Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ninaamini CCM wanauelewa msemo kwamba kesi ya kima huwezi kupeleka kwa nyani. Hakutakuwa na haki katika hukumu.
Vivyohivyo, Watanzania wote wanaelewa kwamba tuhuma za CCM dhidi ya Membe, Makamba na Kinana kwa namna kubwa zilikuwa zinamhusu Magufuli.
Membe siku zote ameonwa kuwa mpinzani na tishio kwa uraisi wa Magufuli. Kinana na Makamba walisemwa kuwa waliongea mambo ambayo yalikuwa dhidi ya Magufuli.
Sasa kitu cha ajabu sana kilichotokea, eti kamati ya CCM iliyotoa adhabu dhidi ya Membe, Makamba na Kinana mwenyekiti wake akawa huyo huyo Magufuli!
Hivi tuseme kwamba katika CCM yote hakuwapo mtu mwenye busara kuona hili halikuwa sahihi? Sio suala la kesi ya kima kuipeleka kwa nyani?
Labda hilo mliliona, lakini ukweli ni kwamba mnamwogopa sana Magufuli na kuhofia kupoteza nafasi zenu kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuthubutu kupendekeza au kutoa wazo kwamba isingekuwa vema Magufuli kuwa mwenyekiti wa kamati itakayowaadhibu Membe, Makamba na Kinana kwa kuwa kesi dhidi yao zilimhusu.
Kwanza hebu tutafakari na kwenda mbali kidogo. Huu uamuzi wa kamati ya CCM iliyotoa adhabu ilikuwa ni uamzi wa kamati au uamuzi wa Magufuli? Katika namna ya staili ya utawala wa Magufuli na uoga kwa Magufuli wa viongozi walio chini yake, hivi kuna mtu anategemea mwanachama yeyote wa kamati hii angeweza kutoa mawazo mbadala ikiwa Magufuli alikuja kwenye kamati hii akiwa tayari ameamua uamuzi gani utatolewa?
Na zaidi, ni wazi Magufuli amekuwa akifanya kila jitihada ya kuwazimisha wanachama wote wa CCM waliojitokeza kugombea uraisi dhidi yake mwaka 2015, kuanzia kina Mwigulu, Mwandosya, January Makamba, Membe nk, pamoja na wale wenye kuonyesha dalili za kuangaza kisiasa zaidi yake kwa sasa.
CCM ngoja tuwaambie ukweli, aliyepewa adhabu hapa wala sio Membe, Makamba na Kinana, bali ni nyie CCM wenyewe! Na hadi sasa mkubali kwamba nyie sio tena CCM inayopaswa kuwa Chama Cha Mapinduzi, bali ni CCM inayopaswa kuwa Chama Cha Magufuli.