Swali la kizushi - Je Pesa za TFF zinazodaiwa kupigwa na Malinzi ni Mali ya Umma ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nimeuliza makusudi ili nipate ufafanuzi .

Kuna fungu lolote kutoka serikalini linatengwa na kuingizwa kwenye akaunti ya TFF ? Nakumbuka wakati wa FAT ya Muhidin Ndolanga , FIFA ilipiga Marufuku kwa serikali kuingilia masuala ya soka , sasa siku hizi FIFA wamebadili msimamo wao ?

Je hela zile ni za Umma ama ni mchango wa FIFA kwa TFF ?

.....................................................
UPDATES
FIFA yaingilia kati , ambapo imetuma ujumbe kuja kufuatilia sakata hilo , inatarajiwa Jumanne ijayo kutafanyika kikao kati ya wajumbe wa FIFA na viongozi wa TFF walionusurika .
 
Nadhani unapaswa kwanza kujua nini maana ya "uma"

Serikali kutoingilia masuala ya soka... je wizi ni suala la soka?

Uhalifu ni uhalifu tu. Au kwamfano Malinzi angefanya mauaji angeachwa kwakuwa FIFA imekataza serikali kutoingilia masuala ya soka?
 
Fedha za Fifa hazihusiki, kinachohusika ni fedha za mikataba ya ndani TBL, Serengeti na nyinginezo. Malinzi kafoji risiti za kujilipa dola laki nne kutoka TFF akidai anaidai, jiulize kwa kazi ipi? Fedha za Udhamini wa TBL na serengeti katombea zote kawanyonga wale watoto kawapa nauli tu. Takukuru ni chombo huru kinachunguza popote penye rushwa na uwizi kama ilivyokuwa kule Fifa kwa Blatter hazikuchunguzwa fedha zao kilichunguzwa ni rushwa ya maamuzi.
NB.
Fedha zinazotuhumiwa kutafunwa na Malinzi si za Fifa ni za mikataba ya ndani pamoja na kutakatisha fedha.
 
Ahsante kaka mkubwa[emoji120] [emoji120]
 
Kumbe mkuu ndio hivyo??
 
Klabu ya Simba imesajiliwa kwa mujibu wa sheria hivyo maofisa wake ni watumishi wa umma (wanachama, wapenzi na mashabiki wa mikia fc) hivyo maofisa hao wanayo dhamana ya kuzitumia mali za klabu kwa malengo yaliyokusudiwa.

Maofisa hao wakiingia kwenye mtego wa kuzitafuna fedha za klabu wanakuwa wametumia ofisi ya umma kwa manufaa binafsi ambapo fasili yake ni RUSHWA. Kwa kuwa wazee wa kazi hiyo wapo, hawana budi kuamsha madude.

Chekecheo, chekecha, watumishi wabovu!!!!
 
Swali zuri hasa ukizingatia jinsi hela ya Escrow ilivyogawanywa kwa kisingizio sio za umma. Nchi za kiafrika zikiamua kumshughulikia mtu ni balaa.
 
Klabu ya Simba imesajiliwa kwa mujibu wa sheria hivyo maofisa wake ni watumishi wa umma (wanachama, wapenzi na mashabiki wa mikia fc) hivyo maofisa hao wanayo dhamana ya kuzitumia mali za klabu kwa malengo yaliyokusudiwa.

Maofisa hao wakiingia kwenye mtego wa kuzitafuna fedha za klabu wanakuwa wametumia ofisi ya umma kwa manufaa binafsi ambapo fasili yake ni RUSHWA. Kwa kuwa wazee wa kazi hiyo wapo, hawana budi kuamsha madude.

Chekecheo, chekecha, watumishi wabovu!!!!
Kwahiyo wachezaji wa simba ni watumishi wa umma? Wakishikilia nyasi za simba wakitaka kodi saizi muda wa usajili wachezaji wanapewa mamilioni ivi wanajua hela inatoka wapi
 
mnamuona malinzi tu je maney loundering ya simba ni za uma? mwizi ni mwizi na wakiachwa serikali itaonekana ya ovyo takukuru kamata wote Hans Pop alishaonjeshwa bado MO na yeye. ajiandae
 
Fedha za Fifa hazihusiki, kinachohusika ni fedha za mikataba ya ndani TBL, Serengeti na nyinginezo. Malinzi kafoji risiti za kujilipa dola laki nne kutoka TFF akidai anaidai, jiulize kwa kazi ipi? Fedha za Udhamini wa TBL na serengeti katombea zote kawanyonga wale watoto kawapa nauli tu. Takukuru ni chombo huru kinachunguza popote penye rushwa na uwizi kama ilivyokuwa kule Fifa kwa Blatter hazikuchunguzwa fedha zao kilichunguzwa ni rushwa ya maamuzi.
NB.
Fedha zinazotuhumiwa kutafunwa na Malinzi si za Fifa ni za mikataba ya ndani pamoja na kutakatisha fedha.
Kuna watu waajabu sana hivi unajitokeza kutetea mtu kama Malinzi!. Kila nikimfikiria yule Nahodha wa Serengeti Boys aliyetelekezwa napata hasira sana na hao watu!
 
Back
Top Bottom