Hapana Mimi Napenda Kuleta Changamoto mkuu Ili Mzielezee..
Sina maana ya Kuwa Outsmart wengine..
Ok safi umeeleza vizuri.. sasa Vipi kuhusu Andiko hili alilosema Yesu..
Kwahyo Ukileta Fitina Kati ya Ndugu Unakuwa Umeleta Ukombozi..?
Unahisi Kwanini aliyefundisha Upendo aje tena Afundishe Fitina kwa Ajili yake ...Yaani Anafurahi endapo Ndugu watafitiniana kwa ajili yake?
Ila biblia Hiyo hiyo inafundisha Upendo na amani na watu wote..
Waebrania 12:14
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"
sasa kama Tunaambiwa Tutafute kuwa na abidii na watu wote halafu tena tunaambiwa Tifanye fitina Baina yetu na Upanga Huoni Ni changamoto..
Au Umesahau Kuwa Zaburi Inatuonyesha Uzuri wa Ndugu kuea Pamoja?
Zaburi 133:1
" Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja."
Sasa Umemsikia Na Yesu alivyosema?
Mathayo 10:34-35..
"34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;"
Sasa Unaona Inavyotuchanganya nikiwemo Mimi?
yaani Zaburi inatuonyesha Uzuri wa Ndugu kuwa Pamoja kwa Upendo ila Yesu anatuambia Alikuwa Kufitinisha Baina ya Ndugu..
Na Unazungumziaje Kauli hii Ya Yesu Boss wangu..
Luka 19:26-27..
26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang'anywa hata alicho nacho.
27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.