Swali la kichokozi: Pamoja na Watumishi hewa kuondolewa na Serikali kutokuongeza mishahara, mbona gharama za mishahara zinapanda kila uchwao?

Excellent put...

This is very good.. good

Umetoa hoja nzuti sana 100%... kuna wanajaribu kubisha lakini, sioni kama wanakuja na hoja zaidi ya matusi.
 
Chadema watapinga tu hawana jema hao
Sio issue ya Chadema, ni mambo ya kitaifa haya.

Namba hazina chama.. Hivi kwani hatuwezi kubishana bila kuwekeana mambo ya uchama?

Dalili za mtu asiyekuwa na hoja ni kuanza kuattach mtu personally, kama wewe unavojaribu kufanya.
 
Payrol ya serikali ni very dynamic. Kuna ajira, mpya, kupanda vyeo/madaraja, malimbikizo ya nyongeza za mshahara, teuzi, tenguzi, taasisi mpya n.k.

Huwezi kutegemea ikabaki vile vile kila mwezi.
 
Tanzania ipi unaizungumzia mkuu? Tuanzie hapo kwanza maana inawezekana tunaishi nchi mbili tofauti.
Ni Tanzania hiihii ya rais Magufuli mkuu, tafuta viambatanisho vya hizo takwimu ulizoleta utaelewa
 
Nilitegemea wewe ndo utie hizo figure kupinga nilichokieleza...

Btw, wakurugenzi 8, hao ni sample tu.. kuna wengi sana walitumbuliwa na wakaendelea kula mshahara kwa miezi kadhaa...
 
Payrol ya serikali ni very dynamic. Kuna ajira, mpya, kupanda vyeo/madaraja, malimbikizo ya nyongeza za mshahara, teuzi, tenguzi, taasisi mpya n.k.

Huwezi kutegemea ikabaki vile vile kila mwezi.
Huna hoja... ajira ilisimama kwa almost 3 years... madaraja hayakupanda, wa vyeti feki walitimuliwa, wafanyakazi hewa waliomgharimu mkuu wa mkoa wa wakati huo wa mkoa wa Shinyanga... athali za hayo yote umeziona kwenye graph la mishahara..!?

Hizi ajira zinazotangazwa sasa ni za kuombea kura tu..

NAMNUKUU MBUNGE MSTAAFU WA KILWA, BWANA BWEGE ... ALISEMA... tunawajua CCM, wanabanaa, lakini wakifika mwishooooniii... WATAACHIA TU...
 
Acha uwongo madaraja na ajira zilisimamishwa..!!!

Nieleweshe kwa kunitajia idara za serikali zilizoongeka
 
Acha uwongo madaraja na ajira zilisimamishwa..!!!

Nieleweshe kwa kunitajia idara za serikali zilizoongeka
Unakataa kwa kigezo gani mkuu? Watu wamepandishwa madaraja wengi tuu na Hilo ni zoezi endelevu
 
Unakataa kwa kigezo gani mkuu? Watu wamepandishwa madaraja wengi tuu na Hilo ni zoezi endelevu
My question is very specific..lakini jibu lako lipo very general...
Vigezo vinavyonisukuma kukataa hoja yako ni hivi vifuatavyo...
1. Hakukuwa na ongezeko la mshahara gharama ingebaki pale pale maana hakukuwa na ongezeko
2. Hakukuwa na kupanda madaraja hivyo gharama isingeongezeka, at least ingebaki pale pale (kwa kigezo hiki)
3. Uhakiki wa madeni ya walimu ulishika hatamu, kusinhekuwa na ongezeko maana hakuna madeni ya walimu yaliyokuwa yanalipwa.
4. Kulikuwa na watu walioonekana kumiliki vyeti feki. gharama ingeshuka maana umewapunguza wa vyeti feki
5. Kulikuwa na wafanyakazi hewa walioondolewa, hivyo kulitakiwa kuonekane kushuka kwa gharama za mishahara kwa vile wafanyakazi hewa hawakuwa wanalipwa tena....
6. Hakukuwa na ajira mpya, hii ingepelekea gharama kubaki pale pale maana hakuna mwajiliwa mpya

NB: tunazungumzia ajira mpya, si za kujaza nafasi ya aliyestaafu, aliyekufa, aliyeacha kazi, maana hawa hawaongezi gharama, bali wanagharimiwa kwa hela ya walioondoka kwa sababu yoyote ile...

Hayo yote umeona effect yake kwenye upandaji wa mishahara?

Hizo ajira na madaraja ni kipindi hiki cha uchaguzi... IN SHORT NI ZA KUOMBEA KURA TU...
 
Acha siasa za kishamba, kila mwaka serkali inaajiri
Pamoja na kuwa hunaga uwezo wa kujenga hoja, au pengine unakimbia hoja, ngoja nijaribu kukujibu.

Wewe na mtoa uzi wote mmesema "ukweli". Serikali ya magufuli inaajiri na pia haiajiri.

Zipo taratibu za ajira, ili kufidia ongezeko la mahitaji ya huduma, kufidia wanaostaafu, kuacha kazi, kufukuzwa kazi, au kufariki. Kwa miaka mingi hizo ndio zimekuwa taratibu za serikali .


Iliwahi kutokea serikali ikasitisha ajira huko nyuma. Matokeo yake mpaka hivi sasa kuna sekta nyingi zinaumia na kuligharimu taifa. Mfano katika mifumo ya vyuo vikuu, mhitimu anayefanya vizuri katika shahada ya kwanza, anaajiriwa kama Tutorial Assistant, TA. Baadae anapandishwa na kuwa Assistant Lecturer . Wakati huu anatakiwa kufanya shahada ya pili, na halafu ya tatu, PhD. Hapa atakuwa chini ya Profesa, ambaye atamwongoza. Hatimaye naye atapanda ngazi mbalimbali kadirivya uwezo wake. Sasa chuo kikiacha kuajiri maTA, huku maprofesa wakiendelea kuzeeka mpaka kustaafu, kutakuwa na "gap" kubwa sana, pale wakianza kuajiri TA tena. Hasara nyingine ya kuajiri watu wengi mara moja ili kujaza hizi "gap", matokeo yake hawa watastaafu wengi kwa mara moja, na tatizo litaendelea. Pia hakutakuwa na uhifadhi wa uzoefu na maarifa yaliyotengenezwa kwa gharama kubwa na kwa miaka mingi, kwa kuwa wafanyakazi " nguli" hawana wa kuwarithisha.

Ni kweli Magufuli anaajiri, lakini si katika utaratibu unaotakiwa kama nilivyotoa mifano hapo juu. Utaratibu wa sasa ni kutoajiri kwa kawaida, ila kwa mlipuko, baada ya miaka kadhaa. Kuna maelfu ya wahitimu wa ualimu, udaktari, nk. wapo mtaani. Ila utasikia wameajiriwa madaktari 1000, wakati wa dharura. Au JKT 70 wamehitimisha mafunzo kwa mbwembwe fulani, rais anafurahi na kuagiza waajiriwe wote! Hapo hakuna taratibu za Personnel management , bali hisia za rais.

Kichekesho kimetokea hapa karibuni. Lilitoka tangazo ka ajira kwenye vyuo kadhaa. Mchakato ukafanyika, wa interviews nk. Ghafla kila kitu kikawekwa kando, likatoka tangazo lingine. Kwamba wanaohitaji kuhamishwa toka serikalini kwenda kufanya kazi kwenye vyuo, wajotokeze! Huu ni mfano tu wa usanii wa serikalivya Magufuli. Maana hata kama kuna ziada ya wafanyakazi huko serikalini, ambapo sio rahisi pia, kuna njia tofauti za kushughulika na hiyo ishu.

Kwa hiyo ki uhalisia, serikali ya Magufuli haiajiri, na hili ni bomu litakalo tuvuruga kwa miaka mingi ijayo, na nina uhakika magufuli hana habari na hili tatizo. Hata akiambiwa, hana uwezo wa kulielewa. Anaweza kuelewa kilomita ngapi za barabara, makalveti mangapi, madaraja mangapi, basi. Hata wewe mpambe wake sina hakika Kama utaelewa ishu subtle kama hizi
 
Unakataa kwa kigezo gani mkuu? Watu wamepandishwa madaraja wengi tuu na Hilo ni zoezi endelevu
Nawafahamu kadhaa waliopandishwa madaraja. Ila waliolipwa stahiki za madaraja yao ni wachache saaana. Wengi wanaarifiwa utalipwa kuanzia tarehe fulani, halafu zinafuata danadana nyiiingi za kuahirishwa kila mara. Usanii wa aina hii haujawahi kutokea
 
Tatizo mnakuwa na majibu yenu Tayari!
 
Nawafahamu kadhaa waliopandishwa madaraja. Ila waliolipwa stahiki za madaraja yao ni wachache saaana. Wengi wanaarifiwa utalipwa kuanzia tarehe fulani, halafu zinafuata danadana nyiiingi za kuahirishwa kila mara. Usanii wa aina hii haujawahi kutokea
Lete number kumaliza utata wa idada ya waliopata stahiki mwaka baada ya mwaka mkuu, kusema tuu kwamba ni wachache inawezekana ukawa sahihi au usiwe sahihi. Waliotoa hizo data lazima wana number sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…