Moja kwa moja kwenye mada husika
Mimi nilichogundua hii jamii forum ya sasa siyo ile niliyokuwa ninaijua kipindi ilipoanzishwa. Nina uhakika mada fikilishi, mada makini zingepata machangio/reactions lukuki na hoja mbadala za kupinga au kusupport hoja. Nakwambia kwenye mada fikilishi zilikua zinatolewa references , analytical comparisons na tafsida na correlation, uhakika zilikua zinatolewa mifano pingamizi au supporting kuhusu hoja zote makini, hoja fikilishi zilizokuwa kwenye motion.
Cha kushangaza, kwa jamii (community) ya jamii forum ya sasa, ukitaka watu wachangie mada yako, toa mada/topics pendwa, toa mada za mapenzi, toa mada za mipira, toa mada rahini za chadema au CCM, Toa mada ya machawa, toa mada za Simba na Yanga. Tena ukitaka zaidi toa mada za kuongelea matukio ya juzijuzi kama kifo cha Dida, Diamond kuachana na Zuchu, yaani mada pendwa mada rahini. mada za mitaani , mada za vijiwe vya kahawa.Itabidi uelewe kwamba mada za uchawi, ulonzi na mambo ya giza giza kama freemanson, mada za kupididdypiddiana ndizo zitakupa wachangiaji lukuki.
Nakwambia ukitaka chapisho/andiko/mada yako ibaki tupu miezi miwili bila kuchangiwa tafuta mada ya kufikilisha, mada inayohusu siasa za ndani za nchi yetu, maamuzi mabaya na mazito yonayohatarisha hatma ya uchumi na usalama wa nchi yetu. Nakuhakikishia hutapata mchangiaji hata mmoja, na sio kwamba hawasomi, wanasoma na kupita tu.
Mimi nimekwisha kujaribu kutoa mada pendwa zimepata wachangiaji mpaka nikashangaa, lakini nilipotaka kutumia ubongo wangu, elimu yangu, huzoefu wangu nchini na nchi zingine kutoa mada fikilishi . Nakuhakikishia sikupata comment hata moja kusupport au kupinga au kuongezea kwenye hoja.Hapo ndipo nikagundua kuna tatizo kubwa ndani ya wanajamii wa jamii forum yetu ya sasa. Inawezekana mimi ndiye niliyepitwa na wakati.
Nakwambia ukitaka husipate mchangiaji hata mmoja, Nenda mbali kwa kutoa mada fikilishi, mada inayomuhitaji msomaji atumie ubongo kuelewa complex narration yako. Mada inyomtaka msomaji kucorrelate variables na issues mbalimbali na kuzilink together.
Kwa mfano nimesoma mada fikilishi nzuri ya bwana Synthesizer isemayo "Hivi, inahitaji akili kubwa kiasi gani kuelewa kwamba kwa kuwa Zanzibar wana serikali na raisi wao, raisi wa Tanzania, kimsingi, ni raisi wa bara?". Mada hii imehusisha watanzania kutoandaa wosia kama mfano rejea na kutotambua kuna siku rais aliyetoka bara anaweza kufariki na akachukua nchi makamu wake kutoka visiwani Zanzibar.Hapa nakuhakikishia hupati wachangiaji kamwe. Nimecheki hakupata changi lolote ingawa topic yake ni fikilishi na mifano yake inamake a lot of sense positively and negatively.
Suala la kujiuliza sasa ni je hawa wanajamii forum wa sasa ndio walewale wa zamani? kama ndio wale wale ni shetani gani wa woga amewaingia na kuathili mbongo zao?, je kimeingia kizazi dhaifu chenye critical thinking pungufu au kizazi kilicho na analytical capabilities tofauti. Au kuna onyo magwiji wetu wamepewa au kuchukuliwa na wasiojulikana ili kutisha wachangiaji mahili wengine au watoa mada mahili? Moderators na wanaforum wa Zamani mnaweza kutupatia majibu? WHAT EXACTLY HAPPENED, THE OBSERVED CONTROVERSY CAN NOT HAPPEN BY CHANCE.