Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Nimefurahishwa na hatua ya Katibu Mkuu wa CCM kujitokeza na kuweka bayana mtazamo wa chama tawala cha CCM kinachosimamia serikali inayotuhumiwa kufanya madudu.
Ni madudu kuhusu operesheni ya kutekwa, kuteswa na kuteketezwa kwa baadhi ya wakosoaji wa serikali inayofanyika kana kwamba Tanzania ni himaya ya kifalme ambamo uhai na umauti wa raia yeyote huwa ni hiari ya mfalme aliyekalia kiti cha enzi.
Dkt Nchimbi ametoa tamko la CCM akifafanua hatua zinazochukuliwa na chama na serikali kupitia agizo la Rais Samia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Alifafanua kuwa Rais amemwagiza Waziri Mkuu kuunda Kamati ya uchunguzi kuhusu operesheni ya kutekwa, kuteswa na kuteketezwa kwa baadhi ya wakosaji wa serikali.
Hata hivyo, ufafanuzi wa Dkt. Nchimbi unayo mapengo ya taarifa muhimu. Mapengo hayo ni kama ifuatavyo:
- Hakuna Kamati ya Uchunguzi inayoweza kufanya kazi kiholela bila kupewa hadidu za rejea zinazotaja aina na mipaka ya majukumu husika (thematic scope). Je, hadidu za rejea zimekwishaandaliwa na kutolewa kwa Waziri Mkuu, na kama tayari ziko wapi?
- Kazi ya kuchunguza utekwaji, uteswaji na uteketezwaji wa raia unayahusu matukio yaliyofanyika tangu 2016 hadi sasa nchini Tanzania. Je, wigo wa kimajira (temporal scope) wa kazi za Kamati ya Majaliwa ni upi?
- Aidha, kazi ya kuchunguza utekwaji, uteswaji na uteketezwaji wa raia inayohusu matukio yaliyofanyika katika mikoa yote ya Tanzania. Je, wigo wa kijiografia (spatial scope) wa kazi za Kamati ya Majaliwa ni upi?
- Uchunguzi ni mradi, na kila mradi huwa una tarehe ya kuanza na tarehe ya kufungwa. Na kwa kuzingatia taharuki iliyosababishwa na operesheni ya kutekwa, kuteswa na kuteketezwa kwa wakosoaji wa serikali sasa Taifa lina kiu ya kupata majibu ya haraka kutoka kwenye Kamati ya majaliwa. Je, ratiba ya kazi (timetable) za Kamati ya Majaliwa imebainishwa, na kama ndio, ratiba hiyo iko wapi?
- Na kubwa zaidi, operesheni ya kutekwa, kuteswa na kuteketezwa kwa baadhi ya wakosoaji wa serikali inayofanyika kati ya Julai 2023 na sasa inatendeka katika uzio wa kisheria (legal framework) uliozaliwa kutokana na marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023. Mabadiliko haya kama yanavyoonekana kwenye vifungu vya 3, 5(2) na 19(1) yameipa Idara hii mamlaka ambayo hayakuwepo hapo kabla. Ni madaraka ya kukamata watuhumiwa wa makosa ya jinai yasiyohusiana na uhaini wala ugaidi. Jambo hili linaiweka Idara hii juu ya sheria na kuiruhusu kufanya kazi za kipolisi. Je, CCM iko tayari kuchukua hatua za haraka kubatilisha vifungu hivi vilivyo kinyume na Katiba ya nchi?
- "3. 'Security"' ..... means the protection of the United Republic from any acts including acts of terrorism, espionage, sabotage and subversion, whether or not it is directed from or intended to be committed within the United Republic."
- "5(2) Save as otherwise provided in any other written law, it shall not be a function of the Service (a) to enforce measures for security";
- “19(1) No action or other proceedings shall lie or be instituted against the Director General or officer of the Service for or in respect of any act or thing done or omitted to be done in good faith in exercise or purported exercise of his function under this Act.”
Kuhusu vifungu hivi Matakwa ya umma mpana wa Watanzania yako hivi:
- Kuhusu kifungu cha 3, Watanzania makini wanataka maneno "any acts" yaondolewe mara moja maana yanatoa nafasi kwa maafisa usalama kujishughulisha na matukio kama vile tamko kwamba mtu haitaki ccm na serikali yake, kitendo cha mtu kuunguza picha ya rais, kitendo cha mtu kuifungia maandazi picha ya rais, na vitendo vya jinai ambavyo sio ugaidi wala uhaini. It is total chaos! Na Kwa kweli mtu aliyependekeza, kurekebisha, kupitisha, au kuidhinisha mabadiliko katika kifungu hiki ni mtu aliyefanya uamuzi ulio hatari sana kwa usalama, amani na utulivu wa nchi.
- Kuhusu kifungu cha 5(2) Watanzania makini wanataka maneno "any other written law" yaondolewe na kusomeka wazi wazi kama "the Prevention of Terrorism Act" na hivyo kuondoa uwezekano wa maafisa usalama kufanya kazi chini ya sheria baki kama vile sheria ya jeshi la polisi.
- Na kuhusu kifungu cha 19(1) Watanzania makini wanataka misingi ya utawala wa sheria izingatiwe kwa kuhakikisha kuwa kinasomeke hivi: “19(1) No conviction or punishment shall lie against the Director General or officer of the Service, after proceedings have been instituted against him, for or in respect of any act or thing done or omitted to be done in good faith in exercise or purported exercise of his function under this Act, provided that there is sufficient evidence to prove that he acted in good faith.”
Hivyo wakamatwaji hawa wanahifadhiwa Katika karakana za mateso zilizoandaliwa kwa dharula kandoni mwa vituo vya polisi.
Karakana hizi ni vituo vya utekaji na utesaji ambavyo vinafanya kazi nje ya utaratibu wa kawaida wa kipolisi na hivyo kulichafua jeshi la polisi.
Watekwaji wakiwa huko gereji wanatendewa kana kwamba wao ni nguruwe, sokwe au nyani, chini ya Kanuni za TISS ambazo hata Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge haijawahi kuziona.
Ukatili huu unafanyika dhidi ya Waafrika katika nchi yao ambamo Rais wake wa sasa ni Samia Suluhu Hassan mwenye asili ya Kiarabu, na unaleta sura hasi sana.
Ni ukatili wenye kuwaweka Waafrika hawa chini ya utumwa mamboleo, baada ya Waafrika hawa kuwa wamesota chini ya Utumwa wa Kiarabu kwa karne 14 ambapo Waafrika wapatao milioni 15 walitekwa, kuteswa na kutumikishwa na Waarabu.
Safari hii Watanzania hawa wanajikuta wakiwa ni watumwa chini ya serikali yao inayoongozwa na Rais mwenye asili ya Kiarabu, na hivyo kutonesha madonda ya utumwa wa kihistoria.
Soma Pia:
- Dkt Nchimbi: CCM imekasirishwa sana na mauwaji ya Ali Kibao na serikali iharakishe haraka uchunguzi na matukio yakomeshwe
- Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa, umewapa 'Kinga ya Jinai' Maafisa Usalama
- Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya Usimamizi wa Rais watua Bungeni
Kutokana na uchambuzi wa intelijensia za kitaifa na kimataifa, kuhusu ukoloni wa Waafrika chini ya Waarabu ulianza karne ya saba, hiyo ndio picha pana inayoonekana.
Kwa sasa Mradi huu wa Kuasisi Dola Shikizi ya Kiarabu ndani ya Tanzania ikiwa inaitwa "Ngorongoro Arabic Satellite State (NASS)" karibu unakamilika, kama hatua za kimkakati hazitachukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kulinda mipaka ya nchi.
KImsingi Katiba ya Tanzania ambayo ni dola ya kidemokrasi na kijamuhuri haikubaliani na mradi huu wenye kumega ukuu wa nafsi ya kiutu katika ngazi ya Taifa.
Katika mazingira haya, maswali madogo mawili yanaibuka:
- Je, viongozi wa CCM wako tayari kumwagiza Spika Tulia Akson na Waziri wa Sheria kubatilisha mara moja vifungu hivyo vilivyoingizwa kihuni katika Sheri ya Idara ya Usalama wa Taifa?
- Na je, viongozi wa CCM wako tayari kuiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kumtaka Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa awasilishe TISS code of conduct ili Kamati iweze kuzipitia na kutoa mwongozo stahiki?
Sisi watu wa Nyerere tunataka kuishi katika nchi ambako kila mtu anajua kesho kutatokea nini.
Katika macho ya Watu wa Nyerere suala la uhai wa binadamu ni nyeti sana kwa sababu kuu mbili:
- Uhai ndio kikonyo cha haki zote za binadamu
- Hakuna mizania huru inayoweza kutumika kupima thamani ya Uhai wa mtu yeyote, Kiasi kwamba ni sahihi kuhitimisha kuwa, and uhai wa mtu kama Rais Samia ni sawa kabisa na uhai wa kina Soka na kina Saanane.
- The instances of goods and bads at stake in legal, moral and political choices are incommensurable values.
- Human life instances are goods in legal, moral and political choices.
- Thus, human life instances are incommensurable.
- Murderers and cannibals unreasonably treat human life instances as commensurable values.
- Thus, "you shall not kill humans" and " you shall neither eat human flesh nor drink human blood" are negative moral precepts which are moral absolutes.
Source: David Luban (1990), "Incommensurable Values, Rational Choice, and Moral Absolutes," Vol. 38:65-84.
Kwa hiyo basi, MHE. KATIBU Mkuu, leo umeongea kama STATESMAN kwa mara ya kwanza tangu ukalie kiti hicho.
Basi, hebu jitahidi kumalizia kibarua ulichokianzisha kwa kutoa ufafanuzi unaoziba mapengo ya taarifa niliyoyabainisha hapo juu.
Utakuwa umeokoka jahazi kwa faida ya wengi.
Jambo la mwisho kabisa, nakuomba uwakumbushe Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kuzingatia kiapo chao kifuatacho:
"Mimi, XYZ, Naapa/Nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria. Ewe Mwenyezi Mungu Nisaidie." (Chanzo: Marekebisho ya 2023 ya Sheria ya TISS)
Nakutakia utekelezaji mwema wa majukumu yako.