Wanajamvi heri ya mwaka mpya 2026.
Baada ya kunywa Balimi zangu kadhaa, nimejiuliza, hivi URAISI una nini hasa kuwafanya watu (Maraisi) wawahi kuzeeka kwa kasi ya kutisha?
Je, ni majukumu mazito ya kuelemea mtu kiasi gani kumfanya mtu (Raisi) azeeke kwa haraka? . Uraisi una siri gani mpaka mtu azeeke chap chap kwa kasi ya ajabu?
Mfano; Jakaya 2005 tu hapo, tuliimba sana nchi imepata raisi kijana " handsome boy" na ni kweli alikuwa "handsome" kweli JK, yaani alikuwa "yankii" mtu flani hivi "blazameni" wa kuajiri "firm" kumvisha, kumpamba na kumbunia mavazi n.k. Mtu flani wa kula bata, kukwea pipa mamtoni mara mbili au mara tatu kwa mwezi haikuwa ishu kubwa kwa JK. Mtu flani hakutaka shida na mtu, ukimsumbua anakuita mezani anakuwekea shilingi mezani, unakuuliza shida nini kijana? Kwanini unasumbua wazee. 😊
Ni enzi za JK, wapinzani walikuwa wanaitwa ikulu pale. Anyway sio mada hiyo, lakini Mzee hakupenda kumkwaza mtu, zaidi zaidi alipenda diplomasia kutatua mambo yake au ku deal na watu/vitu vilivyokuwa vina mzonga.
Ajabu kampeni za mwaka 2010, JK akapoteza nuru kwa kasi usoni, kwa muda miaka 5 tuu madarakani ule ujana "uhendisamu" wa JK ukaisha na akaonekama Mzee wa wazi kabisa. Ukichukua bango za JK za 2005 na 2010, utaona tofauti kubwa sana.
Tuje kwa Hayati Magufuli, ukimtazama Magu 2015 na 2020 utaona kasi ta ajabu sana ya upara, na mvi nyingi kidevuni, akaamua aanze kunyoa kabisa ndevu zile na upara mkali. Hii ni kwa kasi ya miaka mitano tuu, mtu anabadirika kwa kasi kukimbilia uzee huku akiwa raisi, kazi ambayo ina kila aina ya usaidizi, utaalamu na starehe. Sawa wanasema "Mshua" alikuwa anaumwa lakini inaleta ukakasi kwa kasi ile. Kama Jiwe angetoboa 2025 basi angekuwa kachoka sio kidogo.
Mwinyi Jr, wazee hamjaona kama Mwinyi Jr, anazeeka chap chap? Juzi kati tuu hapo anampokea Dr. Shein 2020 alikuwa "yanki" tuu Mwinyi. Dizaini Mwinyi kama ameanza kupata makunyanzi hivi, fuatilieni vizuri. Na Mwinyi ana bahati Zanzibar kumetulia sio kama enzi zile za CUF na Maalim Seif ni vijana. Hakuna rangi mwinyi angeacha kuiona hapo Zanzibar. Zanzibar ya leo imetulia, hakuna purukushani zile za 2000 mpaka 2015.
Nje ya Tanzania; Mtazame Uhuru Kenyatta, sio muda Uhunye anaweza kuanza kutembelea Mkongojo kama baba yake. Angalia Obama, alivyoingia, miaka minne tuu mvi hizoo. Joe Biden yeye ndo "akarusha taulo" miaka minne tuu tayari anasahau speech. 😁
Tuje kwa Bimkubwa 😊. Linganisheni bimkubwa akiwa "Makamo" juzi tuu hapo, halafu angalieni alipokuwa raisi kamili, njoo kampeni zake za Oktoba. Mgizame vizuri bada ya Oktoba, angalia juzi akilihutubia taifa.
Bimkubwa anatepeta kwa kasi tuache utani. Sasa 2030 sijui atakuwaje mama wa watu jameni. Bimkubwa shavu linashuka kwa kasi ya SGR na ndio kwanza asubuhi. Ikifika 2028 huko sijui itakuwaje.
SWALI LANGU LA KIZUSHI: Nini hasa kipo nyuma ya majukumu ya Uraisi na Kuwahi kuzeeka "Kuchoka" mwili? Nini kipo nyuma ya pazia?