Swali kwa wasomi wa Jiografia na Fizikia wenye akili zao, kama ulienda shule kukariri pita mbali

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karibuni
 
Dunia haizunguki, dunia ni tambarare.

Maji hayapindi, maji hufuata level iliyo nyooka, asilimia 75 ya uso wa dunia ni maji.

Jua linazunguka kutoka mashariki kwenda magharibi.

Juu ya anga kuna kizuizi, hakuna anayeweza kutoka. Juu kuna maji chini kuna maji.

As above, so below.
 
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi;
kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Tuanze na ww kwanza unaweza thibitisha dunia inazunguka? Ukipata jibu lako ndio tukupe jibu la swali lako
 
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi;
kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Swali lako lina msingi mzuri, lakini kuna sababu kadhaa za kisayansi zinazofanya ndege au helikopta zisifanye hivyo.

1. Ndege, Helikopta, na Atmosphere Vinazunguka Pamoja na Dunia: Dunia inazunguka kwa kasi ya takriban 1,674 km/h kwenye ikweta. Hata hivyo, si Dunia pekee inayozunguka — angahewa, ikiwa ni pamoja na ndege na helikopta, pia inazunguka pamoja na Dunia kwa kasi hiyo hiyo. Kwa sababu ya hili, kama ndege au helikopta itapaa juu, itabaki ikiendelea kusogea kwa kasi ile ile ya mzunguko wa Dunia.

2. Kanuni ya Inertia: Kanuni ya kwanza ya Newton ya mwendo inasema kwamba kitu chochote kilicho katika mwendo kitaendelea katika mwendo huo isipokuwa nguvu ya nje itumike kukibadilisha. Kwa kuwa ndege au helikopta tayari zina mwendo wa kasi ya mzunguko wa Dunia, zinahitaji nguvu kubwa sana ili kuzizuia zisisogee pamoja na Dunia.

3. Uhitaji wa Nguvu za Nje:Ili ndege au helikopta zisitii mwendo wa Dunia, zingehitaji nguvu ya nje (kama vile injini zenye nguvu) ili kuondoa mwendo huo. Hii haifanyiki kwa sababu ni ngumu mno na kinyume na kanuni za fizikia za kawaida.

Kwa hiyo, ndege au helikopta zinapaswa kuruka kwa kawaida ili kufika mahali zinapohitaji, kwa sababu ziko ndani ya angahewa inayozunguka pamoja na Dunia.
 
Nithibitishe kwa kipi zaidi ya maandishi??

Na tayari nimeandika kwamba asilimia 75 ya dunia ni maji, na maji hayawezi kupinda au kuwa na mkunjo, hivyo kwa kutumia common sense unapata majibu.
fafanua kidogo ongezea nyama
 
Dunia inazunguka pamoja na kilichopo juu ya ardhi, ni sawa na kusema nzi akiwa ndani ya ndege akataka kuruka kutoka siti ya nyuma kwenda siti ya mbele atashindwa kufika kwa vile ndege inakimbia kwa kasi sana, Hapana si kweli huyo nzi atafika vizuri tu sababu ndege inayembea na yeye anatembea hayupo excluded. Ndivyo ilivyo kwa helikopta hiyo uliyoitolea mfano. Ngoja wanafizikia waje wakufafanulie kitaalamu zaidi.
 
Dunia haizunguki, dunia ni tambarare.
Ujinga hujaelewa geography rudi shule
Dunia inazunguka

Mfano ukichukua mpira wa miguu ukaweka sisimizi juu ya mpira kisha uzungushe mkononi sisimizi hawezi Anguka chini

Binadamu na maji yote uyaonayo ya mito na bahari ni kama kisisimizi tu kwenye tufe la dunia ndio maana hata likizunguka hatuwi kichwa chini miguu juu na kudondoka kama sisimizi tu ukiweka juu ya mpira wa miguu atabaki wima tu
 
Mtu/ndege i(u)naporuka i(u)naruka na spidi hiyohiyo ya dunia + yako/yake na uelekeo/direction ile ile hivyo huwezi kutua nyuma/mbele ya.
Kwa ufupi wewe hapo ulipo unatembea spidi sawa na dunia japo hujiskii kama unatembea. Hata ukiwa ndani ya gari linalotembea ukiruka uelekeo mmoja na gari linapoelekea huwezi kuanguka kutoka garini maana tayari uliruka ukiwa na spidi ya gari na uelekeo mmoja sawa na gari.
 
Swali lako lina msingi mzuri, lakini kuna sababu kadhaa za kisayansi zinazofanya ndege au helikopta zisifanye hivyo.

1. Ndege, Helikopta, na Atmosphere Vinazunguka Pamoja na Dunia: Dunia inazunguka kwa kasi ya takriban 1,674 km/h kwenye ikweta. Hata hivyo, si Dunia pekee inayozunguka — angahewa, ikiwa ni pamoja na ndege na helikopta, pia inazunguka pamoja na Dunia kwa kasi hiyo hiyo. Kwa sababu ya hili, kama ndege au helikopta itapaa juu, itabaki ikiendelea kusogea kwa kasi ile ile ya mzunguko wa Dunia.

2. Kanuni ya Inertia: Kanuni ya kwanza ya Newton ya mwendo inasema kwamba kitu chochote kilicho katika mwendo kitaendelea katika mwendo huo isipokuwa nguvu ya nje itumike kukibadilisha. Kwa kuwa ndege au helikopta tayari zina mwendo wa kasi ya mzunguko wa Dunia, zinahitaji nguvu kubwa sana ili kuzizuia zisisogee pamoja na Dunia.

3. Uhitaji wa Nguvu za Nje:Ili ndege au helikopta zisitii mwendo wa Dunia, zingehitaji nguvu ya nje (kama vile injini zenye nguvu) ili kuondoa mwendo huo. Hii haifanyiki kwa sababu ni ngumu mno na kinyume na kanuni za fizikia za kawaida.

Kwa hiyo, ndege au helikopta zinapaswa kuruka kwa kawaida ili kufika mahali zinapohitaji, kwa sababu ziko ndani ya angahewa inayozunguka pamoja na Dunia.

Sahihi kabisa huu uzi kuishia hapa.
 
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi;
kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Mipaka ya dunia inaishia wapi? Ni umbali gani ambao kitu kikiwa umbali huo kinakuwa hakiko duniani?

Je, umbali ambao helikopta inapaa au binadamu anaruka, kwa mifano uliyotoa, wanakua bado wako duniani? Kama bado wako duniani ni sahihi kudondokea pale pale. Kajifunze the so called "escape velocity".
 
Back
Top Bottom