Swali kwa wasomi wa Jiografia na Fizikia wenye akili zao, kama ulienda shule kukariri pita mbali

Swali kwa wasomi wa Jiografia na Fizikia wenye akili zao, kama ulienda shule kukariri pita mbali

"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi;
kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Kwenye dunia na Kwenye sayari nyengine pamoja na nyota na mwezi kunakuwa na kitu kinaitwa tabaka la anga hewa, ambapo tabaka hili linatenganisha sehemu mbili eneo la ndani ya sayari na eneo la nje ya sayari.

Sasa bwana maeneo haya mawili yametengwa na tabaka la anga hewa yani lile eneo la nje ambapo huko mtu anaweza kuelea na wala hakuna oxygen alafu kuna hili eneo la ndani ambalo sisi ndio tunaishi lenye oxygen, eneo hili ndilo tunalo ishi sisi. Ambalo mvua hutunyesheaga

Sasa twende kwenye swali lako kwanini kama dunia inazunguka vitu huwa hawavipotei mwelekeo wake mfano ndege

Kwa kawaida eneo la ndani limezungukwa na hewa ambayo sisi tunapumulia na ndege hupaa kwa sababu ya uwepo wa hewa hiyo ambayo ni oxygen, hydrogen, carbon nk hewa hii ipo ndani ya eneo la dunia yani kwenye sakafu ya dunia na inashikiriwa na kitu kinaitwa gravity, kwa kawaida gravity ya sayari huwa na nguvu sana kwenye sakafu ya dunia na ndani ya dunia kwenye core hivyo hii hupelekea dunia kuwa eneo la ndani lenye mgandamizo wa hewa mbalimbali na eneo la nje ambalo halina gravity yoyote


Gravity ni ile nguvu ya sumanku kwa jawaida sumanku huwa na nguvu ndogo endapo utakaa nayo mbali likini sumanku hiyo huwa na nguvu kubwa endapo utakaa nayo karibu au kwenye sakafu yake mfano huu ndio sawa na dunia kwa kifupi kuna eneo lina nguvu ndogo ambalo ni nje ya dunia na kuna eneo lina nguvu kubwa za mvutano kiasi kwamba ukiwa katika eneo hili huwezi kucholopoka hatakama dunia itakuwa na kasi gani


Wanasayansi wanasema sisi ni kama sisimizj kwenye dunia hii inaweza kuwa sababu ya vitu kutochoripoka nje na hatimae dunia inakuwa na maeneo mawili eneo la ndani la tabaka na eneo la nje ya tabaka ukikaa ndani zaidi ya dunia basi utashikiriwa na dunia na ukikaa mbali basi hauta shikirwa na dunia.
 
Swali lako lina msingi mzuri, lakini kuna sababu kadhaa za kisayansi zinazofanya ndege au helikopta zisifanye hivyo.

1. Ndege, Helikopta, na Atmosphere Vinazunguka Pamoja na Dunia: Dunia inazunguka kwa kasi ya takriban 1,674 km/h kwenye ikweta. Hata hivyo, si Dunia pekee inayozunguka — angahewa, ikiwa ni pamoja na ndege na helikopta, pia inazunguka pamoja na Dunia kwa kasi hiyo hiyo. Kwa sababu ya hili, kama ndege au helikopta itapaa juu, itabaki ikiendelea kusogea kwa kasi ile ile ya mzunguko wa Dunia.

2. Kanuni ya Inertia: Kanuni ya kwanza ya Newton ya mwendo inasema kwamba kitu chochote kilicho katika mwendo kitaendelea katika mwendo huo isipokuwa nguvu ya nje itumike kukibadilisha. Kwa kuwa ndege au helikopta tayari zina mwendo wa kasi ya mzunguko wa Dunia, zinahitaji nguvu kubwa sana ili kuzizuia zisisogee pamoja na Dunia.

3. Uhitaji wa Nguvu za Nje:Ili ndege au helikopta zisitii mwendo wa Dunia, zingehitaji nguvu ya nje (kama vile injini zenye nguvu) ili kuondoa mwendo huo. Hii haifanyiki kwa sababu ni ngumu mno na kinyume na kanuni za fizikia za kawaida.

Kwa hiyo, ndege au helikopta zinapaswa kuruka kwa kawaida ili kufika mahali zinapohitaji, kwa sababu ziko ndani ya angahewa inayozunguka pamoja na Dunia.
Sijaelewa sjui ni kichwa changu kigumuu
 
Wewe punguani hivi ulitolewa marinda na muislamu? Naona unachuki sana,
Hapa dini inaingiaje Punga wewe?
Pole sana kwa kupoteza marinda.
Maalim wengi wa Madrasa za kiislamu sifa ya kwanza lazima wawe na viboko

Hao ndio husifika kuwa maalimu bora ma Proffessor

kurani na maandishi ya kiarabu kusoma na kuandika hayapandi kwa mtoto bila viboko

Takbiriiiiiiiii
 
Maalim wengi wa Madrasa za kiislamu sifa ya kwanza lazima wawe na viboko

Hao ndio husifika kuwa maalimu bora ma Proffessor

kurani na maandishi ya kiarabu kusoma na kuandika hayapandi kwa mtoto bila viboko

Takbiriiiiiiiii
Una akili ndogo kama sisimizi,unaonekana maisha yamekupiga mpaka ukaamua kujifariji kwenye kukashifu imani zingine,

Jitulize tu binti mpaka utakapo pata posa nyingine,kupewa talaka sio mwisho wa maisha yako.
 
Una akili ndogo kama sisimizi,unaonekana maisha yamekupiga mpaka ukaamua kujifariji kwenye kukashifu imani zingine,
Nimekashifu wapi?

Madrasa ziko mitaani na tunaziona na ma ustaadhi na viboko vyao kulazimisha watoto wakariri kuruani na kujua kusoma na kuandika hayo maandishi ya kiarabu ya kutoka kulia kwenda kushoto kwani siri?

Mitaani Madrasa zimezagaa na ma Ustaadhi wana viboko mikononi

Takbiriiiiiiiii
 
Dunia haizunguki, dunia ni tambarare.

Maji hayapindi, maji hufuata level iliyo nyooka, pia asilimia 75 ya uso wa dunia ni maji.

Jua linazunguka kutoka mashariki kwenda magharibi.
Jua linatoka mashariki kwenda magharibi,kwahiyo likifika huko magharibi kesho yake anaelirudisha litoke tena mashariki ni nani,au kuna majua mengine linatokea tena lingine mashariki...
 
Una akili ndogo kama sisimizi,unaonekana maisha yamekupiga mpaka ukaamua kujifariji kwenye kukashifu imani zingine,

Jitulize tu binti mpaka utakapo pata posa nyingine,kupewa talaka sio mwisho wa maisha yako.
Haha Ila watu mnajua kutoana kwenye relii. Mpunguzie mwenzio maneno
 
Jua linatoka mashariki kwenda magharibi,kwahiyo likifika huko magharibi kesho yake anaelirudisha litoke tena mashariki ni nani,au kuna majua mengine linatokea tena lingine mashariki...
Rotation unaelewa maana yake ? Tuanzie hapo kwanza
 
"Kama tunaambiwa Dunia inazunguka kwa kasi ya 1,674km/saa, kwanini ndege au helikopta hazipai juu, zikaganda na kusubiri sehemu inapohitaji kwenda ifike kisha itue?"

Nadhani swali limefanana hivi; kama Dunia inazunguka kasi hiyo, kwanini binaadam akiruka anatua palepale na si sehemu nyingine?

Tunasoma majibu yenu sehemu ya maoni. Karubuni
Ukijua kwanini drone ambayo imefungiwa kwenye basi ikaganda hewan haiwezi kujikuta nyuma ya basi bali itabaki palepale hata kama basi linakmbia utaelewa kwanini ndege ikiganda hewani haiwezi jikuta nchi nyingine.
Ni kwa sababu dunia inazunguka na kila kitu chake hata kilicho kwenye atmosphere
 
Jua linatoka mashariki kwenda magharibi,kwahiyo likifika huko magharibi kesho yake anaelirudisha litoke tena mashariki ni nani,au kuna majua mengine linatokea tena lingine mashariki...
Swali nzuri, kama ambavyo huwezi kusema ni kitu gani kina usukuma upepo, pia hakuna kitu kinacho lisukuma jua.

Jua limeumbwa kuzunguka katika mkondo wake na katika njia yake sambamba na mwezi.

Leo unaona mwezi upo kushoto, kesho unauona umehama kulia.
 
Nje ya mada.

Nakumbuka niliwahi kuchapwa na mwalimu wangu wa physics kwasababu ya kuuliza maswali ya design hii.

Niliwahi kuuliza swali hili; assume una njiwa (ndege) wenye jumla ya uzito wa kilograms 1000 kisha ukawapakia ndani ya ndege (aeroplane) na hao njiwa wakawa wanaruka (wanapaa) pasipo kutua ndani ya hiyo aeroplane, swali; Je, ndege (aeroplane) hiyo itakuwa imebeba uzito kiasi gani? Kwanini?
Mimi huwa napenda kujibu maswali ya kiwaki kama yaha, wewe ungekuwa mwanafunzi wangu wala nisinge kupiga.

Hao njiwa wakiruka humo ndani ya ndege uzito wao utaendele kuhesabika hata kama hawata tua, hii ni kwasababu kwenye cabin kuna hewa ambayo pia ina uzito unajumlishwa kwenye total mass ya ndege,

Njiwa wakipaa humo watasababisha mgandamizo wa hewa humo kwenye cabin yaani mass of air displaced ni sawa na mass ya njiwa.
 
Sijaelewa sjui ni kichwa changu kigumuu

Hapa nitakupa mfano rahisi ili kuelezea kwanini ndege au helikopta hazipai na kuganda kisha kusubiri sehemu zifike.
Dunia inazunguka kwa kasi ya takriban 1,674 km/saa pale ilipo ikiwemo anga na hewa yote inayotuzunguka. Mfano rahisi ni huu:
Fikiria uko ndani ya basi linalotembea kwa kasi kubwa kwenye barabara ya lami.

Ukiwa ndani ya basi hilo, unaweza kucheza mpira, kuruka juu na kushuka chini bila kuhisi kama unazunguka kwa kasi kubwa sana, siyo? Hii ni kwa sababu kila kitu ndani ya basi kinahama kwa kasi moja na basi hilo. Hivyo, mpira wako, wewe, na hewa yote ndani ya basi, vyote vina hama pamoja na basi kwa kasi ile ile.


Sasa angalia angahewa ya Dunia kama hiyo hali ndani ya basi. Wakati Dunia inazunguka, angahewa yote (ikijumuisha ndege au helikopta) inazunguka nayo.

Ndege inapopaa, bado inasukumwa pamoja na angahewa ambayo inahama kwa kasi ile ile ya mzunguko wa Dunia.

Kwa hivyo, ndege haiwezi kuganda hewani na kusubiri mahali pake ifike kwa sababu angahewa yote nayo inahama pamoja na Dunia kwa kasi hiyo hiyo.


Mfano mwingine, fikiria ukiweka mpira juu ya meza inayosogea. Kama meza inavyosogea, mpira hauwezi kubaki palepale kwenye hewa kwa sababu meza na mpira vinahama kwa kasi moja.


Hivyo, ili ndege ihame kutoka sehemu moja hadi nyingine, inabidi itumie injini zake kuondoka kwenye kasi hiyo ya pamoja na angahewa, kwa kuongeza au kupunguza kasi yake kulingana na mwelekeo inaotaka kwenda.
 
Back
Top Bottom