tamsana
JF-Expert Member
- Jan 13, 2012
- 3,739
- 8,044
Kazi iendelee!
Wadau mtakuwa mashuhuda wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na seriksli kupitia Ilani ya CCM tangu awamu ya kwanza hadi hii ya sita. Pongezi nyingi ziwafikie viongozi wote wa awamu zote kwa jitihada zao za kutatua changamoto za wananchi.
Pamoja na hayo, kuna baadhi ya miradi kila awamu tunaona ikitekelezwa maeneo mbalimbali ya nchi hii lakini bado changamoto inabakia palepale.
Kwa mfano, eneo nililopo imefanyika miradi mbalimbali ya maji, vimejengwa visima mbalimbali kwa ajili ya kusambaza maji lakini changamoto ya maji haijawahi kuisha. Yaani mradi ukiisha baada ya mwezi mmoja changamoto inarudi palepale.
Ukifuatilia utagundua kuwa miradi ya maji inatumia fedha nyingi sana zikiwemo za misaada na zile zinazotokana na kodi za wananchi.
Zaidi sana utagundua tangu awamu ya kwanza hadi hii ya sita hakujawahi kukosekana mradi wa maji. Utakuta miundombinu ya maji ipo ni mizuri na pengine ni ya kisasa kabisa lakini upatikanaji wa maji una kuwa changamoto kubwa sana.
Binafsi nimetafakari lakini sijawahi kupata majibu kuhusu baadhi ya hii miradi inayotekelezwa lakini haitatui changamoto za wananchi.
JE, TATIZO NI NINI?