Maoni yangu ni kwamba inabidi tuelewe vizuri na tukubaliane, nini hasa maana ya MASLAHI YA TAIFA. shida iko hapo. kwa upande wa watawala wetu, maslahi ya taifa ni maslahi yao. maslahi ya CCM ndiyo maslahi ya taifa. Full Stop. sasa shida inaanzia hapo. Chukulia suala la Lissu na Bombadia iliyokamatwa. Hoja ya Lissu ilikuwa ni kwamba Taifa linapelekwa kwenye hatari kubwa ya kuvunja ovyo mikataba, hali ambayo itapelekea tulipishwe faini kubwa na nyingi, na hii inaathiri kwa kiasi kikubwa MASLAHI YA TAIFA. Lissu alijenga hoja yake katika kauli ya Waziri wa Sheria na Katiba, Prof. Kabudi, na Waziri wa habari nk., Dr. Mwakyembe, ambaye pia ni mwanasheria nguli. hawa walisema bungeni, baada ya hoja za Lissu kuhusu tahadhari kwa maamuzi ya serikali mintarafu mikataba, kwamba Tanzania ni Sovereign State, na kwa hiyo hatuwezi kuogopa kuvunja mikataba. Lissu alitahadharisha kwamba hii kauli ni Reckless na haina umakini wala weledi, hasa ikitoka kwa wanasheria nguli. kwa hiyo hoja ya Lissu iko wazi sana, kwamba anatetea MASLAHI YA TAIFA. Ilibidi aseme wazi kwa sababu kuna ajenda ya watawala ambayo wanaipigia kelele nyingi sana kwa kutumia vyombo vyao vyenye nguvu. sasa Tundu Lissu ni mtu mmoja tu, tena asiye na nguvu kama Dola. ilibidi apige kelele namna ile ili taifa lisikie.
Watawala katika jitihada za kumzima Lissu, kuwafanya wananchi wasimsikilize, wakampaka rangi ya kukosa uzalendo, kutojali maslahi ya taifa, na kufurahia matatizo ya nchi. hii ni propaganda ambayo wenye akili wanatarajiwa kuiona na kuiweka wazi. Aliyesababisha hasara hii kubwa kwa taifa, ndiyo huyo ambaye sasa hivi ndiye Rais wetu. ameingia kwenye mzozo mkubwa na wapinzani, kutokana na njia zake ambazo siyo za kikatiba, na kinyume cha sheria na kanuni za vyama vingi, na pia anatumia nguvu za Dola kuwabana, kuwatesa na kuwanyanyasa wapinzani. haya yote yanatakiwa kutiliwa maanani, namna nyingine tutakuwa tunacheza ngoma za wapika propaganda.
Kwa hiyo suala la Morality lina nafasi yake, lakini morality hapa ni kuwaumbua watawala, kuwaweka mbali na kile kinachoitwa MASLAHI YA TAIFA. kama kweli maslahi ya taifa yangewekwa mbele, tusingeshuhudia bomoa bomoa inayoendelea hivi sasa katika barabara ya kimara - kiluvya, kwa mtindo huu, tena kinyume na maamuzi ya mahakama.
MASLAHI YA TAIFA ni kujua ni kwa vigezo gani Magufuli alivunja mkataba ule, ukweli uwekwe wazi kabisa, siyo kuficha ficha eti kwa sababu Magufuli ni Rais. inabidi tufanye kama kule Israel, ambapo mtawala anaweza kushitakiwa wakati wowote. kumfanya mtawala kuwa nusu mungu ni kunajisi maslahi ya taifa na siyo moral.