Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Naomba kuuliza kwanini nauli za kutoka Dar kwenda mikoa mingine zinatofautiana na zile za kurudi hasa vituo vya njiani kwa mfano, hivi majuzi nilipanda bus moja kutoka Morogoro kwenda Mbeya nikalipa Tshs 45,000, jambo la kushangaza wakati narudi nilipokwenda kukata tiketi kwenye bus lilelile kurudi Morogoro nikaambiwa nauli ni Tshs 58,000 ambayo ni nauli ya Mbeya - Dar, nilipowauliza kwanini wakasema ni mwongozo wa LATRA kuwa nauli za kurudi kutoka mikoani haiangalii vituo vya njiani nauli ni flat rate regardless unashuka wapi