Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Nimeona niulize haya sababu kinachoendelea inabidi ukiangalie kwa macho yako na sio kusikiliza kinachosemwa.... Sababu Siasa zishakuwa Ulaghai;
www.jamiiforums.com
Je Mwananchi ni Mwenye Nchi ?
Sidhani, huyu jamaa field hana maamuzi, hata wale ambao hata kama akiwachagua wamuwakilishe na kumtetea (wabunge) ni kama wamekuwa watetezi na wapiga propaganda wa Serikali
Je Mwananchi ni Nguvu Kazi ?
Iwapo huyu mtu hata katika kutafuta skills (ujuzi) hapewi grants na anakopeshwa ili aje kudaiwa (na kama hana pesa basi hawezi kupata ujuzi) na mbaya zaidi akitoka huko baada ya kufilisi mali za wazazi wake kwa kumsomesha mtu huyu ujuzi aliopata wala hautafutiwi sehemu ya kuutumia ili angalau mtu huyu apate ujira (Yaani ingawa tuna uhaba wa waalimu na wauguzi ila bado kitaa kuna wauguzi na waalimu hawana ajira)
Mwananchi amekuwa Kitega Uchumi (Chanzo cha Mapato)
Ingawa hili hapo juu lilikuwa swali hapa chini naliweka kama statement..., na nitatoa mifano michache kuonyesha nachokiongelea... ingawa vitu ni vingi kuanzia kwenye matozo makubwa ya miamala bei za bundle n.k. hapa taongelea vitu viwili tu; ambavyo mwananchi huyu hata akiwa kwenye shida bado anakamuliwa...
1st Case Study; Loss Report
Sasa hivi kutokana na teknolojia ukipoteza kitu au kuibiwa hauhitaji kwenda polisi unaweza tu ukaingia kwenye mtandao na kutoa taarifa;Lormis
ni jambo jema ila kuna mambo mawili:
2nd Case Study: Passport ya Muda
Ingawa tuliambiwa East Africa tutaweza kuingiliana bila shida hilo sitaliongelea sababu linahusisha policy za nchi jirani; lakini hapo kale passport ya muda nadhani ilikuwa haizidi 1,500/= kama sikosei hata kama ilikuwa 10,000/= (nadhani sasa hivi officially huenda ikawa 20 lakini mtu mpaka aipate hata 50 itamtoka)...., Mbaya zaidi Hati hii wakati zamani ilikuwa inakaa mwaka mzima sasa hivi ni kwamba ni safari moja..., yaani ukisafiri ukirudi imekwisha (tena within miezi michache) Sasa kama mtu anafanya biashara ya kufuata matunda Kenya hata faida yake huenda haifiki hio 50k sasa hizo pesa za kulipia hio Hati anatoa wapi ?!!!
Nadhani tumetoka kwenye reli dhima ya Serikali iwe kutoa Huduma na sio kuangalia ni jinsi gani wanaweza kukusanya as much as possible; Nadhani waliomfukuza Mkoloni hawaku envision hii hali...
Siasa Mamboleo - Mdomo unapojaribu Kulidanganya Sikio
Siasa na Propaganda zimekuwa zikifanyika tangia enzi...; ila imefika wakati watu kujaribu kukwambia kwamba nyeusi ni nyekundu yaani wanadhani wakitamka mara nyingi zaidi hata wao wenyewe mdomo wao utali-convince sikio lao... Angalizo kwa hawa watu ukiwa ni mtu wa kusifia bila kupinga utaondoa...
Je Mwananchi ni Mwenye Nchi ?
Sidhani, huyu jamaa field hana maamuzi, hata wale ambao hata kama akiwachagua wamuwakilishe na kumtetea (wabunge) ni kama wamekuwa watetezi na wapiga propaganda wa Serikali
Je Mwananchi ni Nguvu Kazi ?
Iwapo huyu mtu hata katika kutafuta skills (ujuzi) hapewi grants na anakopeshwa ili aje kudaiwa (na kama hana pesa basi hawezi kupata ujuzi) na mbaya zaidi akitoka huko baada ya kufilisi mali za wazazi wake kwa kumsomesha mtu huyu ujuzi aliopata wala hautafutiwi sehemu ya kuutumia ili angalau mtu huyu apate ujira (Yaani ingawa tuna uhaba wa waalimu na wauguzi ila bado kitaa kuna wauguzi na waalimu hawana ajira)
Mwananchi amekuwa Kitega Uchumi (Chanzo cha Mapato)
Ingawa hili hapo juu lilikuwa swali hapa chini naliweka kama statement..., na nitatoa mifano michache kuonyesha nachokiongelea... ingawa vitu ni vingi kuanzia kwenye matozo makubwa ya miamala bei za bundle n.k. hapa taongelea vitu viwili tu; ambavyo mwananchi huyu hata akiwa kwenye shida bado anakamuliwa...
1st Case Study; Loss Report
Sasa hivi kutokana na teknolojia ukipoteza kitu au kuibiwa hauhitaji kwenda polisi unaweza tu ukaingia kwenye mtandao na kutoa taarifa;Lormis
ni jambo jema ila kuna mambo mawili:
- Hii ingebidi iwe nyongeza ya huduma hivyo mtu akienda polisi kama polisi ni karibu basi apate huduma sio kuambiwa nenda stationery (sitaki kuamini kwamba polisi wanashindwa kuchukua taarifa mpaka aende pengine)
- Gharama ya Loss report ilikuwa 500/= (control number) sasa hivi imekuwa (1,000/=) hio unaweza kusema sio issue sana (ingawa mtu kaibiwa) lakini hawa jamaa wameweka categories badala ya mtu kuibiwa vitu 20 uweze kuviweka vyote wameweka categories ili kila kitu ukiweke peke yake (yaani ni kama wamefanya hivyo kuongeza mapato)