Swali la kichokozi: Pamoja na Watumishi hewa kuondolewa na Serikali kutokuongeza mishahara, mbona gharama za mishahara zinapanda kila uchwao?

Swali la kichokozi: Pamoja na Watumishi hewa kuondolewa na Serikali kutokuongeza mishahara, mbona gharama za mishahara zinapanda kila uchwao?

You might have a point... lakini kumbuka haya
1. Ajira ilisimamishwa
2. Madaraja yalisimamishwa

HIYO EFFECT YA WAFANYAKAZI HEWA NA WA VYETI FEKI, UMEIONA KWEYE GRAPH? Kwa maelezo uliyoyatoa, nilitegemea graph ipande, ifike mwaka wa kuondolewa wafanyakazi hewa na wa vyeti feki, at least kuwe na significant drop ya gharama, then ipande kwa uliyoyasema...

Ulivyoongea ni as if baada ya kutoka walioondoka, wakaajiriwa wapya wa ghara ile ile kama walioondolewa na siku hiyo hiyo walioondolewa...

Kumbuka hili..
Wale wakurugenzi 8 waliotumbuliwa, watano walikuwa replaced emadiately wakati kesi bado inaunguruma... Kwa hiyo, waliotumbuliwa wakawa wanaendelea kulipwa mishahara.. Hii maana yake, kwa nafasi zile 5, mishara miwili ilikuwa inalipwa kwa nafasi moja... aliyetumbuliwa na mpya... THIS WENT ON FOR A YEAR.. na watumbuliwa wakaja lipwa..!!! UFAHAMU TU KWAMBA PARTLY, MISHAHARA ILIPANDA KWA SABABU YA MAAMUZI YASIYOFUATA TARATIBU TULIZOJIWEKEA
Excellent put...

This is very good.. good

Umetoa hoja nzuti sana 100%... kuna wanajaribu kubisha lakini, sioni kama wanakuja na hoja zaidi ya matusi.
 
Chadema watapinga tu hawana jema hao
Sio issue ya Chadema, ni mambo ya kitaifa haya.

Namba hazina chama.. Hivi kwani hatuwezi kubishana bila kuwekeana mambo ya uchama?

Dalili za mtu asiyekuwa na hoja ni kuanza kuattach mtu personally, kama wewe unavojaribu kufanya.
 
Payrol ya serikali ni very dynamic. Kuna ajira, mpya, kupanda vyeo/madaraja, malimbikizo ya nyongeza za mshahara, teuzi, tenguzi, taasisi mpya n.k.

Huwezi kutegemea ikabaki vile vile kila mwezi.
 
Tanzania ipi unaizungumzia mkuu? Tuanzie hapo kwanza maana inawezekana tunaishi nchi mbili tofauti.
Ni Tanzania hiihii ya rais Magufuli mkuu, tafuta viambatanisho vya hizo takwimu ulizoleta utaelewa
 
Lakini figures si zipo, kwa nini hazipatikani tunafanya guess work. Tupe idadi ya waliotumbuliwa na kiasi cha mishahara yao, then tupatie idadi ya watumishi hewa na mishahara yao. Ninavyofahamu mimi naweza nikawa sipo sahihi wafanyakazi walikuwa wanaendelea kupandishwa madaraja. Wakurugenzi 8 hata kama wanaendelea kulipwa kwa mwaka moja impact yao kwenye graph haiwezi kuwa kubwa kulinganisha na idadi ya waliokuwa na vyeti fake.

BTW unaweza kuweka time frame na ushahidi wa: 1. Ajira ilisimamishwa, 2. Madaraja yalisimamishwa au link kuangalia time frame.
Nilitegemea wewe ndo utie hizo figure kupinga nilichokieleza...

Btw, wakurugenzi 8, hao ni sample tu.. kuna wengi sana walitumbuliwa na wakaendelea kula mshahara kwa miezi kadhaa...
 
Payrol ya serikali ni very dynamic. Kuna ajira, mpya, kupanda vyeo/madaraja, malimbikizo ya nyongeza za mshahara, teuzi, tenguzi, taasisi mpya n.k.

Huwezi kutegemea ikabaki vile vile kila mwezi.
Huna hoja... ajira ilisimama kwa almost 3 years... madaraja hayakupanda, wa vyeti feki walitimuliwa, wafanyakazi hewa waliomgharimu mkuu wa mkoa wa wakati huo wa mkoa wa Shinyanga... athali za hayo yote umeziona kwenye graph la mishahara..!?

Hizi ajira zinazotangazwa sasa ni za kuombea kura tu..

NAMNUKUU MBUNGE MSTAAFU WA KILWA, BWANA BWEGE ... ALISEMA... tunawajua CCM, wanabanaa, lakini wakifika mwishooooniii... WATAACHIA TU...
 
Kabisa
Na pia kuna watumishi wa kada tofauti wamepandishwa madaraja kwa kipindi hiki cha miaka4,
kumekua na uboreshaji wa utendaji uliopelekea kuboresha au kuanzishwa vitengo na idara mpya serikalini ambazo zimeongeza waajiriwa pia
Na kuna ulipwaji wa stahiki za watumishi ikiwa ni pamoja na likizo, malimbikizo, uhamisho na kadhalika.
Ukiwauliza wizara husika watakupa majibu sahihi
Acha uwongo madaraja na ajira zilisimamishwa..!!!

Nieleweshe kwa kunitajia idara za serikali zilizoongeka
 
Acha uwongo madaraja na ajira zilisimamishwa..!!!

Nieleweshe kwa kunitajia idara za serikali zilizoongeka
Unakataa kwa kigezo gani mkuu? Watu wamepandishwa madaraja wengi tuu na Hilo ni zoezi endelevu
 
Unakataa kwa kigezo gani mkuu? Watu wamepandishwa madaraja wengi tuu na Hilo ni zoezi endelevu
My question is very specific..lakini jibu lako lipo very general...
Vigezo vinavyonisukuma kukataa hoja yako ni hivi vifuatavyo...
1. Hakukuwa na ongezeko la mshahara gharama ingebaki pale pale maana hakukuwa na ongezeko
2. Hakukuwa na kupanda madaraja hivyo gharama isingeongezeka, at least ingebaki pale pale (kwa kigezo hiki)
3. Uhakiki wa madeni ya walimu ulishika hatamu, kusinhekuwa na ongezeko maana hakuna madeni ya walimu yaliyokuwa yanalipwa.
4. Kulikuwa na watu walioonekana kumiliki vyeti feki. gharama ingeshuka maana umewapunguza wa vyeti feki
5. Kulikuwa na wafanyakazi hewa walioondolewa, hivyo kulitakiwa kuonekane kushuka kwa gharama za mishahara kwa vile wafanyakazi hewa hawakuwa wanalipwa tena....
6. Hakukuwa na ajira mpya, hii ingepelekea gharama kubaki pale pale maana hakuna mwajiliwa mpya

NB: tunazungumzia ajira mpya, si za kujaza nafasi ya aliyestaafu, aliyekufa, aliyeacha kazi, maana hawa hawaongezi gharama, bali wanagharimiwa kwa hela ya walioondoka kwa sababu yoyote ile...

Hayo yote umeona effect yake kwenye upandaji wa mishahara?

Hizo ajira na madaraja ni kipindi hiki cha uchaguzi... IN SHORT NI ZA KUOMBEA KURA TU...
 
Acha siasa za kishamba, kila mwaka serkali inaajiri
Pamoja na kuwa hunaga uwezo wa kujenga hoja, au pengine unakimbia hoja, ngoja nijaribu kukujibu.

Wewe na mtoa uzi wote mmesema "ukweli". Serikali ya magufuli inaajiri na pia haiajiri.

Zipo taratibu za ajira, ili kufidia ongezeko la mahitaji ya huduma, kufidia wanaostaafu, kuacha kazi, kufukuzwa kazi, au kufariki. Kwa miaka mingi hizo ndio zimekuwa taratibu za serikali .


Iliwahi kutokea serikali ikasitisha ajira huko nyuma. Matokeo yake mpaka hivi sasa kuna sekta nyingi zinaumia na kuligharimu taifa. Mfano katika mifumo ya vyuo vikuu, mhitimu anayefanya vizuri katika shahada ya kwanza, anaajiriwa kama Tutorial Assistant, TA. Baadae anapandishwa na kuwa Assistant Lecturer . Wakati huu anatakiwa kufanya shahada ya pili, na halafu ya tatu, PhD. Hapa atakuwa chini ya Profesa, ambaye atamwongoza. Hatimaye naye atapanda ngazi mbalimbali kadirivya uwezo wake. Sasa chuo kikiacha kuajiri maTA, huku maprofesa wakiendelea kuzeeka mpaka kustaafu, kutakuwa na "gap" kubwa sana, pale wakianza kuajiri TA tena. Hasara nyingine ya kuajiri watu wengi mara moja ili kujaza hizi "gap", matokeo yake hawa watastaafu wengi kwa mara moja, na tatizo litaendelea. Pia hakutakuwa na uhifadhi wa uzoefu na maarifa yaliyotengenezwa kwa gharama kubwa na kwa miaka mingi, kwa kuwa wafanyakazi " nguli" hawana wa kuwarithisha.

Ni kweli Magufuli anaajiri, lakini si katika utaratibu unaotakiwa kama nilivyotoa mifano hapo juu. Utaratibu wa sasa ni kutoajiri kwa kawaida, ila kwa mlipuko, baada ya miaka kadhaa. Kuna maelfu ya wahitimu wa ualimu, udaktari, nk. wapo mtaani. Ila utasikia wameajiriwa madaktari 1000, wakati wa dharura. Au JKT 70 wamehitimisha mafunzo kwa mbwembwe fulani, rais anafurahi na kuagiza waajiriwe wote! Hapo hakuna taratibu za Personnel management , bali hisia za rais.

Kichekesho kimetokea hapa karibuni. Lilitoka tangazo ka ajira kwenye vyuo kadhaa. Mchakato ukafanyika, wa interviews nk. Ghafla kila kitu kikawekwa kando, likatoka tangazo lingine. Kwamba wanaohitaji kuhamishwa toka serikalini kwenda kufanya kazi kwenye vyuo, wajotokeze! Huu ni mfano tu wa usanii wa serikalivya Magufuli. Maana hata kama kuna ziada ya wafanyakazi huko serikalini, ambapo sio rahisi pia, kuna njia tofauti za kushughulika na hiyo ishu.

Kwa hiyo ki uhalisia, serikali ya Magufuli haiajiri, na hili ni bomu litakalo tuvuruga kwa miaka mingi ijayo, na nina uhakika magufuli hana habari na hili tatizo. Hata akiambiwa, hana uwezo wa kulielewa. Anaweza kuelewa kilomita ngapi za barabara, makalveti mangapi, madaraja mangapi, basi. Hata wewe mpambe wake sina hakika Kama utaelewa ishu subtle kama hizi
 
Unakataa kwa kigezo gani mkuu? Watu wamepandishwa madaraja wengi tuu na Hilo ni zoezi endelevu
Nawafahamu kadhaa waliopandishwa madaraja. Ila waliolipwa stahiki za madaraja yao ni wachache saaana. Wengi wanaarifiwa utalipwa kuanzia tarehe fulani, halafu zinafuata danadana nyiiingi za kuahirishwa kila mara. Usanii wa aina hii haujawahi kutokea
 
Huu ni muendelezo wa kutoa habari kuhusu utafiti wangu wa kitaalamu huhusu namba za serikali ambazo zinapatikana Wizara ya Fedha, kwenye report ya serikali ya kila mwaka.

Ni muunganiko wa nyuzi ambazo nimekuwa nikizotoa na kuzipa jina 'Namba zinanuka'

. ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii
. ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

Leo nitauliza tu swali la kichokozi baada ya kupitia Wage Bill ya Serikali kuanzia mwaka wa fedha 2016 mpaka 2019.

Nilichogundua ni kwamba, wage bill inakuwa kubwa siku hadi siku, haiakisi kitendo cha serikali kutimua wafanyakazi hewa maelfu na kitendo cha kutokuongeza mishaara kwa watumishi wa umma.

Ki nadharia, kitendo cha kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, pamoja na kutoongeza mishaara kungetosha kabisa kuwa kunapunguza wage bill ya serikali. Sasa tunavyoona serikali imefanya hayo yote na bado tunaona wage bill inaongezeka, lazima tuhoji, Je, nini kinasababisha hii wage bill kupanda mwaka hadi mwaka?

View attachment 1490972

Year
2016​
2017​
2018​
2019​
Wages, salaries, and employee benefits in Tzs '0008,783,734,5218,652,125,85710,129,046,51810,927,828,010
% changeN/A
-1.50%​
17.07%​
7.89%​

Ukiangalia kwa makini hiyo chart hapo juu, utagundua kwamba, kutoka mwaka wa fedha wa 2018 mpaka 2019, wage bill ime shoot kwa takribani asilimia 24.96% (Kutoka Trillioni 8.6 mwaka wa fedha 2017, mpaka Trillioni 10.9 mwaka wa fedha 2019)

Unakaa ukijiuliza, je sababu haswa ya serikali kutokuongeza watumishi mishahara ilikuwa ni ipi, kama bado wage bill inaendelea kupanda mwaka hadi mwaka?

Kwa nnavyoona inawezekana kuna mismanagement fulani ambayo mimi na wewe hatuijui, labda serikali siku moja watoke kidedea kutujibu hili swali la ni kwanini pamoja na hatua zote za 1) Kuondoa wafanyakazi hewa, 2) Kutumbua wenye vyeti feki, 3) Kustopisha kuajiri kwa miaka zaidi ya mitatu, 4) Kustisha ongezeko la mishaara kwa watumishi wa serikali, lakini bado wameshindwa kudhibiti ongezeko kubwa la wage bill ambalo linaonekana wazi kwenye namba za serikali na kwenye report za kibajeti.

Kuna nini haswa kinaendelea? Au ndo ule usemi wa wataisoma namba unatimia?


Uzi Tayar.

N. Mushi
Tatizo mnakuwa na majibu yenu Tayari!
 
Nawafahamu kadhaa waliopandishwa madaraja. Ila waliolipwa stahiki za madaraja yao ni wachache saaana. Wengi wanaarifiwa utalipwa kuanzia tarehe fulani, halafu zinafuata danadana nyiiingi za kuahirishwa kila mara. Usanii wa aina hii haujawahi kutokea
Lete number kumaliza utata wa idada ya waliopata stahiki mwaka baada ya mwaka mkuu, kusema tuu kwamba ni wachache inawezekana ukawa sahihi au usiwe sahihi. Waliotoa hizo data lazima wana number sahihi
 
Back
Top Bottom