Swali la kizushi - Je Pesa za TFF zinazodaiwa kupigwa na Malinzi ni Mali ya Umma ?

Kwani fedha za ndama mtoto ya ng'ombe zilikua ni za umma.. Mbona amefikishwa mahakamani
 
Hazina, ukiuliza kwa Mzee Makamba unaonyeshwa
Hazina iko mkoa gani? Me pia niliona video somewhere katibu wa tff alienda kumtembelea captain kama wiki moja hvi iliyopita usibishe.
 
Nadhani unapaswa kwanza kujua nini maana ya "uma"

Serikali kutoingilia masuala ya soka... je wizi ni suala la soka?

Uhalifu ni uhalifu tu. Au kwamfano Malinzi angefanya mauaji angeachwa kwakuwa FIFA imekataza serikali kutoingilia masuala ya soka?
Asprin mbona unakurupuka sana, mifano yako ni hovyo sana. Kuua sio kazi ya FIFA au umechangia tu kuonekana upo?
 
Kwa uelewa wangu mdogo, hize hela sio za umma na wala serikali haina mamlaka ya kuingilia na kuwakamata viongozi wa TFF. Naongezea maswali mawili ya kizushi;-
1. Alieshtaki nani takukuru?
2. Ukaguzi wanoutumia takukuru alifanya nani na kwa niaba ya nani?
Angalizo, wasijione wana meno, basi wakayatumia hata kung'ata chuma!!!
 
mkuu, mimi naona depending on legal interpretation, hii issue inaweza kusababisha Tz kufungiwa kwani masuala ya football (be it technical or administrative) hayatakiwi kupelekwa mahakamani.

mkuu Petro E. Mselewa unasemaje?
 
Asante kwa hoja yako, naomba ufafanuzi huu. Hela za wadhamini wa ndani sawa, hao wadhamini waliletwa na serikali? Je umewahi kusikia wadhamini wakaingilia matumizi yako? Au wadhamini mipaka yao ni ipi? Maana tusichanganyane hapo. Urudi mapema ili tujue Takukuru haki yao iko wapi?
 
Swala tu sio kuwa pesa za Umma, hata mtu binafsi pesa zake zikitumika visivyo mf kuibiwa nk, polisi wataingia kazini na baadaye mahakama. Pesa za TFF ziwe za umma au zisiwe ili mradi kuna kosa limefanyika lazima washughulikiwe. Haya mambo ya kuanza kuhoji kama pesa ni ya umma au la yametoka wapi? Kosa ni kosa!
 
Malinzi alikuwa hafai tena kuongoza tff kwa sababu amefanya blunders kibao, sasa ilikuwa ni kumsubiri kwenye muda mwafaka ili kuzuia mbio zake za kwenda tena tff, kesi yake atapata dhamana na anaweza kushinda ila si kabla ya uchaguzi wa tff! hahahah bongo tambaraleee
 
mkuu, mimi naona depending on legal interpretation, hii issue inaweza kusababisha Tz kufungiwa kwani masuala ya football (be it technical or administrative) hayatakiwi kupelekwa mahakamani.

mkuu Petro E. Mselewa unasemaje?
Mkuu,ukipitia makosa ya akina Malinzi utaona bayana kuwa yote ni makosa ya jinai. Makosa ya jinai ni makosa binafsi na si ya kitaasisi. FIFA hukataza kuingilia mambo ya kisoka kama uchaguzi,uteuzi wa timu ya taifa na kadhalika. Si jinai. Kwa jinai,hata Messi,Neymar na viongozi waandamizi wa FIFA walifikishwa mahakama za kawaida za kinchi.
 
mkuu, mimi naona depending on legal interpretation, hii issue inaweza kusababisha Tz kufungiwa kwani masuala ya football (be it technical or administrative) hayatakiwi kupelekwa mahakamani.

mkuu Petro E. Mselewa unasemaje?
Tunavyoongea sasa hv C Ronaldo ana kesi huko ya kukwepa kodi kutoka kwenye mshahara wa ke, Blatter (Aliekuwa bosi wa FIFA) nae kesi iliyomkabili kipindi kilichopita ilishughulikiwa na FBI.... Ila kwa taarifa yako kesi za soka kwa makosa yasiyokuwa ya kijinai hazipaswi kupelekwa mahakamani, lkn taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa ndio pekee zilizokubaliwa na FIFA kuingilia wakati wowote wanapoona kuna kitu hakijakaa vizuri (kumbuka aliekuwa bosi wa FIFA) Mr Blatter nae alikaangwa alipotumia vby ofisi..... Hakuna mahsli ambapo fifa wameandika au kutaka kuwa mtu hata akitenda jinai asishughulikiwe eti sheria za fifa haziruhusu. TFF haijapelekwa mahakamani, aliepelekwa ni Malinzi na Mwesigwa hizo ni kesi binafsi sio taasisi. Hata wewe na wenzako mkianzisha vicoba huko mtaani ili mradi mkaisajili, akatokea mtu akajinufaisha kwa maslahi binafsi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hakuna atakae hoji ni za umma au sio umma.
 

Mkuu kwanza kabisa, neno 'umma'.

Kwenye kamusi ya kiswahili neno hili

Umma = Wananchi wote kwa ujumla. Sehemu nyingine wametafsiri umma ni jamii ya watu wanaoishi pamoja na kuwa na historia moja.
Kwa wenzetu Islam, 'umma' ni jamii ya watu wenye imani moja na kumuabudu Mola wao kwa pamoja.
......

Sasa TFF ni mali ya mtu binafsi? Hapana, ni taasisi inayosimamia soka la Tanzania. Watanzania zaidi ya mil 45 wanaitazama TFF. Pesa yyt iliyoko pale kwenye taasisi ni kwaajili ya hawa watanzania zaidi ya mil45.

Isitoshe TFF kuwa na utaratibu wa kujitawala hakuiondoi kuwa chini ya Baraza la Michezo Tanzania ambalo linawajibika chini ya Wizara husika ktk maswala ya michezo. Sasa ukifuatilia sana utagunduapesa ya TFF ni pesa ya umma. Hata isingekuwa ya umma yale ni makosa binafsi ambayo yanawahusu watuhumiwa binafsi na sio taasisi (TFF)
 
TFF ni Mali ya umma chochote kinachoingizwa na kumilikiwa na TFF ni Mali ya umma.
 

Sawa mkuu nakuelewa vizuri sana, ila usichukie na wala usichoke kurudi tena. Swali langu ni hili, umesema ni makosa binafsi wameyafanya Malinzi na Mwesiga, je wameyafanya wakiwa kwenye nyadhifa zao au?

Na kam wameyafanya wakiwa madarakani, Je ni nani alienda kuwashitaki takukuru? Na takukuru ushahidi wao atauleta nani mahakamani?

Maana sitaki kwenda mbali sana. Hii kesi ndani yake inautakatishaji fedha, sielewi vizuri hii money rounderin inakaaje, ila kwa uelewa mdogo ni kuzichukua hela halamu ukazifanya kuwa halali

mfn: ndio ule wa madawa ya kulevya kupata hela, kuziingiza bank nakuzitoa tena, hapo umezitakatisha. Sasa basi hao akina Malinzi mametakatishaje? Rudi mkuu, tafadhali. Kuna maswali mengi yasio na majibu.
 
Nadhani unapaswa kwanza kujua nini maana ya "uma"

Serikali kutoingilia masuala ya soka... je wizi ni suala la soka?

Uhalifu ni uhalifu tu. Au kwamfano Malinzi angefanya mauaji angeachwa kwakuwa FIFA imekataza serikali kutoingilia masuala ya soka?
Brilliant Asprin. Mwizi na rushwa ni makosa ya jinai. Sett Blatter mwenyewe ilibidi asalimu amri
 
Fifa walimchangia Malinzi na Cargo Star au Tanzania Football Federation?
 
Kama Malinzi ni clean anahangaika nini na TFF? Kampuni ya Cargo Star imeishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…