Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi.

Kama kawaida yangu, kila nikipata muda, nashuka na zile makala zangu elimishi za KMT - "Kwa Maslahi ya Taifa". Mada ya leo ni swali la kitu kinachoitwa "morality": "Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia?.

Na tukija kwenye medani za siasa, kabla ya kuusema ukweli wowote tunaousikia, je ni lazima tuseme tuu kila kitu tunachokisikia au kwanza, tutangulize mbele maslahi ya taifa kwa kujiuliza kwanza, hicho unachotaka kusema kina maslahi kwa taifa?, na unatakiwa kuupima kwanza huo ukweli kwa kujiuliza, je, ukweli huu ukijulikana una matokeo gani kwa taifa?, ndipo tuuseme, au tuendelee tuu na hii tabia ya kusema kila kitu unachokisikia?. Ukisikia jambo lolote, wewe liseme tuu bila kujali jambo hilo linamatokeo gani as long as jambo hilo ni la kweli?.

Na ili kupata manufaa ya kisiasa, je ni lazima wanasiasa wetu, wapoliticise kila kitu?, kila jambo? na kila tukio?.

Declaration of interest.
Mimi Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu ya kwanza ya mwana habari, (cardinal rule ni " tell nothing but the truth, no matter what!", lakini before telling the truth, mwandishi anatakiwa kutumia kitu kinachoitwa "objectivity test" yaani kuwa objective kwa kuupima ukweli huo una faida au manufaa gani kwa jamii, taifa na mhusika?.

Hivyo mimi as a journalist ni mtu mkweli daima, na ni muumini wa ile ahadi ya mwana TANU ya " Nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko", ila katika kuusema ukweli au kuandika ukweli, nasema na kuandika kwa kutumia kitu kinachoitwa responsible journalism kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kabla sijaandika, ninajiuliza kwanza, je ukweli huu ukisemwa, utajenga, au utabomoa?.

Ukisikia jambo, au ukiona jambo, japo ni ukweli lakini kama ukweli huo, ukijulikana, badala ya kujenga, utabomoa, then ukweli huo, siusemi. Huu ndio uzalendo wa kweli wa taifa lako kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Mfano mzuri ni kwenye issue ya JPM, kuna ukweli fulani niliowahi kuusikia kumhusu JPM, hivyo niliposikia anaweza kuja kuwa rais wa JMT, niliusema kwenye bandiko hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
Kwenye bandiko hilo kuna kitu nilisema nitakisema, mwisho wa siku, sikukisema!. Na baada ya JPM kuwa rais wa JMT, kuna siku nilikiulizia, Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko? nikakuta hakuna anayekijua. Kwa vile sasa tayari JPM ndie rais wetu, ukweli huo ninaoujua ukijulikana, hautasaidia kitu, sio tuu, haujengi bali unabomoa, hivyo siusemi kabisa, lakini ili kuzuia jambo kama hili lisijirudie in future, nilitoa ushauri Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu?
Sometimes ukweli too much unaponza!.
The Bitter Truth, The Bitter Reality. Kisa cha Kweli nilipomzwa kwa Kusema Kweli.
Mimi ni mtu kutoka makabila ya Kanda ya Ziwa, ambayo we are notorious with light skinned ladies!, nilifunga ndoa mapema nikiwa kijana just 25 years kwa kumuoa schoomate na classmate sweetheart wangu who was just 21 years!.

Ujana ni maji ya moto na una changamoto zake, hivyo nilioa nikiwa mtangazaji maarufu, navuta pesa za kutosha, fame utangazaji wa TV wakati huo bongo ndio kwanza TV zinaanza na ukijumlisha na Usukuma, life ya mwanzo ilikuwa kazi kidogo. Akatokea mdada mmoja aliyenizimikia na kunifia, kiukweli nakiri kukosa uvumilifu, nikashindwa kuvumilia, nikaanguka dhambini, sisi Wakatoliki ukifanya dhambi unaungama kwa padri, zambi zako zinaondolewa, maisha yanaendelea.

Hivyo katika kuamua kuwa mkweli kabisa, nikaamua kuusema ukweli kwa wife kuwa ni kweli, shetani allinipiti, akanidanganya, hivyo nili cheat mara moja tuu kwa kuchepuka!, nikiamini kwa vile I was her first, na ananipenda kweli na kwa kwa dhati, and and I'm the one and only man she knew, hivyo nikasema ukweli kwa hopes kuwa nitasamehewa, kwa sababu hapo tulipo tuko watoto kibao na wa mama kibao, hivyo ku cheat mara moja tuu na kwa mrembo kama yule, to me was not a very big deal, nikasema ukweli nikaomba msamaha, nikijua yatakwisha!, kumbe I realized, kusema ukweli, sometimes ni detrimental!, kunaponza, kumbe kule kusema kweli kwangu, ndio kukawa the beginning of an end!.

The point is japo ni ukweli, na ukweli ni lazima usemwe, ila kuna ukweli mwingine kabla hujausema, lazima upimwe, kwa kuusema ukweli, jee utajenga?. Kwetu sisi wanaume wa kiafrika, kuwa na extra marital affair is not a big deal, tume justfy kuwa its our nature, lakini sijui ni wanaume wangapi wako tayari kuupokea na kuubali ukweli kuwa hata wanawake wake za watu, they do it as well!, how many men are bold enough kuusikia ukweli huo na kuukubali?!.

Naomba kukiri, nimekuwa prompted kuandika uzi huu kufuatia mchango wa mwana jf huyu katika bandiko fulani.

Je tunadaiwa Canada au hatudaiwi? je Lisu amesema ukweli kuhusu vikao vya siri huko Canada au la? kwama yote ni ndio kwanini Umemkamata?.

Mkuu HTP, kanuni ya ukweli inasema "seek the truth" na ukiulizwa ndio "tell the truth". Sio lazima kuusema kila ukweli unaoujua, kama kuna ukweli fulani unaujua kuhusu jambo fulani, kama kwa kuusema utasaidia kitu au utajenga, then unaweza kuusema ukweli huo, lakini kama kuna ukweli unaujua na ukisema utabomoa, unaamua kukaa nao tuu bila kuusema! haswa kama ukweli huo ukisemwa, ama utakudhalilisha, ama hauna maslahi kwa taifa!.

Jee Kila Ukweli Ni Lazima Usemwe?. Some Truths are Better of or Best if Kept Silence!.
Mfano mimi na wewe ni marafiki, na ni family friends hadi wake zetu wanafahamiana. Mimi ndio nilikuwa Best man wako. Ndoa yenu ni miaka 5 sasa hamjajaaliwa kupata mtoto, huku wake na mawifi wakimsakama wife wako kuwa ni tasa/mgumba kazi yake ni kujaza tuu choo!. Kumbe tatizo sio mkeo, bali ni wewe una low sperm count.

Ikatokea niko safari, nikakutana na wife wako, akanitafuta kunielezea matatizo yako ya under performance, hivyo kila siku unamlaza na njaa mkeo. Tumekunywa pombe nazo zikatutuma yetu, nikakusaidia kum service wife wako!. Kutokana na good performance, wife wako akaniomba niwe nam service at least once a month!. Mimi kama rafiki mwema na best man, nikakubali kwa nia njema kabisa ya kusaidia, wakati tukitafuta suluhisho la kudumu la ndoa yenu kupata mtoto.

Naamua katika mazungumzo yangu kujifanya mimi ndio nina tatizo la under performance, hivyo nahitaji some medical help, ili na wewe useme yako, huku nikiendelea kumservise mkeo. Baada ya muda najifanya nimesaidiwa na kweli sasa nimepona, na niko ok kwenye service ili na wewe uguswe uende kupata msaada, lakini hutaki unaendelea kufanya siri.

Mwisho mkeo anaana kupata wasiwasi kwa sababu ya time ya female fertility ina age limit, hivyo na kwenye idara hiyo naamua kusaidia, mkeo ana conceive, na sasa mna watoto wawili and its a happy family, masimango kwa mkeo yamekwisha, wewe unasijikia kidume, na family friendship inaendelea.

Jee ni busara kuusema ukweli?, nikueleze mimi ndie ninayemtosheleza mkeo na hao watoto sio wa kwako ni wangu?, jee ukweli huo unasaidia?!.

The Political Reality.
Its an open secret kuwa Tanzania bado tuna demokrasia changa, hivyo political capitalization is an order of the day. Lakini ili kupata political mileage, ni lazima kutangaza kila kitu unachokisikia kuhusu nchi yako?.

Mfano kwenye hili la kukamatwa kwa ndege yetu, Kama Mhe. Tundu Lisu kama Rais wa TLS, baada ya kulipata hilo, kama angetafuta a chance kuomba appointment kumuona Magufuli na kumshauri how TLS can help badala ya kuitisha press conference na kulitangaza, ni wapi angepata more political mileage?.

Kuna mangapi ya CCM, CUF, Chadema na vyama, au ya watu, sisi watu wa the fourth estate tunayajua na tumeyakalia kimya kwa sababu hayajengi?. Kama kila mtu angekuwa anasema kila ukweli aliousikia, jee tungekuwa ni watu wa taifa la namna gani?.

Nchi ni Kama Nyumba, na Nyumba Pia Ina Mitaa Yake, Kuna Siri za Nyumbani, Chumbani, Jikoni Etc.
Nchi ni kama nyumba, taasisi ya kwanza ya jamii ni familia, kuna siri za familia, kuna siri za nyumbani, kuna siri za jikoni, kuna siri za chumbani, kuna siri kwenye handbags za wake zetu, kuna siri za vijeluba, kuna siri za simu, atc etc, sio busara kila ukweli kuhusu familia yako kuutoa nje ya familia, vivyo hivyo na nchi ni kama nyumba, ni kama familia, kuna vitu unaweza kusikia kuhusu nchi yako, na vikawa ni vitu vya kweli kabisa, lakini ukiongozwa na uzalendo (patriotism), na utaifa, (nationalism), hivyo kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, unaweza kuvisikia vitu hivyo vya kweli kabisa na kuamua kuvikalia kimya, kutovitangaza, bali kuvifanyia kazi kimya kimya na ukimya huu ndio uzalendo wenyewe.

Rais Japo ni Mtumishi Wetu, Ndiye Mkuu wa Nchi, Ni Kama Baba wa Familia, Aheshimiwe
Moja ya sifa za uandishi mzuri wa habari, ni assertiveness na persistence, yaani unatafuta habari kwa nguvu, na anakuwa kinganganizi kupata majibu, siku ile nilipoalikwa ikulu, ilinibidi kufanya persistence measures kupata nafasi ya kuuliza swali, na nilipo ipata hiyo nafasi, niliuliza maswali mawili, hakuna hata swali moja lililojibiwa vema, swali la kwanza lilifinyangwa finywangwa, swali la pili lilikwepwa jumla!,

Nilipaswa kuwa persistence kwa kumwambia Mhe. Rais hujajibu swali!, lakini kwa kuzingatia huyu ndiye mkuu wa nchi yetu, ni kama baba kwenye familia, licha ya kutokujibu maswali yangu, sikuwa kinganganizi kulazimisha yajibiwe nilinyamaza kwa heshima na unyenyekevu, wala sio kwa uoga, ila wanaojua wanajua kuwa rais Magufuli hakujibu maswali yangu, lakini naamini hata yeye mwenyewe anajua kuwa hakujibu, lakini kwa heshima na unyenyekevu, unakubali yaishe.

Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli | Page ...
Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo... | Page 9 | JamiiForums ...

Hii Kamata Kamata ya Kila Waompinga Magufuli, Ni Magufuli Anawatuma au Polisi Wanajipendekeza Tuu?.
My honest opinion, ingawa ni kweli rais Magufuli hapendi critics, mimi nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu toka kwenye kinywa chake na sio kwa kuhadithiwa, alisema anapenda challenge, ila hizo challenge ziwe ni ukosoaji wa kweli wenye nia njema, hivyo naamini hizi kamata kamata zinazoendelea za kuwakamata karibu kila wanasiasa wanaompinga rais Magufuli, siamini kama ni Magufuli anawatuma!, naamini hivyo ni kazi ya polisi wetu ambao wana jikomba komba tuu ili kuonekana wanafanya kazi.

Kwenye siasa za multipartisim duniani kote, kazi ya the opposition ni kupinga, kuopose kila kitu kinachofanywa na chama tawala hata kiwe ni kitu kizuri namna gani!, that is their right, kupinga, ndio maana wanaitwa wapinzani. Na serikali zote zinazoheshimu demokrasia ya kweli, lazima zikubali kupingwa.

Nimeishi kidogo UK, US, na Uswiss. Uingereza pale Times Squire karibu kila siku ni maandamano. US ule mtaa jirani na Capitol Hill kuna uwanja unakuwa huru kupinga chochote, Uswiss uwanja huru wa kupinga, ni pale uwanja wa wazi nje ya ukumbi wa Bunge, the The Bundes House. Hivyo sioni mantiki ya sababu zozote wanaompinga rais kubughudhiwa!, this is not democracy, Tanzania sio nchi ya kidikiteta!, tena kiukweli, kama katiba yetu imeruhusu mikutano na maandamano, hakuna any justified reasons at all za rais Magufuli kupiga marufuku, ni ukiukwaji wa wazi wa katiba ya JMT, but to be honest, yeye kama rais wa JMT kwa mujibu wa katiba yetu, hana mamlaka ya kuzuia jambo lililoruhusiwa na katiba, and he gas nothing to loose akiruhusu mikutano na maandamano.

Wito kwa IGP, Kamanda Sirro, controll vijana wako watekeleze majukumu yao kwa sheria taratibu na kanuni na sio kwa kutaka kujipendekeza au kujikomba komba!.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti ...


Jee Wapinzani Kazi yao ni Kupinga Tuu Kila Kitu au Kukosoa Tuu Hakuna Kupongeza Hata kwa Mazuri?.
Japo kazi ya upinzani ni kupinga na kukosoa, lakini tunapokuja kwenye issues muhimu kwa maslahi ya taifa, maslahi yataifa ndio yanatangulizwa mbele, sisi sote kama Watanzania, we stand as one, tunakuwa kitu kimoja, tunakuwa watu wamoja, tunaweka mbembeni tofauti zetu za kisiasa, hakuna tena siasa za vyama, wala siasa za watu, tunaweka pembeni siasa, tunaitanguliza mbele Tanzania, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, we stand as one, na kila kitu kinafuatia baadae.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...
Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El ...


Mfano mwingine wa kuujua ukweli fulani na kutousema ni ukweli huu nilio uandika kuhusu Bunge letu tukufu. Kwanza niliandika Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?, kisha nikaandika Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? Bunge likakasirika, nikaitwa Bungeni kuhojiwa na Kamati Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge nilihojiwa Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge na baada ya mahojiano, Bunge walinyamaza kimya, na mimi kuna ukweli niliwaambia ukawaingia wakanyama kimya na mimi sikuwahi kusema kilitokea nini kule , nimenyaza mpaka leo mpaka kesho, kwasababu sio lazima kila ukweli usemwe, ukweli mwingine ukijulikana ni aibu!. Ukweli mwingine una bagaza, na hausaidii chochote!.

Hata lile tukio la Machi 17, kuna watu tunajua lilitokea lini na Jamaa alichomoka kwa ugonjwa gani!, lakini kwa vile tumetangaziwa ni tarehe 17 na ugonjwa ni ule, japo ukweli tunaujua, lakini hatuusemi!. Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?
Conclusion
Namalizia kwa haya maswali ya msingi, kuhusu ni hoja za morality kusema kweli daima, lakini je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia?. Kwenye medani za siasa, kabla ya kuusema ukweli tunaousikia, je tutangulize kwanza mbele maslahi mapana ya taifa kwa kuupima kwanza, ukweli huo una matokeo gani, ndipo tuuseme, au tuendeleze kusema tuu, kupayuka na kuropoka kila ukisikia lolote, lisema tuu kwa sababu ni la kweli?. Je Ili kupata manufaa ya kisiasa, je ni lazima wanasiasa wetu, tupoliticise kila kitu?.
Wito wangu ni sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni cha kweli!, tujifunze kunyamaza, ukimya nao ni jibu!.

Wasalaam.

Paskali

Rejea.
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa ...
Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
Kitendo cha kuita nchi majirani zako kuwa ni "vinchi" ni uungwana ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hoja ya Udikiteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi ...
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio ...
 
walishasema kazi yao kuuu ni kupingapinga tu basi lakini nafikiri kuna haja ya kujitafakari sio kila kitu kuropokaropoka kuna issues nyingine ni too classified sio lazima Uzi disclose for political gain hii issue ni national matter against our enemy na wanatushangaa baadhi yetu kuwa upande wao
 
As long as UKWELI utahusiana na KODI ninayolipa basi lazima usemwe.Ukifanya baya lazima lisemwe.Ukifanya zuri litasemwa pia,kama linamakosa litakosolewa ili liwe zuri zaidi.

Hakuna mtu aliyempinga JPM kwenye issue za Madini aka Makinikia lakini onyo lilitolewa na wayfoward ili kuepuka malipo zaidi kama tuliyonayo leo ya madege yetu kutaka kupigwa mnada huko UGHAIBUNI.

Ukiwa kiongozi lazima ukubali kusikiliza hata kama hupendi kuusikiliza ukweli lazima uusikilize.

JPM hapendi kuambiwa ukweli anapenda kusifiwa tu hata anapoharibu.Na ili uapte cheo basi lazima umsifie ufanye anayofanya yeye,Ukinyanyasa wapinzani lazima upewe nafasi kubwa.

Akina Ndugai wanasubiria U-PM ndiyo sababu hata huko Bungeni wanafanya vihoja.Ukienda Mahakamani Mahakama ni Bubu sababu Jaji Mkuu anataka apewe ulaji kamili hivyo anajali tumbo kwanza hakuna haki,haki katafute Mbinguni.

Kama Taifa tumeishakufa tumebaki kama Makaburi yaliyopakwa chokaa.
 
Namalizia kwa haya maswali ya msingi, japo kuhusu ni hoja za morality kusema kweli daima, lakini Jee ni Lazima Kuusema Kila Ukweli Unaousikia?. Kwenye Medani za Siasa, Kabla ya Kuusema Ukweli Tunausikia, Jee Tutangulize Mbele Maslahi ya Taifa Kwa Kuupima Kwanza, Ukweli Huo Una Matokeo Gani, au Ukisikia Lolote, Lisema Tuu kwa Sababu ni la Ukweli?. Jee Ili Kupata Manufaa ya Kisiasa, Jee ni Lazima Wanasiasa Wetu, Tupoliticise Kila Kitu?.Sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni ni kweli!.

hahahahah..bado mnahangaika tu

Mnafanya maamuzi mabovu na kuingiza gharama nchi halafu mnataka wenye nchi yao wasijue????? uzwazwa huo
 
Nyakati fulani tuwe wa kweli, si kila ukweli ni lazima usemwe upenuni, tatizo linakuja pale ukweli unaposemwa chumbani na msema kweli, bado mtu anayeambiwa kweli hasikii wala kubadilika. Matokeo yake ni ukweli huo au siri hizo kutoka nje. Hasa hasa kama ukweli huo au siri hizo au jambo hilo linaumiza wengine ambao hawakustahili huku likiwaacha wengine wakifaidi kwa majivuno na tambo kubwa kana kwamba ni malaika, kumbe sivyo. Sasa wewe ambae ulipoambiwa ukweli mlipokuwa wawili au chumbani tena sio mara moja au mbili na ukagoma kuupokea, unatarajia mwonyaji au msema ukweli afanye nini zaidi ya kupiga panda hadharani labda utashtuka akifanya hivyo. Na kweli wabishi wengi jambo likitoka nje utawaona reactions zao tu .........! Hawajikiti kwenye kujibu hoja bali hu-deal na mtoa hoja!
 
"Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko" - ahadi ya/za mwanaTANU/CCM ambazo tulifundishwa tangu shule. Ni muhimu sana kukumbushana ahadi hizi hususan kuwakumbusha ahadi zao hizo. Tena siku hizi imeboreshwa zaidi - "MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU", naam Mungu na akawe shahidi wa haya tusemayo.
 
Paskal,
Naamini umetumia muda kuandika waraka huu lakini kuna makosa madogo madogo,ndio ubinadamu.
Andiko lako lote limeshindwa kuleta rejea zenye maana kuhusiana na hasa ulichodhamiria,morality katika kuelezea ukweli!!
Washiriki wakuu wa andiko lako ni serikali iliyoko madarakani na upinzani lakini umeshahu kuwa kashfa zote kubwa ambazo zingine zimetuvua nguo mpaka kumgusa mkuu wa nchi (mgao wa Escrow uliingia Ikulu,Suit za kifahari...) zilizungumzwa na upinzani.
Sijawasikia wapinzani wakiuliza kwa nini tumenunua vifaru vya Urusi kuliko vya Marekani au makombora ya kudungulia ndege yamepitwa na wakati,naamini wanaijua mipaka hayo.
Katika andiko lako hili umeweka rangi (kumpamba) Mkuu kuwa ulimsikia akisema anapenda challenge lakini naomba nikuulize kuwa baada ya kumsikia vipi matendo yake?
Kama kweli napenda challenge na hafurahii yanayotokea mbona hajakemea mpaka leo?Mikutano yake yote inaanza na kuhimiza amani na umoja lakini mwishowe ni vijembe na vittisho.
Twende kazi,ndio kwetu hapa na JPM ndiye Raisi wetu!!!
 
Back
Top Bottom