharau sana wanaosusa kupiga kura. Mpaka sasa mimi pia nimeshaungana nao, wewe kashiriki tu na endelea kuwashawishi wapinzani wabebe maji kwenye tenga huku ukiwasifia wana busara.
Mkuu Amri Kuu ni Upendo, kama kweli Amri Kuu ni Upendo, then, hata adui mpende, usimtendee kitu usichopenda kutendewa, kwa vile serikali zote za mataifa huwekwa na Mungu, hivyo hata serikali ikitutenda vibaya kupitia Tume yake ya Uchaguzi, bado tunapaswa kuipenda tuu hivyo hivyo na kushiriki igizo la uchaguzi kwa upendo na sio kususa, kuzira au kugomea, maana Mungu akiamua, anaweza kufanya muujiza kama wa Kenya kwa chama cha KANU, Malawi kwa chama cha MPC na Zambia kwa chama cha UNIP.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…