Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Swali la kijinga toka kwa mjinga. Kama hujui maana ya ujinga na mjinga, unaweza kunicheka kwa kuona au kudhani najitukana mwenyewe.
Lakini ukweli wa mambo ni kwamba ujinga si tusi. Binadamu wote wana ujinga.
Hakuna mtu ajuaye kila kitu.
Sasa basi, leo ngoja niulize.
Katika Tanzania yetu hii, ni nani mwenye mamlaka ya kuamua kuanzishwa mchakato wa kupata katiba mpya?
Ni wananchi wenyewe?
Ni wananchi kupitia wabunge?
Au ni Rais ambaye kwa Tanzania ni Mungu mtu aliye juu ya kila kitu, ikiwemo katiba yenyewe?
Nauliza hivyo kwa sababu sasa hivi Rais Samia anapewa shinikizo la kuanzisha tena mchakato wa katiba mpya.
Sasa mimi sielewi na sijui. Yeye Samia [rais] ndiye mwenye hayo mamlaka?
Kama yeye ndiye, hayo mamlaka yanatoka wapi?
Yameandikwa kwenye katiba? Sheria?
Au tunadhani tu kuwa yeye ndiye mwenye hayo mamlaka kwa sababu yeye ni Rais lakini kiukweli hayo mamlaka hana?
Kwa nini mchakato wa kupata katiba mpya ni mpaka yeye aridhie ilhali yeye ni mtumishi wa wananchi ambao ndiyo wenye nchi?
Wajuzi na wajuvi, naomba mnifute huu ujinga nilionao. Tafadhalini sana 🙏.