Pre GE2025 Swali kwa Kinana, lini Rais Samia alipigiwa Kura na wajumbe au amerithi kiti hicho cha urais?

Pre GE2025 Swali kwa Kinana, lini Rais Samia alipigiwa Kura na wajumbe au amerithi kiti hicho cha urais?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
NI wazi kwamba Samia Suluhu Hassan alirithi kiti cha urais baada ya Hayati Magufuli kufariki dunia huyu ndiye aliyepitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu na vikao vya chama hadi akawa rais.

Kinana asipotishe umma kwamba desturi ya CCM NI kumwachia rais aliyepo sasa kuendelea na mhula mwingine bila kushindanishwa lini Samiah alipigiwa Kura ya vikao vya CCM na kupitishwa kuwa mgombea wa uraisi hajui kama mama amerithi kupitia kwa mwenzake?

Kinana ujuwe kuwa nchi hii ina watu wenye akili timamu kauli kama hizo ni kauli zinazoleta mtafaruku ndani ya nchi kwani ni vizuri demokrasia ikatawala na watu wachukue form wapate. raisi wanaoona anafaa kuwaongoza hivyo mama ashindanishwe kwani hata akishindanishwa akashinda basi atakuwa ametetea kiti chake na ndiyo maana ya demokrasia.

Hakuna mtu anayesema wala kubisha mama hafai isipokuwa ashindanishwe na wagombea wengine ndani ya CCM hiyo ndoo demokrasia tunayoijuwa.

Kauli hizo tunaomba makamu mwenyekiti wa chama ysiendelee kuzisema kwani zinaibua maswali mengi ndani ya chama na nchi kwa ujumla.

Mama mwenyewe tayari anawasili wake alishawatonya anahitaji kujipumzikia iweje Leo mumlazimishe.
Hadi anakuwa Mwenyekiti hakupigiwa kura?

Hata kwenye Kugombea Urais formality zitafuatwa Kwa kupigwa kura.

Mwisho fomu ya Urais itakuwa Moja,huwezi mpoteza Rais Mwana Mageuzi kama Samia kisa chuki za kipumbavu.
 
Point kubwa hii
Mhe Samia amepigiwa kura mara mbili na wananchi wakiwa pamoja na Mwamba ! [emoji23][emoji120][emoji120]
Alipigiwa kura kwaajili ya kuwa Makamu wa Rais siyo kwaajili ya kuwa Rais. Wewe ukiteuliwa kuwa mkuu wa idara, na mwenzako msaidizi wako, haimaanishi aliyewateueni anamaanisha yule msaidizi wako anafaa kuwa mkuu wa idara. Ameteua ili aweze kukusaidia, na atafanya kazi chini ya maelekezo yako, na endapo kwa sababu yoyote ile kama utaondoka ghafla, yeye atashikilia nafasi yako wakati mtu sahihi kwa nafasi hiyo iliyo wazi akiwa anatafutwa. Japo inawezekana, wakati msaadizi akikaimu nafasi akadhihirisha kuwa ana uwezo, na baadaye akathibitishwa.

Ni wakati wa Rais Samia, baada ya kuwa Rais wa kipindi cha dharula, kama anataka kuwa Rais wa kuchaguliwa, kupitia hatua zote ili awe Rais wa kuchaguliwa. Asiitumie dharula kama ndiyo automatic chance ya kuwa Rais bila ya kushindanishwa.
 
Sasa akifa ndio Makamu anakuwa Rais automatically

Ambaye hajapigiwa kura ni Mpango

Very simple 😂
Hii katiba hii! Katiba ingesema substantive akifa au akishindwa kutekeleza majukumumu yake jwa sababu a,b,c Makamu wake atakaimu kwa kipindi a,b,c then uchaguzi mkuu uitishwe! Lakini hii katiba haiko hivyo Tuombe katiba mpya..
 
Alipigiwa kura kwaajili ya kuwa Makamu wa Rais siyo kwaajili ya kuwa Rais. Wewe ukiteuliwa kuwa mkuu wa idara, na mwenzako msaidizi wako, haimaanishi aliyewateueni anamaanisha yule msaidizi wako anafaa kuwa mkuu wa idara. Ameteua ili aweze kukusaidia, na atafanya kazi chini ya maelekezo yako, na endapo kwa sababu yoyote ile kama utaondoka ghafla, yeye atashikilia nafasi yako wakati mtu sahihi kwa nafasi hiyo iliyo wazi akiwa anatafutwa. Japo inawezekana, wakati msaadizi akikaimu nafasi akadhihirisha kuwa ana uwezo, na baadaye akathibitishwa.

Ni wakati wa Rais Samia, baada ya kuwa Rais wa kipindi cha dharula, kama anataka kuwa Rais wa kuchaguliwa, kupitia hatua zote ili awe Rais wa kuchaguliwa. Asiitumie dharula kama ndiyo automatic chance ya kuwa Rais bila ya kushindanishwa.
Uko sahihi sana mkuu🙏🙏
 
Hii katiba hii! Katiba ingesema substantive akifa au akishindwa kutekeleza majukumumu yake jwa sababu a,b,c Makamu wake atakaimu kwa kipindi a,b,c then uchaguzi mkuu uitishwe! Lakini hii katiba haiko hivyo Tuombe katiba mpya..
SSM ameshindwa kutekeleza majukumu yake sababu hatoshi, Ameshindwa kusimamia uchumi sababu ni mweupe.

Umeme, maji, kuuza misitu, rushwa, bandari, Ngorongoro, nidhamu serikalini, mfumuko wa bei nk ingependeza amwachie Makamu wake hadi uchaguzi mkuu.

Mpango aliusimamia uchumi vizuri alipokuwa waziri wa Fedha.
 
Hii katiba hii! Katiba ingesema substantive akifa au akishindwa kutekeleza majukumumu yake jwa sababu a,b,c Makamu wake atakaimu kwa kipindi a,b,c then uchaguzi mkuu uitishwe! Lakini hii katiba haiko hivyo Tuombe katiba mpya..
Ndio maana tunaitaka hiyo Katiba mpya ije iyaondoe mapungufu yote na sintofahamu zote zinazojitokeza almost kwenye vipengele vingi sana vya Katiba iliyopo !
Hii Katiba iliyopo ilikusudiwa kwa ajili ya utawala wa Chama kimoja cha siasa !
Enzi zetu za Chama kushika Hatamu ! 🙏🙏
 
Back
Top Bottom