Swali kwa CCM: Ikiwa "makosa" ya Membe, Makamba na Kinana yalihumhusu Magufuli, ilikuwa sahihi kwa Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Kamati iliyowaadhibu?

Swali kwa CCM: Ikiwa "makosa" ya Membe, Makamba na Kinana yalihumhusu Magufuli, ilikuwa sahihi kwa Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Kamati iliyowaadhibu?

Kamati ndio iliyowasilisha taarifa na CC ikabariki uamuzi wa kamati maana ndio ilyofanya kazi ya kuwasikiliza na kuja na maamuzi na kazi ya CC nikukubaliana na kamati ambayo ilipewa kazi na CC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CC ya CCM imebariki tuu maamuzi, the kangaroo court was ile Kamati ndio imeamua, CC ikabariki.
P

Good point Pascal, lakini angalia hii extract toka IPPMedia;

1582972113606.png

1582972181692.png
 
Kawaida ni utamaduni au utaratibu
Kikao kilichomfukuza Zitto Chadema Mwenyekiti alikuwa Mbowe ma Katibu alikuwa Dr Slaa ambao wote walikuwa Wagomvi wa Zitto kwa nafasi ya Uenyekiti na ugombea Urais.

Kikao kilichomvua Uanachama wa CUF Prof Lipumba Kiliongozwa na Mtatiro na Seif ambao walikuwa ndio Walalamikaji

Aliekuwa anagawa Fomu za kugombea Urais wa Znz kupitia CUF alikuwa Seif Sharif Hamad ambae pia ndie alikuwa Mgombea wa Milele.

Kikao kilichomfukuzisha Uanachama na hatimae Kufungwa Maisha kwa tuhuma za uongo za Uhaini Marehemu Bibi Titi Mohamed Mlalamikaji alikuwa Nyerere na Mwenyekiti alikuwa Nyerere 1968.

Kwny Siasa hayo ni ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app

B-50
 
Kuna TACO na TAKO .... Lakini zote zinatamkwa tako... Sio mbaya mkiita CCM lakini ikiwa ni CHAMA CHA MAGUFULI itaendelea kubaki tu ni ccm......
Mkuu TACO na TAKO ni lugha mbili tofauti huwezi kulinganishaila hili la CCM Mapinduzi na Magufuli hawawezi kukwepa 🙂
 
Ninaamini CCM wanauelewa msemo kwamba kesi ya kima huwezi kupeleka kwa nyani. Hakutakuwa na haki katika hukumu.

Vivyohivyo, Watanzania wote wanaelewa kwamba tuhuma za CCM dhidi ya Membe, Makamba na Kinana kwa namna kubwa zilikuwa zinamhusu Magufuli.

Membe siku zote ameonwa kuwa mpinzani na tishio kwa uraisi wa Magufuli. Kinana na Makamba walisemwa kuwa waliongea mambo ambayo yalikuwa dhidi ya Magufuli.

Sasa kitu cha ajabu sana kilichotokea, eti kamati ya CCM iliyotoa adhabu dhidi ya Membe, Makamba na Kinana mwenyekiti wake akawa huyo huyo Magufuli!

Hivi tuseme kwamba katika CCM yote hakuwapo mtu mwenye busara kuona hili halikuwa sahihi? Sio suala la kesi ya kima kuipeleka kwa nyani?

Labda hilo mliliona, lakini ukweli ni kwamba mnamwogopa sana Magufuli na kuhofia kupoteza nafasi zenu kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuthubutu kupendekeza au kutoa wazo kwamba isingekuwa vema Magufuli kuwa mwenyekiti wa kamati itakayowaadhibu Membe, Makamba na Kinana kwa kuwa kesi dhidi yao zilimhusu.

Kwanza hebu tutafakari na kwenda mbali kidogo. Huu uamuzi wa kamati ya CCM iliyotoa adhabu ilikuwa ni uamzi wa kamati au uamuzi wa Magufuli? Katika namna ya staili ya utawala wa Magufuli na uoga kwa Magufuli wa viongozi walio chini yake, hivi kuna mtu anategemea mwanachama yeyote wa kamati hii angeweza kutoa mawazo mbadala ikiwa Magufuli alikuja kwenye kamati hii akiwa tayari ameamua uamuzi gani utatolewa?

Na zaidi, ni wazi Magufuli amekuwa akifanya kila jitihada ya kuwazimisha wanachama wote wa CCM waliojitokeza kugombea uraisi dhidi yake mwaka 2015, kuanzia kina Mwigulu, Mwandosya, January Makamba, Membe nk, pamoja na wale wenye kuonyesha dalili za kuangaza kisiasa zaidi yake kwa sasa.

CCM ngoja tuwaambie ukweli, aliyepewa adhabu hapa wala sio Membe, Makamba na Kinana, bali ni nyie CCM wenyewe! Na hadi sasa mkubali kwamba nyie sio tena CCM inayopaswa kuwa Chama Cha Mapinduzi, bali ni CCM inayopaswa kuwa Chama Cha Magufuli!

Chama ni saccos binafsi mwenye saccos yake ndo kaamua iwe hivo
 
Kama ni hivyo basi tuna tatizo kubwa katika siasa za Tanzania. Hata hivyo, matarajio yetu ni kwamba CCM ni chama kilichokomaa kuliko Chadema, CUF nk. Kama vyama vingine vinafanya upuuzi basi CCM ilipaswa kujipambanua kuonyesha wao wana busara zaidi.

Mkeo akitembea nje ya ndoa na Juma, wewe husawazishi kwa kutembea nje ya ndoa na Mwajuma!
Huyo anapotosha; kesi ya Zito ilikua dhidi ya kula njama ya kumpindua mwenyekiti na kufanya hujuma dhidi ya chama.
Kesi ya Membe na wenzake ilikua dhidi ya Mh Magufuli, kwenye yale mazungumzo amna sehemu iliyozungumzwa ccm kama chama. Iwapo yale mazungumzo yangekua na nguvu wangeshtakiwa na serikali au na Magufuli mwenyewe.
Mbona wanachama wengi wa CCM wanatukana na kugombana na watu kila kukicha huku mtaani kwanini hawajastakiwa kwenye chama?
Ni mpuuzi tu ndo anaweza kuamini kua kile kilikua barua ya kuwaita kwa mashtaka yanayousiana na yale mazungumzo.
 
@blome-e kwaiyo ukitaka kila kikao kikao cha halmashaur kuu ya chama ikikaa kumjadili mkosaji katiba ya chama ibadilishwe kama **** kuna mjumbe anamaslah na mtu fulani anaejadiliwa? Ukumbuke katiba ya imetaja kama mwenyekiti
 
@blome-e kwaiyo ukitaka kila kikao kikao cha halmashaur kuu ya chama ikikaa kumjadili mkosaji katiba ya chama ibadilishwe kama **** kuna mjumbe anamaslah na mtu fulani anaejadiliwa? Ukumbuke katiba ya imetaja kama mwenyekiti
Huhitaji kuweka vitu kama hivyo kwenye katiba, hata common sense itatosha. Kwani mwanachama wa hiyo kamati akiwa ndio mtuhumiwa naye atabaki kwenye hichi kikao kama member wa kamati? Kwa hiyo kama kuna kipengele kinasema atapisha basi kinapaswa kutumika hata kwa mwenyekiti kupisha ili kikao kifanyike askiwa hayupo. Haijalishi kama yeyey sio mtuhumiwa bali suala ni kwambaanahusika moja kwa moja katika tuhuma zinazojadiliwa
 
Back
Top Bottom