Swali la Leo: Ukiona watu wanakimbia huku wanalia

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Ukikutana na watu wanakimbia huku wanalia na wewe unajiunga nao huku unawauliza wanakimbia nini au unawasimamisha wasikimbie ili wakuambie kinachowakimbiza au unaendelea kwenda kule ambako wao wanakimbia ukaone kinachowakimbiza?
 
Mi ntabaki kuwatazama,maana kama nna safari zangu i've to accomplish it first
 
Najiunga nao huku nawauliza wanakimbia nini?
 
Inategemea mkimbio wao utakuwa nipi na kilio chao kikoje
 
Ukikutana na watu wanakimbia huku wanalia na wewe unajiunga nao huku unawauliza wanakimbia nini au unawasimamisha wasikimbie ili wakuambie kinachowakimbiza au unaendelea kwenda kule ambako wao wanakimbia ukaone kinachowakimbiza?

Unajiunga nao mnakimbia mengi utajua huku mwisho wa safari
 
Mimi nitakimbia kuwazidi halafu nitasimama kuwasubilia, wakifika nitawambia wasikimbie maaana nikikimbia hawatanikamata!

jamani tujaribu kuwa tunasoma thread vizuri ndo tuanze kupost comments zetu, ebu soma mara mbilimbili then i hope kuna kitu utakigundua anachomaanisha mwanakijiji.
 
napita tu
mapinduzi mema mmkj
 
Mzee, mi nakupa mji kitendawili chako kigumu, nipe jibu.
 
nitajiunga kukimbia huku nikiwauliza kulikon nikishajua nitaamua either niendelee kukimbia na kulia au niwaache na kuendelea na ishu zangu!
 
nikiwauliza hawatanijibu kwa sababu watakuwa wanalia sasa cha kufanya ni kubadili direction na mimi natimua
 
Sijui hili kama ni utani ama la!
Nasikia kabila la Wanyakyusa wa huko Mbeya huwa mwanamke akisikia msiba mahali anaanza kwa kulia na kugaragara kwanza, labda kwa nusu saa hivi, kisha uchungu ukimpungua ndiyo anatulia na kuuliza.."Aliyefariki ni nani?"

UKIENDA KWA WENYE CHONGO NAWE VUNJA LAKO JICHO!...lIia na waliao, kimbia na wakimbiao!
 
Swali wanalilia nini? lazima ujuwe kwanza....mana hata vichaa huwa wanalia.
 
Ntakimbia ile mbaya! Mfano mzuri ni mwindaji mahiri anapomkimbiza swala ghafla swala anakugeukia akuja mbio! Usimngoje! Ujue huko mbele kakurupushwa na mnyama mkali na anaemtisha kuliko wewe! Usidhani umepata kitoweo we nawe timka!
 
lazima ujue wanakimbia nini na nini kinawaliza.....
mengine.....ndo yatafuata
 
Kiubinadamu, mzuwie japo mmoja umwulize kulikoni, pengine ni kuna jambo ambalo ungewa kuwasaidia au angalau kuwafariji, pengine ni masuala ya kifamilia haykuhusu lakini utaondoka na nafsi yako haitokusuta baadae . Kiusalama hata wako wewe, pengine wanakimbia hatari, ukielewa na wewe utatafuta wapi pa kuelekea.

Tatizo ni kuwa siku hizi ulimwengu umeharibika. Ikiwa ni vijijini watu wanaelewana na hakuna tatizo hata ukikimbia nao, lakini mjini shule. Inawezekana hao watu wamekuwa wakikufuatilia kwa muda, wanajitia kukimbia, ukiwafuata na kufika wanapohisi hawaonekani wanakugezia kibao. Cha kufanya kwa usalama wako, sio ukimbie nao bali hakikisha kwanza pana watu wengine karibu na tukio ili iwapo ni mabzazi upate msaada.
 
kwa wabongo lazima uende ukachungulie ujue nini kinawaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…