Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Wanabodi,

Hili mada ya swali kuhusu tabia ya kususa, kisiasa, huu mtindo wa kuzira au kususa susa, kususia kila jambo usilokubaliana nalo, sio tabia za kike hizi?, au sio tabia za kitoto?!. Mtu unasusia jambo fulani la kisiasa, ili upate nini?. Kususia jambo lolote la kisiasa bila kupiga hesabu ya what do you want to achieve na kususa huko, sio political suicide?.

The Motive Behind Kususa.
Jee ni nini the motive behind kususa jambo fulani, una susa ili uachieve nini, na baada ya kususa, jee hao wasusaji huwa wanakipata kile walichokusudia?!. Kususa jambo fulani bila malengo, sio tuu ni utoto, bali ni ujinga, kwa sababu ni sawa na kumsusia ngedere shamba la mahindi!, utayavuna mabua!.

My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki uchaguzi sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.

1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, japo sio inclusive lakini ni Tume Huru, licha ya kuteuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama kimojawapo, kwa uhuru ule ule wa Mahakama zetu ambazo majaji huteuliwa na rais huyo huyo ambaye pia humteua Mtendaji Mkuu wa Bunge letu. Kama Bunge limeweza kuwa huru kwa mfumo huu, na Mahakama ni huru, hata Tume pia ni huru, ila ionekane kuwa huru, something more needs to be done kwenye Tume Hii.
2. Sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kutoa ushindani wa haki. Tusiilaumu Tume kwa chochote kinachotokea kwa sababu Tume inatekeleza sheria zilizopo, kama ni sheria kandamizi, ni kosa la sheria na aliyezitunga na sio kosa la mtekelezaji.
3. The political game playing field is not level, we need to create a level playing field ili kupata ushindani wa haki. Hili nalo ni tatizo la kikanuni, mfano uchaguzi wa 2020, kuna mgombea mmoja anaingia kwenye kinyanganyiro na vingora, msafara, media, na wasaidizi kibao, huku budget yake is fully footed by state, ashindane na makapuku!, unategemea nini?. Tangu tumeanza uchaguzi wa vyama vingi, kuna chama dola kinashindana na vyama makapuku!.
4. Now it's high time vyama vya siasa, vianze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi mbalimbali, kwa kukubali kushiriki uchaguzi katika mazingira haya, na tukishindwa kihalali kwenye sanduku la kura, katika uchaguzi huru na wa haki, tukubali matokeo, na sio kutafuta visingizio.
5. Lazima tufike mahali, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya kasoro za hapa na pale, ambazo hazitaathiri, matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, tujifunze kukubali matokeo na kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani. Kisha turudi nyuma kujitathmini where did we go wrong. Tulipaswa kufanya nini ili kupata ushindi katika mazingira kama haya.
Conclusion.
The bitter reality kwa wapenda demokrasia wa kweli wa mfumo wa vyama vingi nchini, mimi nikiwemo, tumeshuhudia hali hii ndio uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania ndio umefikia hapa baada ya miaka 26 ya vyama vingi, naweza kusema kuwa this is the peak ya upinzani Tanzania, upinzani Tanzania, ndio imefika mwisho wake sasa!. Sasa tuanze kujiuliza, jee kama hali ni hii sana, je hali itakuwaje kwa uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili mbinu na strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye ushindani usio sawa kupitia sanduku la kura, then, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuna hatari kubwa kwa CCM, kuyarejesha majimbo yote ya uchaguzi yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani, hivyo kuirudisha Tanzania kuwa ni nchi rasmi ya chama kimoja cha siasa, something which is not healthy at all to true modern democracy!.

Hongereni sana CCM kwa ushindi mtamu.
Poleni sana Chadema/Ukawa kwa kupoteza majimbo, wabunge na madiwani.

Tanzania kama taifa, tujipe pole kwa gharama kubwa za chaguzi hizi, ila tuombe sana Mungu alisaidie taifa letu kama gharama hizi za uchaguzi wa kinachoitwa demokrasia ya uchaguzi huru na wa haki, zinajumuisha, machozi, jasho na damu za Watanzania, kwa kugharimiwa na damu na roho za Watanzania, hakuna namna nyingine yoyote ya fidia kwa damu za watu na roho za watu, zaidi vya karma!'

Nawatakia Furahi Day ya Ijumaa Njema.

Wasalaam.

Paskali

Rejea za kuhusu Kususa.
Baada ya uchaguzi wa 2010, Chadema ilisusia matokeo na kujidai kuwa hawamtambui JK, ila bunge tuu lilipoanza, niliibua mjadala huu
Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Matokeo ya Chadema Kususia Hotuba ya JK na Kuapishwa kwa Pinda

Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.

Uchaguzi wa 2015 Ukawa wakadai Lowassa ndie mshindi, hivyo wakajifanya kususa, na kutomtambua Magufuli, mimi niliwapa ushauri ufuatao
Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake - JamiiForums

Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!. - JamiiForums

Japo umegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, ulikuwa huru na wa haki!. Hongera CCM, CHADEMA poleni!. Mungu saidia Tz - JamiiForums

Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! - JamiiForums
Tabia za kike? Mkuu ni jana tu wenyewe walikuwa na maadhimisho yao, na moja ya agenda kuu nikutaka usawa. Leo umeweka kichwa cha habari cha aina hii, wakikusikia hawato kuacha.
 
Tabia za kike? Mkuu ni jana tu wenyewe walikuwa na maadhimisho yao, na moja ya agenda kuu nikutaka usawa. Leo umeweka kichwa cha habari cha aina hii, wakikusikia hawato kuacha.
Siku zote ukweli usemwe.
P
 
Ili kuweka kumbukumbu zetu sawa, ni lini hasa ulijiunga ccm? Maana ili ugombee ubunge, kama ulivyojaribu kufanya mwaka huu, sharti uwe mwanachama hai. Na je, hatimaye ulipata bei (price tag)? Narejea yaliyotokea baada ya ule mkutano na waandishi wa habari wa Rais Maguful, ambapo uliuliza maswali ya msingi
Mkuu Mindi , makaburi mengine hatari kuyafukua!. Kwa heshima yangu, niko chini ya miguu yako, naomba hili bandiko lako ulifute!, ni ombi tuu, sio amri!, ukiisha lifuta, nitakuambia kitu!, please!.
P
 
Ni katika kujikumbusha tuu, na kukumbushana tuu kuhusu hii tabia ya kususa, Chadema hawakuanza leo.

kuna vitu unaweza kususa, na kuna vitu huwezi kususa!, hata majumbani mwetu, mara ngapi tunabaniwa?, watabana.. mwisho wataachia!.

Hawa watu wanajifanyaga kususa, eti hawakubali matokeo, na hawamtambui rais!. Rais akiisha apishwa, yeye ndio rais, umtambue usimtambue ndio rais wako!. Kuna vitu unaweza kususa, kama kula, lakini kuna vitu huwezi kususa kwasababu vipo in existence, kama kususa kuvuta pumzi, au kususa kushusha, ikitokea need ya kushusha, lazima ushushe, huwezi kususa, na hata ukisusa, bado mzigo utashuka!.

Huwezi kususa kumtambua rais!.

P
 
Mwaka huu nenda kapige kura , hakuna kura ya mtu itakayoibiwa. ..........Mh. Tundu Lissu.
Baada ya uchaguzi:
Nimeibiwa kura zoooote...hahhhahaha
Hii tabia ya kutokukubali matokeo inabidi tuitafitie dawa
Naunga mkono hoja, tena kuna akina sisi, tuliwashauri vizuri kabisa kabla
p
 
Huu ndio ukweli ninaowaeleza msije mkajichanganya mkagomea bunge la awamu hii.

Nu kweli uchaguzi hakua wa haki lakini hampaswi kususia bunge.

Kwasababu hata mkisusa hamta gain chochote mnatakiwa kufahamu watanzania bado hawajaamka na asilimia kubwa elimu ni tatizo so hata mkizira wao hawana mda na nyie.

Eaacheni vichwa kama halima mdee, suzan kiwanga ester bulaya nk

Waacheni wakapambane hata kama watakua peke yao, shujaa hakimbii vita

Mnafikiri mkisusia bunge baada ya hapo itasaidia nini?

Kazi kwenu sawà
Naunga mkono hoja, Chadema, hapa walipo tayari they are half dead, wakisusa kutoa ushirikiano kwa Mbunge wao wa ngama, na kususia kuteua wabunge wa viti maalum, then kwa Chadema, that will be the final fenale, Chadema itakuwa finito, totally kwishney, their only place will be 6ft under!.


Watu tunakesha humu kuwaombea uteuzi, kumbe wenzetu wanapanga kususa!.

Hawajajifunza kilichowapata CUF na sasa ACT kususa ile 2016?.

Kama ni kususa, suseni ila msije kujuta...

P
 
My Take. (Maoni Yangu).
Kususia kushiriki uchaguzi sio suluhisho, huku ni kujiua kabisa kisiasa, dawa ni kujenga hoja madhubuti na kukaa mezani kuzungumza, vingine tuitumie mahakama yetu kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.
Kazi ya kususa inaendelea...
P
 
Kazi ya kususa inaendelea...
P
Mahakama gani unaongelea Paskali ???, hizi za ccm zilizo chini ya mkono wa serikali dhalimu ambayo watendaji wake (Takukuru) wamekiri kwamba kulikuwa na kesi 147 waliwabambika watu !!, ambazo sasa wametangaza kuzifuta, za polisi ndio hazihesabiki
 
Yan unaweza kusema tume ya uchaguzi Tanzania ni tume huru? You are insulting your own intel
Kwa mujibu wa sheria iliyounda Tume ya Uchaguzi NEC, ni Tume huru, iko independent, tatizo ni sio shirikishi yaani NEC is independent, but not inclusive, kinachotakiwa ni kuifanya tuu kuwa Inclusive, na hili liko ndani ya uwezo wa Mama Samia!.

Paskali
 
Back
Top Bottom