Swali kwa Tundu Lissu: Kama Corona ipo Tanzania, kwanini toka alipoingia Tanzania na kipindi chote cha kampeni miezi mitatu hakuvaa Barakoa?

Alikua akiomba kura Ila kwa sasa kanyimwa anainanga serikali.
 
Maalimu Seif anaumwa nini tuanzie hapo
Ulisikia madaktari wakiongea chochote au yeye ndiye alijiongelesha? Utamwaminije mtu muongo aliongea kusudi madaktari wakanushe waseme haumwi anaumwa ugonjwa mwingine halafu aje kisiasa kusema madaktari wametoa siri za ugonjwa wake kinyume na maadili ya kidaktari kuwa ugonjwa ni siri kati ya daktari na mgonjwa

Seif anaumwa siku nyingi tena mno hajaanza leo gonjwa analoumwa analijua mwenyewe lakini huwa anashinda akitibiwa nje ya nchi
 
OK kwa hiyo alitoka eneo la Corona FREE la Tanzania ambako CORONA hakuna alikokuwa havai barakoa toka kuingia nchini akawa anaingia Corona zone ya kupaa kuelekea eneo lenye Corona!!
 
Kwani YEHODAYA . Corona (Covid 19) haipo Tanzania? Kwani aibu ya nini na Corona haijaanzia Tz?!

Tundu ndiyo unaemuona? Waulize viongozi wenye dhamana wamewaandaa wananchi namna gani.

Waulize wengine waliofanya dhihaka na Corona, leo wanajuta.
jibu swali uliloulizwa
 
Katika kipindi chote cha kampeni hakukaribiana na macorona ya CCM.
 
Natoka Muhimbili JKCI sasa hivi hakuna kuingia kumuona daktari kama hujavaa barakoa na wateja wamepungua sana kwa kuogopa maambukizi.
Jitu linaropoka eti hakuna Corona ilihali hana research,facts wala figures.
jibu swali ulilo ulizwa na mtoa mada, tumia akili au hujaelewa swali
 
Muulize mnafiki mwingine huyu anayesema Corona ipo Tanzania na huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara barakoa hana!!!! Kama Corona ipo mbona domo lake halina barakoa na hazingatii social distancing?

 
Ilipunguaje hiyo corona hapa Tz mkuu au ndio yale maombi? mimi hili jambo la Corona kupungua linanitatiza sana.
mkuu kuna hii inaitwa heard immunity watu wengi wanapata mwisho wa siku kunakuwa na kinga kwa watu na kitu kimoja muhimu Tanzania vijana wengi unaweza kupata corona wewe na wala usisikie kitu mpaka unapona na usijue kama ulikuwa na corona, ikitokea umeenda kupima lakini umeshapona corona wewe hukujuwa wao wataona hawa askari Antibodies dalili ulipata corona sasa hawa askari ndio kinga. Na wengi sana wana corona bila kuumwa. chukulia Malaria akija mtu toka nje maisha yake hajawahi kupata malaria akija kupata anapata shida sana mwili ukijenda askari wa malaria akija kupata tena ataenda kununua dose tu mwenyewe. umewahi kusikia wachezaji maarufu kwa kuwa wanapimwa corona kimchezo anaambiwa una corona ila hawaumwi kitu ina maana asingepima wala asingejuwa kama ana corona.
 
Kusema wewe kitu ni cha msingi sio lazima kiwe cha msingi kwangu au kwa mwingine

Itoshe kusema ni la msingi kwako wewe

Mimi naliona hovyo kabisa

Asante
Ila sishangai maana hata humu mnabishana kwamba wengine wanasema corona hakuna na wengine wanasema ipo halafu wote mnazungumzia nchi moja,kila mtu kachagua kuona anavyotaka.
 
Natoka Muhimbili JKCI sasa hivi hakuna kuingia kumuona daktari kama hujavaa barakoa na wateja wamepungua sana kwa kuogopa maambukizi.
Jitu linaropoka eti hakuna Corona ilihali hana research,facts wala figures.

Watu tuchukue tahadhari afya yako ndio mtaji wako. Mimi pia jana nimeenda hospital dodoma, hospital ni full barakoa. Pia sijaona sababu ya kusubiri mpaka tuambiwe wakati njia za kujikinga tunajua.
 
Upinzani mbaya sana.

Mtu anatamani ata nusu ya Watanzania wafe ili apate la kuongea, kwann Watanzania tusiwe wamoja.
Anayetamani wafe ni yule anayewadnganya tatizo halipo kumbe lipo na yeye anajua lipo.
 
Ndio maana niksema kuwa hili suala la Corona kupungua linanichanganya kwa sababu kila mmoja anaeleza kivyake kuhusu kupungua kwa corona Tz,wengine wanasema tulifanya maombi na kuzingatia tahadhari za kujikinga na corona kama kuvaa barakoa kunawa mikono na kuepusha misongamano hizo ndio mbinu zilizotumika hadi corona ikapungua.
Sasa wewe unaeleza habari za heard immunity.
 
Muulize mnafiki mwingine huyu anayesema Corona ipo Tanzania na huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara barakoa hana!!!! Kama Corona ipo mbona domo lake halina barakoa na hazingatii social distancing?

Kwania corona haipo Tanzania.......Raisi alisema watu wamekwenda nje kupata chanjo na wameleta corona ya ajabu ajabu.......bado unampinga hata yeye....au ni Tanzania gani unayoisemea?
 
Suala la maombi ondoa hilo, kuomba ni vizuri lakini hakuna maajabu katika kupona ni lazima utibiwe. Suala la kunawa mikono, kuvaa barakoa na mikusanyiko kuzuiwa wakati ule yes inaweza kuwa imesaidia sana tu lakini pia kuna heard immunity. haya yote uliyosema yalichangia ila tusiseme maombi hapana hiyo ni siri ya Mungu kama alipokea maombi au hapana hatuna njia ya kuthibitisha. Tuseme kweli maombi sasa tumekosa nini tena limeturudia tena?
 
Lissu kutovaa barakoa hakumnyimi uhuru wake wa kusema Corona ipo na ilikuwepo. Labda hakuwa akiamini kama COVID19 inaenezwa kupitia mdomoni, sikioni na machoni as long as mtu hajakugusa

Bottom line: ukweli unabaki kuwa ukweli regardless ya mtu anasema na kuamini kipi
 
Upinzani mbaya sana.

Mtu anatamani ata nusu ya Watanzania wafe ili apate la kuongea, kwann Watanzania tusiwe wamoja.
Anaetamani wafe ni yupi anayetamani ujihadhari au anayekudanganya ili ufe.
 
Mpaka kufika hapa sijaona jibu lolote la maswali ya mleta mada zaidi ya makejeli tu yasio na maana yoyote ile.
 
Duh haya mkuu.
 
Subiri itapokulaza au kumlaza ndugu yako ndo utajua ipo au haipo.
 
wewe im
Subiri itapokulaza au kumlaza ndugu yako ndo utajua ipo au haipo.
Itakulaza wewe unayeamini ipo.wewe imekulaza? ndugu yako gani imemlaza tupe jina mahali aliopkuwa akiishi na hospitali alikatokomea na kifo tuhakiki kama kafa kwa Corona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…