Kiubinadamu, mzuwie japo mmoja umwulize kulikoni, pengine ni kuna jambo ambalo ungewa kuwasaidia au angalau kuwafariji, pengine ni masuala ya kifamilia haykuhusu lakini utaondoka na nafsi yako haitokusuta baadae . Kiusalama hata wako wewe, pengine wanakimbia hatari, ukielewa na wewe utatafuta wapi pa kuelekea.
Tatizo ni kuwa siku hizi ulimwengu umeharibika. Ikiwa ni vijijini watu wanaelewana na hakuna tatizo hata ukikimbia nao, lakini mjini shule. Inawezekana hao watu wamekuwa wakikufuatilia kwa muda, wanajitia kukimbia, ukiwafuata na kufika wanapohisi hawaonekani wanakugezia kibao. Cha kufanya kwa usalama wako, sio ukimbie nao bali hakikisha kwanza pana watu wengine karibu na tukio ili iwapo ni mabzazi upate msaada.