Swali la kizalendo: Mabeberu ni kina nani?

Swali la kizalendo: Mabeberu ni kina nani?

Dunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!

Wakati wa vita baridi neno Mabeberu lilitumika sana hapa Tanzania. Enzi zile beberu alikuwa ni mtu yoyote asiye mjamaa, mpinga mapinduzi, anayeamini katika soko huria na uliberali..
Mabeberu in wale wanaowakopesha ccm ambao huwaita wahisani
 
Mabeberu ni neno linatumiwa na wanasiasa ili kulaghai wananchi ambao uelewa wao wa dunia ni mdogo. Wanasiasa wanao tumia neno wanasema kwa midomo tu ila mioyoni mwao wanajua kwamba siyo kweli.
 
Dunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!

Wakati wa vita baridi neno Mabeberu lilitumika sana hapa Tanzania. Enzi zile beberu alikuwa ni mtu yoyote asiye mjamaa, mpinga mapinduzi, anayeamini katika soko huria na uliberali...
Beberu ni mtu yeyote anayetaka kukupa msaada au huduma kwa njia ya kukudhalilisha, anayetaka kuchukua uhuru wako, kwa kutumia nguvu zake au uwezo wake kifedha nk,

jina beberu linatumika kwa mfano wa mbuzi dume ambae hupenda kumtolea sauti nzito shingoni mwa mbuzi jike hasa pale anapotaka kufanya mapenzi na mbuzi jike.

Hivyo huonyesha kama anamkoromea mbuzi jike. Sasa mabeberu wa kizungu hupenda kutaka kutukoromea sisi waafrica na kutumia misaad yao kutunyanyasa na kutupangia wanachotaka wao hata kama ni cha kudhalilisha.
 
Ubeberu ni hatua ya juu ya Ukoloni(imperialism), ambapo nchi tajiri zinaendelea kuzinyonya nchi maskini kwa njia ya uchukuaji wa rasilimali na pia misaada na mikopo yenye masharti magumu.
La mkuu umekariri! Hivi bado mnafundishwa hii Definition hata leo!
 
Beberu ni mtu yeyote anayetaka kukupa msaada au huduma kwa njia ya kukudhalilisha, anayetaka kuchukua uhuru wako, kwa kutumia nguvu zake au uwezo wake kifedha nk,

jina beberu linatumika kwa mfano wa mbuzi dume ambae hupenda kumtolea sauti nzito shingoni mwa mbuzi jike hasa pale anapotaka kufanya mapenzi na mbuzi jike
Hivyo huonyesha kama anamkoromea mbuzi jike.
Sasa mabeberu wa kizungu hupenda kutaka kutukoromea sisi waafrica na kutumia misaad yao kutunyanyasa na kutupangia wanachotaka wao hata kama ni cha kudhalilisha.
Mfano mmoja ni ushoga.
Vipi kuhusu Wachina!
 
Ubeberu ni hatua ya juu ya Ukoloni(imperialism), ambapo nchi tajiri zinaendelea kuzinyonya nchi maskini kwa njia ya uchukuaji wa rasilimali na pia misaada na mikopo yenye masharti magumu.

Je hapa kwetu tunamaanisha nini ? Na mataifa gani tunapaswa kuyaita Mabeberu sisi watanzania?
 
Hivi Leo hii nchi yetu bado inaweza kusimama kifua mbele na kusema sisi ninnchi ya Kijamaa!
Mbona ujamaa ulifia Zanzibar ...Azimio la Zanzibar(ambalo halina andiko) Pale Mwinyi aalipisema ..Tumelizimua Azzimio la Arusha!?
Ukweli tuo kwenye mtanzuka wa Kisera,tunafuata misingi ya Uliberali lakini,tunataka tuchanganye na Ujamaa!
Kama tunafuata Uliberali tukubali na misingi yake ..amabayo Ni Uhuru wa.mawazo kinzani,na Haki za Binadamu!
Kinyume chake tutakuwa tunarudi nyuma!
Na Kama tunataka Ujamaa Basi tuwe wajamaa wa ukweli...Kama alivyaamini na kuishi amwalimu Nyerere!
 
Dunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!

Wakati wa vita baridi neno Mabeberu lilitumika sana hapa Tanzania. Enzi zile beberu alikuwa ni mtu yoyote asiye mjamaa, mpinga mapinduzi, anayeamini katika soko huria na uliberali...
Beberu anaweza kuhasiwa na akawa si beberu tena bali ndafu! Anakuwa haruki ruki anakuwa ametulia. Hivyo basi leo nchi fulani inaweza kuwa beberu kesho ikawa si beberu
 
Profesa Shivji na Bashiru Ally(Yule wa.wakati ule..😩lakini huyuhuyu wa leo) waliwahi kuandika Kijitabu ..KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA!
Ni Kitabu Kizuri kisomwe...Ila Bashiru Ally mhh....Zilongwa mbali,zitendwa mbali!
 
Beberu anaweza kuhasiwa na akawa si beberu tena bali ndafu! Anakuwa haruki ruki anakuwa ametulia. Hivyo basi leo nchi fulani inaweza kuwa beberu kesho ikawa si beberu
Kwa hiyo sisi Sera zetu ni Kuhasi Màbeberu ...ili waendane na tunachotaka!?
 
Mchina hana mda wa masharti yeye akupe pesa ule usile yeye anachotaka ulipe riba yake na mkopo basi ila mambo yako na nchi yako hayamuhusu.
Mchina haingilii Mambo ya ndani lakini ana masharti magumu na lazima pesa yake irudi, rejea mtafaruku wa Sri Lanka na hapa kwetu Bandari ya Bagamoyo
 
“Name calling a k a verbal abuse is the lowest form of intellectual discourse”. Wikipedia.
 
Ubeberu ni hatua ya juu ya Ukoloni(imperialism), ambapo nchi tajiri zinaendelea kuzinyonya nchi maskini kwa njia ya uchukuaji wa rasilimali na pia misaada na mikopo yenye masharti magumu.
Magufuli kachakopa 40T toka kwa beberu,Ila yeye hajatumwa na beberu bali anapigania raslimali zetu kwa kukopa toka kwa beberu,kwa hiyo mkuu nakuomba sana hilo neno mikopo litoe kwenye hii post,lina harufu ya uchochezi
 
Back
Top Bottom