Swali la Kizushi; WanajamiiForums wa sasa mbona hatuchangii mada fikirishi/Mada ngumu na tu Wepesi Kuchangia Mapenzi, Mipira, Uchawi na ushirikina

πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hyo Jerusalem mkuu unayoisubiri inatokea Kwa wap mkuu nije tujitege wt itupitieee
 
Huenda ni kwa vile hata uwe serious vipi mambo Bado yako vile vile. Yaani Hovyo hovyo, vululu vululu...
😁😁😁😁kiongozi anatamka wazi kuwa yeye ni chura kiziwi ...sasa hapo kuna nini tena ?
 
Je hawa wana JF wa sasa ndiyo wale wale wa zamani? Jbu ni hapana. Zamani wana JF wengi walikuwa watu wenye elimu, watu wa maofisini na walioko nje ya nchi kwa sababu siyo ''kila mtu'' alikuwa na access na Internet kipindi hicho. Tulikuwa tunajadili mambo ya nchi na viongozi wengi walikuwa wanachama japo walikuwa wanatumia majina bandia. Baada ya smartphone kuwa affordable na ''kila mtu'' kujua social media. JF imevamiwa na wajinga wengi. Wale wa zamani wengi wamekimbia baada ya kuona hizi mada za kijinga na kitoto.
 
Zamani wapuuzi walikua wachache ,hivyo ilikua ukiweka mada ya kipuuzi utaona watu wameiyangalia kisha wamepita bila ya kukoment.
Sasa hivi Jf imekua na watumiaji wengi na wapuu wameongezeka,kwahiyo ukiweka Mada ya kipuuzi inapata wachangiaji.
 
Mimi binafsi uwezo wangu wa kufikiri ni mdogo kwa hiyo sioni sababu ya kuchangia hizo maada ngumu ngumu, ata darasani kwenye mtihani maswali magumu nilikuwa sihangaiki nayo
 
Tumeona hakuna jipya....hivyo tumechagua kutojiumiza kichwa
 
Mada za malavidavi na mpira zimetalawa sana na Zina wadau kibao

That's why nchi hii kuitawala ni simple sana
 
Aksante sana Bro kwa jibu lako makini na analysis iliyotulia. Nakubalia na wewe asilimia 100% Nafikiri suala muhimu ni je tufanye nini kurudisha yale magwiji na kupunguza utoporo
 
Mada fikirishi hazipo tena na zikipostiwa zinafutwa chap,

Post nyingi zakitoto, ukifungua unakutana na trending threads za ajabu ajabu unatoka ukirudi unakutana nazo tena basi isiwe case unafungua Quora au Reddit.
 
Mtoa mada ungejaribu kutoa hoja fikirishi kama usemavyo kisha uone watu watakavyo changia.

Hakuna mada fikirishi unadhani watu watachangiaje
 
Mimi binafsi uwezo wangu wa kufikiri ni mdogo kwa hiyo sioni sababu ya kuchangia hizo maada ngumu ngumu, ata darasani kwenye mtihani maswali magumu nilikuwa sihangaiki nayo
Sawa kabisa na hilo ni jibu sahihi kama kweli uko honest
 
Mtoa mada ungejaribu kutoa hoja fikirishi kama usemavyo kisha uone watu watakavyo changia.

Hakuna mada fikirishi unadhani watu watachangiaje
Unaweza ukatrack hoja zangu zote nilizowahi kutoa humu, nyingi ni hoja pendwa na zimepata wachangiaji kibao. Angalia hoja ngumu moja, mpaka leo mwezi mzima hakuna mchangiaji hata mmoja, wakati hii tu within 30 minutes imepata wachangiaji zaidi ya 20
 
Unaweza ukatrack hoja zangu zote nilizowahi kutoa humu, nyingi ni hoja pendwa na zimepata wachangiaji kibao. Angalia hoja ngumu moja, mpaka leo mwezi mzima hakuna mchangiaji hata mmoja, wakati hii tu within 30 minutes imepata wachangiaji zaidi ya 20
Naungana nawewe pamoja na baadhi ya wachangiaji mada

Kwamba Siku hizi watu wameacha kuchangia mada nzito nzito Kwa kuogopa kutekwa n.k

Hii hali ilianza kushamiri mwanzoni mwa Mwaka 2016 imeendelea hadi leo hii

Kuna baadhi ya watu wa Serikali hawataki kukosolewa

Wamesahau kukosolewa kunaweza kufanya ufanye vizuri zaidi ukifanyia kazi hizo dosari

Wasiogope kujisahihisha, ndiyo maana Mwalimu Nyerere Mwaka 1995 aliandika Kitabu cha Tujisahihishe ili kuonesha Viongozi wasione dhambi kukosea na kujisahihisha
 
Akili zenyewe mbili tutachangia nini mkuu
Na hili ni jibu sahihi ingawa wengi watakubeza, unajua elimu yetu imeondoa kabisa eneo la kusharpen critical thinking yetu, angalia ufundishaji na maswali ya mitihani mpaka univerisity yanatest uwezo wa kuswallow na kuregurgitate materials. ufundishaji wa zamani mfano english na kiswahihi kwa mfano unasoma riwaya vitabu vikali, maswali yanakuhitaji ufanye overall analysis ya content za kitabu zinazohusiana au kikingana na mada ya swali ;nakumbuka issue ya conflict ilikuwa kubwa sana kwenye english literature. Hapa ulikuwa unakuwa tested critical thinking na how to make a case using examples from the narration. Sasa maswali hayo hayako, vijana hawasomi vitabu wanahand-out za summary ya vitabu na maswali. Wewe fikilia hesabu ni za kuchangua, ina maana ukiwa smart utafanya na kurudia mara 6 mpaka upate jibu;that is probability.....Kwa kweli hakuna ubishi kwa poor product of our graduants and students
 
Ndo maana pamoja na mapungufu yake ila kipindi cha kikwete kila kitu kilikuwa on fire Bunge lilikuwa nawatu wa kuoji sana, mahakama zilikuwa poa ndo maana ata ubunge ulikuwa unapigwa mahakamani nawatu wanatema ngoma CAG alikuwa anatoa Audit Queries na baadhi ya watu walio fanya madudu wanawajibishwa. Nikipindi pekee nikikuwa nawafahamu mawaziri na manaibu wao kwa Majina mpaka sura. Bunge nilikuwa namfahamu katibu wa bunge na wasaidizi wake mpaka wasaidizi wa spika kwa majina. Njoo kipindi hiki sasa yani sijui chochote kuhusu bunge wala ofisi ya CAG yani ni vulugu tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…